Pages

 

Sunday, June 24, 2012

NAIBU WAZIRI AIBUKA NA KUKANUSHA KUFUMANIWA

0 comments
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mh. George Simbachawene(Mb)
Jana ziliibuka na kuenea habari za Naibu Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene kuwa alifumaniwa na mke wa askri huko Singida katika hoteli maarufu mjini humo ya Aqua.

NAIBU Waziri  ameibuka na kukanusha vikali uvumi mbele ya waandishi wa habari mjini Karatu jana jioni, Simbachawene ambaye pia ni Mbunge Kibakwe (CCM) mkoani Dodoma, alisema habari hizo ni uongo na kudai kuwa zimeenezwa na baadhi ya wabunge wa Chadema aliokutana nao mjini Singida jana wakati akiwa njiani kwenda msibani Karatu.

Alisema kuwa katika hoteli aliyofikia, kuna mtu alifumaniwa akiwa na mke wa askari na kufafanua kuwa watu walizua jambo hilo kwa kuwa naye alilala katika hoteli hiyo.

“ ...ukweli ni kwamba jambo hilo halijanitokea. Mimi nilifika hapa jana (juzi) nikitokea Dodoma kuelekea Karatu kuhudhuria msiba wa shemeji yangu,” alisema Simbachawene.

Aliwataja watu wanaodaiwa kueneza uvumi huo hizo kuwa ni wanachama wanane wa Chadema akiwemo Mbunge wa Viti Maalumu kupitia chama hicho, Christina Lissu.

“Baada ya kufika Singida nilikwenda katika baa moja na kuwakuta wabunge wa Chadema na baadhi ya wanachama, nilipata kinywaji na kurudi hotelini kulala,” alisema Simbachawene.

Huku akivua shati kuwaonesha waandishi wa habari kwamba hakukatwa mapanga mikononi kama ilivyodaiwa, alisema kuwa alipoamka asubuhi ndipo alianza kusikia habari kuwa amefumaniwa na mke wa mtu.

Awali taarifa kutoka Singida zilizowekwa pia kwenye mitandao ya kijamii zilidai kuwa Naibu Waziri huyo alikumbwa na mkasa huo jana alfajiri.

Tukio hilo ambalo inaelezwa kuwa lilitoka majira ya saa kumi, baada ya taarifa hizo kumfikia mwenye mke, ilimlazimu mmiliki wa hoteli hiyo kutoa taarifa Polisi ili kuzuia maafa zaidi

Katika uvumi wa jana ilidaiwa kuwa baada ya taarifa hizo, iliwalazimu askari Polisi kwenda katika hoteli hiyo ili kumuokoa Simbachawene, ambaye tayari alikuwa amejeruhiwa mkono kwa sime na askari huyo mwenye mke.

Mara baada ya purukushani hizo katika eneo hilo, Naibu Waziri huyo alidaiwa kwenda kutoa taarifa katika kituo cha Polisi mkoani Singida, ambapo ilidaiwa kuwa katika maelezo yake aliandika jina la Josephat Joseph badala ya kutumia jina lake halisi.

Hata hivyo, Mbunge Christina Lissu, alisema anashangazwa na taarifa za yeye kuhusishwa kueneza uvumi huo.

Alisema walikutana na Naibu Waziri huyo, katika hoteli hiyo, wakiwa wanatoka mkoani Tabora katika kesi na wabunge wa Chadema, Conchesta Rwamlaza, Philipa Muturano na John Mrema ambaye ni Mkurugenze wa Bunge na Halmashauri ya chama hicho.

“ Tulipofika Singida nilimwona Simbachawene nilimwita jina, alitufuata na kutununulia vinywaji hapo hotelini,” alisema Lissu na kuongeza;

“Hata tulipofika hoteli, baada ya muda tukasikia kutoka kwa mmiliki wa hoteli akisema kuna watu wanataka kumharibia biashara. Tulipomuuliza kulikoni? Akasema kwani hamna habari si mmewaona Polisi wakati mnaingia hapa, huku akisema kuna kigogo wa Serikali amefumaniwa na mke wa askari.”

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Linus Sinzumw alipoulizw alisema, hakuna tukio kama hilo lililotokea mjini Singida wala mahali popote katika mkoa huo.
“Huo ni uzushi tu, hakuna tukio hilo mjini Singida na wala sijasikia taarifa zozote za aina hiyo kutoka maeneo mengine mkoani hapa, alisema Sinzumwa.

UNAWEZA KUCHUNGULIA NA HII 
Read more...

Saturday, June 23, 2012

BREAKING NEWS:NAIBU WAZIRI AFUMANIWA NA MKE WA MTU LEO

0 comments
Kuna habari kutoka Singida zinasema NAIBU WAZIRI.. (JINA LIMEHIFADHIWA) amefumaniwa akiwa na mke wa mtu (mke wa askari mmoja) pale Singida katika Hotel ya Aqua. 
 
.Kwa mujibu wa Blog ya The Choice  amefumaniwa  saa 10 alfajiri. Baada ya kupata tip hiyo, maaskari walikwenda wakazingira hotel hiyo, wakati WAZIRI HUYO akitoka yule askari mwenye mke kumbe alikuwa ameficha sime/panga akamkata Mheshimiwa Naibu Waziri.


Habari zinasema alikuwa yuko njiani kwenda msibani ukweni kwake, Karatu. Hata wakati wa kupiga kura jana jioni hakuwepo bungeni, akiaga kuwa anawahi msibani.
Habari zaidi zitawajia kadri nitakavyozinasa
Read more...

Friday, June 22, 2012

MNYIKA AELEZA SABABU YA KUOMBA MUONGOZO SAKATA LA MADAKTARI BUNGENI LEO

0 comments

Lengo la Kuomba Mwongozo - Sakata la Madaktari

Kwanini niliomba muongozo-Sakata la Mgomo wa Madaktari

Leo nilitaka kuomba muongozo wa Spika kwa mujibu wa Kanuni 49 (2) baada ya Waziri wa Afya kutoa kauli juu ya utekelezaji wa madai ya madaktari. Kanuni hiyo inataka kauli isiwe ya kuzua mjadala lakini aliyoyaeleza waziri juu ya uboreshaji wa maslahi ya madaktari yanazua mjadala kwa kuwa yanatofautiana na majibu ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliyoyatoa bungeni jana, (Juni 21, 2012) na pia hayana uhalisi. Mathalani, wakati serikali ikidai imeongeza posho ya kuitwa kazini (on call allowance) toka Februari, 2012 na kutumia bilioni 7.9 kwa miezi michache, imetenga kwa watumishi wa Afya bilioni 18.9 tu kwa mwaka mzima wa 2012/2013 kiwango ambacho hakitoshi.


Hivyo nilitaka kuomba muongozo Spika awezeshe kauli hiyo ijadiliwe kama ilivyokuwa kwa kauli juu ya fedha za rada. Nakusudia kumuandikia barua Spika kushauri aelekeze kamati ya bunge ya huduma za jamii kauli hiyo ya waziri.


Pia bunge halipaswi kunyimwa fursa ya kutumia mamlaka yake kwa mujibu wa ibara ya 63 ya kuishauri na kuisimamia serikali kusuluhisha mgogoro na madaktari ili kuepusha mgomo wenye athari kwa nchi na wananchi kwa kisingizio cha kusudio la serikali kupeleka mgogoro mahakama kuu kwa kuwa mpaka leo taarifa iliyotolewa bungeni bado hakuna shauri katika kitengo cha kazi. Hivyo, Spika anapaswa kutoa jukumu kwa kamati husika ya bunge kuendelea na usuluhishi kabla ya serikali kukimbilia mahakamani.


Wabunge tupewe nakala ya taarifa ya majadiliano ya pande mbili yaliyochukua zaidi ya siku 90 badala ya kupewa hotuba ya nusu saa ya upande mmoja wa serikali pekee.


Hata serikali ikizuia mgomo wa wazi kwa zuio la kimahakama ieleweke kuwa mgomo wa chinichini kwa watumishi wa afya ambao una athari ya muda mrefu kwa maisha ya wananchi nchini.


Mwisho, serikali ipunguze matumizi yasiyo ya lazima na ipanue wigo wa mapato.


John John Mnyika.

Mbunge Jimbo la Ubungo (CHADEMA)
22 Juni, 2012
Read more...

KENYAN POLICE SEIZE INBOUND EXPLOSIVE SHIPMENTS IN MOMBASA

0 comments

Port of Mombasa in Kenya
According to Reuters, Kenyan police had arrested two Iranians after they seized chemicals they suspected were going to be used to make explosives in Mombasa, which has been hit by a series of attacks.

The port city, the capital Nairobi and other parts of Kenya have suffered a series of grenade attacks since Kenya sent troops into Somalia last year to try to crush al Shabaab insurgents it blames for a surge in violence and kidnappings threatening tourism in east Africa's biggest economy.

Police arrested the Iranians on Wednesday in Nairobi. On the same day, police impounded a container in Mombasa originating from Iraq and suspected to be carrying explosives.

On Thursday, police flew one of the suspects to Mombasa, where he led police to recover 15 kg of powder, which security experts took to their laboratory for testing.

"They are cooperating well. They are giving us key information that might help us reduce terrorist attacks in the country," Ambrose Munyasia, a senior police officer at the Coast region told Reuters.
"We want to find out whether these substances are linked to any terror groups, including al Shabaab, al Qaeda and any other group," Aggrey Adoli, Coast provincial police officer, added.

Francis Kimemia, Kenya's acting head of civil service who was in Mombasa, said the government had sought the help of international agencies such the FBI and Interpol in helping deal with security threats.
"We have been working with them in terms of identifying criminals. We cannot fight terrorism alone. You have to work with other partners and other state organs," he said.

In the most recent attack, a bomb exploded in a trading center in the heart of Nairobi in late May, wounding more than 30 people. One person later died from their injuries.
Gunmen also detonated grenades outside a nightclub in Mombasa in May, killing one person and wounding several others.

Al Shabaab seeks to impose a strict version of sharia, Islamic law. The group emerged as a force in 2006 as part of a movement that pushed U.S.-backed warlords out of Somalia's capital, Mogadishu.
At present it also has hundreds of foreign fighters in its ranks.
Read more...
 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797