Pages

 

Thursday, May 17, 2012

MAREKANI YARUHUSU DAWA MPYA YA KUZUIA UKIMWI IANZE KUTUMIKA

0 comments
MAMLAKA ya Chakula na Dawa ya Marekani (FDA), imeidhinisha dawa ya Truvada kuwa tiba ya kuzuia kuenea kwa Virusi Vya Ukimwi (VVU).Dawa hiyo ambayo awali ilikuwa katika kundi la zile zinazotumiwa kwa ajili ya Kupunguza Makali ya VVU (ARV), imepandishwa chati wakati ambapo tayari ipo sokoni ikiuzwa kama moja ya ARV za kawaida.

Kwa mujibu wa maelezo ya FDA, mwathirika anayetumia dawa hiyo anaweza kujamiiana na mwenza wake ambaye hana VVU bila kutumia kondomu na hatomuambikiza.

Matokeo ya utafiti huo yaliwahi kuchapishwa kwenye gazeti hili toleo la Februari 12, mwaka huu na sasa kilichofanyika ni FDA kuidhinisha Truvada ambayo ilionyesha kufanya kazi vizuri ikilinganishwa na ARV nyingine.

Uidhinishaji wa dawa
Jopo la wanasayansi 22 wa FDA waliokutana Jijini Washington wiki iliyopita, walipitisha Truvada baada ya kupitia ripoti ya utafiti kuhusiana na ufanyaji kazi wa dawa za ARV.

Wanasayansi hao waliisifu dawa hiyo baada ya kuonekana kufanya kazi vizuri kwa watu waliopo kwenye hatari ya kuambukizana VVU kwa kasi zaidi.

Kwa namna dawa hiyo inavyofanya kazi, mwathirika akiitumia hawezi tena kumwambukiza mtu mwingine ambaye atashiriki naye tendo la ndoa bila kutumia kondomu.

Lakini, dawa hiyo masharti yake hayatofautiani na yale ya ARV kwani mtumiaji atapaswa kuitumia maisha yake yote ili kumwekea kinga asiwaambukize wengine na yeye aishi muda mrefu.

Kulingana na ripoti ya utafiti uliofanyika Marekani, dawa hiyo ina uwezo wa kuzuia maambukizi ya VVU hadi asilimia 90.Hata hivyo, kwa watu ambao wamekuwa wakitumia dawa holela hasa za ARV, hali imekuwa tofauti kwani Truvada imeonekana ikifanya kazi kwa kiwango cha asilimia 44 tu.

"Hii ni ishara kwamba kuna kundi la watu ambao dawa hiyo haitafanya kazi kikamilifu kutokana na mazingira ya matumizi ya dawa holela,"ilisema sehemu ya ripoti.

Hata hivyo, wanasayansi wanasema  tatizo hilo linafanyiwa uchunguzi ili kupata njia bora ya kukabiliana na tatizo hilo.

Faida ya Truvada
Wataalamu wameeleza kwamba itasaidia watu ambao wana VVU lakini, hawapendi kufanya tendo la ndoa kwa kutumia kondomu."Leo ni siku ya tukio la kuwasisimua wengi katika kuzuia maambukizi ya HIV,” alisema mmoja wa wataalamu kutoka Taasisi ya kujitolea kusaidia jamii ya Fenway, Dk Kenneth Mayer ambaye alikuwa miongoni mwa wajumbe wa FDA walioipitisha dawa hiyo.

"Ingawa (Truvada) haikuweza kuonyesha uwezo wa asilimia 100 kuzuia maambukizi ya VVU, namna inavyofanya kazi itakuwa na matokeo mazuri ya kupambana na Ukimwi duniani,” alisema Dk Mayer.

Tahadhari
Hata hivyo, wataalamu hao walihimiza kuwepo kwa uchunguzi zaidi wa kitafiti ili kujua kama Truvada itafanya kazi vizuri duniani kote.Mtaalamu wa Dawa kutoka Taasisi ya Taifa ya Saratani nchini Marekani (NCI),  Dk Lauren Wood alilalamika akisema kuwa utafiti huo haukuzingatia matatizo ya figo.

Alisema matatizo ya figo yamekuwa yakijitokeza kwa waathirika wengi wa Ukimwi hasa barani Afrika."Mimi sikufurahishwa sana kwa sababu utafiti huu haukuzingatia maeneo ambayo watu wengi wako kwenye hatari ya maambukizi,” alisema Dk Wood.

Lakini, alisema utafiti uliofanyika nchini Marekani umeonyesha wazi kwamba ni dawa inayoweza kupunguza kwa kiwango kikubwa kasi ya kusambaa kwa VVU.

Wataalamu kadha nao walisema pamoja na Truvada kupitishwa na FDA, ni lazima maelezo ya kitaalamu yatolewe kwa madaktari ili wawe na uelewa wa kutosha kuhusu matumizi yake.

Mabingwa hao walipendekeza kwamba, wanaotumia kabla ya kuruhusiwa kutembea na wenzi wao bila kondomu lazima wachunguzwe kitaalamu ili wajulikane kama dawa iyo imewakubali au la.

Mwanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Afya cha Cincinnati, Dk Judith Feinberg alikosoa ripoti ya uchunguzi akisema ilipaswa kwenda mbali zaidi katika kuchunguza madhara yanayoweza kujitokeza kwenye matumizi ya dawa hiyo.“Tusipokuwa makini katika hilo, tunaweza tukawa tumepitisha jambo ambalo litasababisha madhara zaidi kuliko faida,” alionya Dk Feinberg.


Utafiti wa ARV
Wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Johns Hopkins ni miongoni mwa wale ambao walifanya uchunguzi juu ya ARV, kuwa moja ya dawa zinazopunguza maambukizi ya VVU.

Watafiti hao walibainisha kuwa wale wanaotumia ARV baada ya muda fulani, huweza kushiriki tendo la ndoa bila ya kutumia kondomu na mtu ambaye hana VVU na asimwambukize kwa asilimia 95.

Mkuu wa Mtandao wa Maabara za Kuchunguza VVU katika chuo hicho, Profesa Susan Eshleman alisema kwenye ripoti ya ugunduzi huo, wamebaini dawa za kurefusha maisha kwa waathirika wa HIV, sasa zinaweza kutumika kama sehemu ya kuzuia maambukizi.

Profesa Eshleman alisema kwamba, mwathirika wa VVU anayetumia ARV kikamilifu, anaweza kujamiiana na mtu ambaye hana virusi bila kondomu na asimwambukize.

“Huu ni ugunduzi wa kustajabisha,” alisema Profesa Eshleman akifafanua: “Matokeo haya yameleta mapambazuko mapya katika sayansi ya kuzuia maambukizi na inawaweka watafiti kwenye mazingira mazuri zaidi ya kupata suluhisho la kukabiliana na maradhi haya.”

Walivyogundua
Profesa Eshleman anasema utafiti huo walioupa jina la HPTN 052, walifanya kupitia maeneo mbalimbali ya dunia.

Kwenye ripoti hiyo ambayo pia ilichapishwa kwenye jarida maarufu la kisayansi linaloitwa Science, watafiti hao walisema mtu anapotumia ARV, hufikia wakati fulani wingi wa virusi mwilini hupotea kiasi kwamba anakuwa karibu sawa na yule ambaye hajaambukizwa.

“Jambo la msingi katika utafiti huu ni kwamba dawa hizi za kurefusha maisha zinapotumiwa kikamilifu, hupunguza mzigo wa virusi mwilini kwa zaidi ya mara 200. Ni sawa na kusema inapunguza hadi kufikia karibu na sifuri,” inaeleza ripoti hiyo.

Ni katika mazingira hayo, ripoti hiyo inasema kuwa damu ya mwathirika inakuwa haina virusi na hivyo uwezekano wa kumuambukiza mpenzi wake unakuwa haupo.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa ARV inafanya kazi mbili, kwanza kurefusha maisha ya mwathirika kwa kupunguza virusi mwilini na pili ni kumkinga asiambukize wengine.Sifa nyingine ya ARV, alisema ni kupunguza uwezekano wa waathirika kupata ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) kutokana na kiwango cha kinga za mwili kuongezeka.
SOURCE: mwananchi.co.tz
Read more...

BOY FINDS HUMAN FINGER IN HIS SANDWICH!

0 comments
Ryan Hart, a 14-year-old boy from Jackson, Michigan, had a rude surprise when he bit into his Arby's roast beef sandwich. "I was like, 'that's got to be a finger,'" he told reporters. "It was just nasty."
Reportedly, a restaurant employee cut off her finger with a meat slicer while preparing the meal. She left her station to deal with the emergency, and other employees, who were unaware of the injury, continued to complete the order.
"Somebody loses a finger and you keep sending food out the window," said the teen's mom, Jamie Vail. "I can't believe that." She added that following the gruesome discovery, her son was "traumatized," couldn't eat or sleep, and had been prescribed medication.
Ryan Hart
John Gray, Arby's vice president of corporate communications, gave the official Arby's statement:

"Arby’s wants to reassure customers, we are committed to providing quality food in a safe and healthy environment
We are deeply concerned and apologetic to the guest involved in this unfortunate incident. This is an isolated and unfortunate accident occurred in a franchisee’s Jackson, Michigan restaurant in which an employee was injured.
After learning of the incident, the franchisee’s restaurant team shut down food production and thoroughly cleaned and sanitized the restaurant. The franchisee fully cooperated with the Health Department during the investigation, and the restaurant was given the approval to remain open."

This is not the first time human remains have been found in a fast food meal but this case might be the most extreme.
•    A Dayton Ohio man sued Arby's in 2005 for serving his chicken sandwich with human skin on top.
•    An Albany-area man found a bandage with blood on it in his pizza crust at Pizza Hut last year
•    Also in 2011, Texan woman found blood on her French fries at a Houston area Crackle Barrel.
Read more...

LULU ANAUMWA

0 comments
Elizabeth ` LULU` Michael

Habari  zinaeleza kuwa staa wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amekwaa gonjwa baya akiwa mahabusu katika Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam.

Akizungumza  baada ya kuonekana kwenye duka moja  linalouza madawa ya binadamu,  Kinondoni, hivi karibuni, rafiki wa karibu wa Lulu alisema kuwa alikuja kununua dawa za kumpelekea Lulu gerezani kwa kuwa amepatwa na ugonjwa unaomshambulia sehemu nyeti wa Urinary Tract Infections (U.T.I).

“Namchukulia Lizzy (Lulu) dawa, amepata U.T.I, si unajua mazingira ya usafi kwenye vyoo vya gerezani? Ni rahisi sana mtu kupata au kuambukizwa U.T.I kwa sababu ni vyoo vya public (vinavyotumiwa na watu wengi),” alisema rafiki huyo ambaye huwa  gerezani hapo mara kwa mara.

  Lulu  anaendelea vizuri huku hofu kubwa ikiwa kwenye ujauzito wake kuhofiwa usije   kutoka.

Lulu yupo ndani ya mahabusu ya Segerea kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha msanii mwenzake Steven Kanumba na atafikishwa tena mahakamani  Jumatatu hii.



Read more...

SAUDI MILLIONAIRE BUYS A BOTTLE OF WINE FOR $136,000

0 comments
A Saudi millionaire splurged $136,000 on a bottle of champagneat Dubai’s glitzy Cavalli club over the weekend, a UAE newspaper reported on Tuesday.
“The Saudi Arabian and his friends guzzled” a bottle of Louis Roederer Cristal in the early hours of Saturday morning, the 7DAYS newspaper said.
The vintage bottle was “one of just three believed to be available worldwide,” the paper added. The other two were for sale at nightclubs in New York and London.
According to 7DAYS, the Cristal bottle was from a “batch made in 1990 in Champagne, France,” originally intended for the Millenium celebrations.
Club’s manager David Lescarret would not divulge the Saudi’s total bill for the night, saying only that it was “very high” and included a “luxurious dinner.”
The manager said the Cavalli club bought the champagne at a Christie’s auction house in London at a cost of around $93,000.
Read more...

MAFISANGO KUAGWA LEO,RAGE AELEZA KILICHOTOKEA

0 comments
Hili ndio gari alilopata nalo ajali marehemu Mafisango

Leo Ijumaa watu watapata fursa ya kuuaga mwili wa marehemu Patrick Mafisango kwenye  viwanja vya TCC Club Chang'ombe jijini Dar es Salaam. kuanzia saa nne asubuhi (awali ilikuwa imepangwa mwili uagwe katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni) . Taarifa zilizotolewa baadaye na msemaji wa familia zimetaarifu kuwa mwili wa marehemu Patrick utasafirishwa na ndege ya saa kumi tayari kwa kuzikwa katika mji aliozaliwa wa Kinshasa huko nchini Congo DRC (awali taarifa zilizotolewa na meneja wa Simba Nico Nyagawa zilizema mwili wa Mafisango baada ya kuagwa utaondoka na kusafirishwa na ndege ya shirika la KQ kuelekea kwao Rwanda kwa ajili ya kuzikwa).

Anaelia ni mmoja wamarafiki wa marehemu Mafisango ambao alikuwa nao ndani ya gari



Haruna Moshi `BOBAN` akilia kwa uchungu jana msibani
 Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, marehemu Patrick alipata ajali alfajiri ya kuamkia jana Alhamisi katika maeneno ya TAZARA alipokuwa akiendesha gari na kutaka kuziwahi taa za kuongozea barabara na ndipo alipokutana na mwendesha pikipiki (taarifa nyingine zinasema ni mwendesha baiskeli ya matairi matatu - guta) na katika harakati za kujaribu kumkwepa kwa bahati mbaya gari lake lilikosa uelekeo na kugonga mti kisha kuingia mtaroni na kusababisha ajali iliyomwacha na majeraha makubwa.
BOBAN na wenzake wakiwa msibani

Ndani ya gari hilo inasemekana alikuwa ameambatana na mdogo wake pamoja na rafiki zake wakirejea kutoka kwenye klabu ya starehe. Patrick aliaga dunia muda mfupi baadaye alipokuwa akiwahishwa hospitalini. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam na maombolezo ya msiba yapo kwenye nyumba iliyopo maeneo ya Keko Toroli jirani na kituo cha Chang’ombe Maduka Mawili (Njia Panda ya Sigara).

Patrick alijiunga kuichezea Simba SC mwaka jana, akitokea timu ya Azam FC aliyojiunga nayo alipohamia nchini Tanzania miaka mitatu iliyopita. Awali alkuwa akiichezea APR ya Rwanda. Video za baadhi ya magoli aliyowahi kufunga zipo youtube.

Akina mama ambao ni washabiki wa marehemu Mafisango wakilia kwa huzuni msibani jana
 Patrick alizaliwa tarehe 9 Machi 1980 mjini Kinshasa, Kongo D.R.C lakini alikuwa na uraia wa Rwanda

Amefariki siku chache tu baada ya kocha wa timu ta taifa ya Rwanda, Milutin Sredojovik (Micho) kumuita kujumuika katika timu ya Taifa ya nchi hiyo kwa ajili ya maandalizi ya mechi za kuwania kufuzu kucheza kombe la dunia 2014.
Read more...

Wednesday, May 16, 2012

PATRICK MAFISANGO WA SIMBA SC AFARIKI DUNIA KWA AJALI ALFAJIRI YA KUAMKIA LEO

0 comments
MCHEZAJI Patrick Mafisango wa timu ya Simba ya Dar es Salaam amefariki dunia leo kwa ajali ya gari katika eneo la Tazara jijini Dar es Salaam. Taarifa ambazo zimetolewa kutoka Klabu ya Simba zimesema Mafisango amefariki dunia leo asubuhi kwa ajali ya gari maeneo ya Tazara. Mtandao huu utawaletea taarifa zaidi za tukio hilo muda mfupi baadaye. Mtandao huu pia unatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na klabu nzima ya Simba kwa pigo hilo.
Read more...

Tuesday, May 15, 2012

MARA BAADA YA KUFIKA INDIA WASTARA AONGELEA TATIZO LILILOJITOKEZA

0 comments
Wastara wakati akichangisha hela ya matibabu ya Sajuki katika kipindi cha Leo Tena cha Clouds Fm

Wastara,Mke wa msanii wa filam za kibongo,Juma `Sajuki`Kilowoko aliongea katika kipindi cha `Leo Tena` na Dina Marios kwa njia ya simu moja kwa moja kutoka India ambako Sajuki ameenda kwa ajili ya matibabu.Dina ameyaweka maongezi hayo kwenye blog yake ya dinamarios.blogspot.com.Haya ndio maongezi yao:
SOURCE:www.dinamarios.blogspot.com
Read more...

Katherine Jackson Discuss Conrad Murray, Says He’s Not Serving Enough Jail Time

0 comments
Katherine has said that she’s never met Dr Murray nor, to her knowledge, has he ever reached out to meet her.  And she’s also expressed her feelings on his sentence, noting that she doesn’t think four years is long enough.  You can tell this will be a really emotional interview; she appears sad and teary eyed throughout the entire clip.
Read more...

PICHANI LIVE! KIJANA ALIVYOBAMBWA UBUNGO AKICHUNA MBWA KWA AJILI YA BIASHARA YA MISHIKAKI

0 comments
PICHA KUTOKA THE CHOICE TZ
Read more...
 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797