Pages

 

Sunday, June 10, 2012

FLOYD MAYWEATHER SR. BELIEVES PACQUIAO WON LAST NIGHT FIGHT

0 comments
 Everyone has an opinion on who won the fight last night (sunday morning in Tanzania) and that includes Floyd Mayweather’s Dad, Floyd Mayweather Sr.  He spoke with a couple ESPN reporters last night after watching the Pacquiao/Bradley fight.  Check out who he thought won.... reporters tweeted

Read more...

AJALI YA NDEGE:WAZIRI SAITOTI AFARIKI DUNIA

0 comments
Hayati George Saitoti



Hayati Joshua Ojode

Waziri wa Usalama wa ndani wa Kenya Profesa George Saitoti na Naibu wake Orwa Ojode wamefariki dunia katika ajali ya helikopta ya polisi iliyotokea leo asubuhi katika eneo la Kibiku, karibu na mji wa Ngong takriban kilometa ishirini kutoka mji mkuu wa Nairobi.
Abiria wote sita, wakiwemo marubani wawili na walinzi wa mawaziri hao waliokuwa kwenye helikopta hiyo wamefariki dunia na miili yao kuteketezwa kwa kiasi cha kutoweza kutambulika.
Kilichosababisha ajali hiyo bado hakijajulikana

Kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Habari la Uingerza BBC waziri Saitoti na maafisa wengine wa juu katika wizara ya usalama wa ndani walikuwa wakielekea katika eneo la Sotik kwa mkutano unaohusu mambo ya usalama.

 Saitoti alikuwa miongoni mwa wanasiasa mashuhuri nchini Kenya waliokuwa wakipania kugombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao.

Walioshuhudia ajali hiyo wamesema waliona helikopta hiyo ikizunguka angani kabla ya kuanguka katika msitu wa Ngong.
Polisi wamezingira eneo la ajali hiyo na kamishna wa polisi Mathew Iteere aliyepo katika eneo la ajali anatarajiwa kutoa taarifa kamili kuhusiana na ajali hiyo.

Ajali hiyo ya helikopta imetokea katika siku ambapo Kenya inaadhimisha miaka minne tangu kutokea ajali ya ndege iliyowauwa mawaziri wengine wa serikali, Kipkalya Kones na Lorna Laboso

SOURCE: BBC.http://www.bbc.co.uk/swahili/habari
Read more...

Monday, June 4, 2012

WARAKA WA GODBLESS LEMA KWA RAIS KIKWETE HUU HAPA: "IKULU iliingilia kesi yangu ya Ubunge"

0 comments

“ Ndugu Wananchi;
 Napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi na shukrani nyingi kwa ndugu zetu wa Arusha kwa kuwapokea vizuri na kuwakarimu vyema wageni wetu hao. Nawaomba waendelee na moyo huo mpaka watakapoondoka wote. Naomba kuwepo kwa mkutano huu kuwakumbushe umuhimu wa mji wenu kuwa tulivu. Miaka miwili iliyopita isingekuwa rahisi kwa watu au shirika kubwa la kimataifa kama Benki hii kuamua kufanya mkutano wake Arusha. Isitoshe hata sisi wenyewe tusingeshawishika kuomba au kukubali maombi ya namna hiyo. Lakini sasa imewezekana. Naomba kila mmoja wetu aweke azimio moyoni mwake la kuhakikisha kuwa hali ile haijirudii tena. Nyota ya Geneva ya Afrika lazima iendelee kuangaza. Yaliyopita si ndwele tugange yajayo . ( J.K . KIKWETE.)
“Narudia tena , IKULU iliingilia kesi yangu ya Ubunge”.
Mh Rais nimekusikiliza kwa makini sana ila nakupa pole kwani bado unafikiri unaongea na Tanzania ya mwaka 1961 , umesema sasa Arusha ni shwari tofauti na miaka miwili iliyopita kwani sasa kuna amani na utulivu wa kutosha ndio maana hata mkutano wa AFDB umefanyika Arusha .
Mh Rais , najua IKULU iliingilia kesi yangu kama ilivyoonekana na ndio sababu hata Mkuu wa Mkoa wa Arusha wakati anaapisha Wakuu wa Wilaya alimpongeza Jaji kwa hukumu nzuri aliyowafurahisha wakati kesi hiyo iko mahakama ya Rufaa , lakini jambo moja la msingi ambalo huwezi kulitambua kwa sasa ni kuwa Haki na Ukweli haviwezi kushindwa na dhuluma, ubaya wala mamlaka , natambua wewe ni Rais na unayo mamalaka makubwa katika Taifa hili lakini vile vile nataka utambue kuwa huna mamlaka makubwa dhidi ya haki , utu na ukweli.
Mh Rais hakuna Amani Duniani inayozidi Haki na usawa ,utu na ukweli , haipo na wala haitakuwepo , ndio maana kila siku nasema ni “Afadhali Vita Inayotafuta Haki na usawa kuliko Amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa Mwanadamu “ umefurahia sana mkutano uliokupa fursa ya kutoa maneno ya kebehi na kudhihirisha ila chafu iliyofanywa na Serikali yako na kujaribu kuhadaa Umma kama ilivyo kawaida ya Serikali yako na Chama chako , hata hivyo wakati huu kuna mambo ya msingi yakushughulikia zaidi ya kebehi na hadaa , Uchumi wa Nchi umeyumba, huduma za msingi za jamii zimepuuzwa, Mpasuko katika suala la Muungano na vururugu zinazoendelea Zanzibar , mfumuko wa bei hizi ni sababu chache ambazo haziwezi kuruhusu wakati huu kuwa wakati wa kebehi na mizaha isipokuwa kazi .
Mh Rais , Mama Theresa , Nelson Mandela , Martin Luther Jr na Malcom X hawakuwa Wabunge kupigania haki za Nchi yao na watu wao , sihitaji Ubunge kupigania ukweli, haki na utu , nahitaji dhamira safi , nia njema na huu utakuwa wajibu wangu mpaka nakwenda kaburini , nitakapomaliza mbio hizi najua nitapata fursa ya kutazama nyuma yangu nione nini nilifanya , ukweli nisingependa kuona vituo vya mafuta , magorofa , magari na viwanja vingi kila kona ya Nchi bali Haki ,Usawa na utu vikiwa kama nguzo ya imani ya watawala wetu watakaokuwepo, pengine sitaishi miaka mingi sana kama utachukizwa sana na waraka wangu huu kwani Polisi , Usalama wa Taifa na Jeshi la Wananchi wanakutii wewe , hata hivyo siogopi kufa kwani nisipokufa kesho , nitakufa siku moja ambayo siijui , napenda kuishi maisha marefu nimwone mke wa mtoto wangu kama itawezekana , lakini kuliko iwezekane kwa kuishi kwa hofu ni bora ishindakane kwa kuthamini haki , kwa hiyo kama utakuwa umekasirika sana , unaweza kufanya jambo lolote baya kwa kutumia mamlaka yako , niko tiyari sio kesho wala leo isipokuwa sasa hivi, najua IKULU imewazulumu watu wa Arusha Mbunge wao.
Mh Rais ninajua wazi njama zote na hasira hizi zinaweza kuwa zimetokana hasa na mkutano tuliokaa Osterbay Dar mimi na wewe kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 hata hivyo sikupuuza maongezi yetu isipokuwa nilichagua kufuata dhamira yangu na wito wangu wa utumishi wa kweli katika Jimbo langu na Nchi yangu.
Mh Rais nimekuelewa na Wananchi wamekuelewa kila mahali , wewe ni Rais unayo mamlaka makubwa na mimi ni mwananchi mamlaka yangu makubwa ni kwa mke wangu tu , sina Polisi wala Usalama wa Taifa lakini nitawaomba wanyonge wafunge na kusali tuone kama mamlaka yako inaweza kushindana na haki na ukweli .
Mh Rais “Mtu anaweza kuzini kwa siri lakini hawezi kuugua ukimwi kwa siri” Serikali na Chama cha Mapinduzi kimepuuza watu na haki zao kwa muda mrefu , lakini wakati umefika ambapo hawatapuuzwa tena hata hivyo kwa kauli yako hii naamnini haiwezi kuwafundisha kazi majaji wa mahakama ya rufaa .
“ ONLY TIME WILL TELL”.
GODBLESS .J. LEMA.
Read more...

Saturday, June 2, 2012

ZANZIBAR UAMSHO `BUDDING NEW AL-SHABAAB`-TIPF WARNS

0 comments
Demonstrations was supposed to be peaceful until things came out of hand shortly afterwards. Here Uamsho senior leaders kick starting demonstration on the day of Zanzibar violence
Few days following last week Zanzibar violence, Tanzania Islamic Peace Foundation have urged government to take a closer look on the group Uamsho( THE AWAKENING)

Director of  TIPF Sheikh Sadik Godigodi was issuing the foundation`s statement condemning recent Zanzibar violence which saw arsonic acts against churches and looting

In its statement, the foundation expressed its concern that Uamsho has the same trend Somali extremist group Al-Shabaab had when it began. TIPF  also claimed to have full understanding of  religious movements in the island and refused to believe Uamsho denial that they are not responsible for the Zanzibar`s last week violence.TIPF see the violence as meaningless and abusive by damaging churches and looting shops because if nature of violence was political claims it is irony that religious and other non-political areas were involved.

Suspects being arrested during last week`s Zanzibar violence
Roads were blocked by rocks and bon fire until security forces interfered

Sheikh Godigodi said churches do not belong to neither goveenment nor any political party or NEC(National Electoral Commission) and TIPF understand that Uamsho was centered in organizing  open religious meetings aiming to providing islamic teachings to muslims and others interested people but they long  have been instilling hates instead


Muungano (the union of Tanganyika and Zanzibar) has been  strongly debated among Zanzibaris in recent years,questioning  interests of its being.The pact was installed by the then Tanganyika President late Mwalimu Nyerere and Zanzibar`s first president late Abeid Karume in late April of 1964,by mixing sands from either part.


Sheikh Godigodi urged Zanzibaris to realise that christianity and churches were run in the island since 1870,so they should stop questioning their elligibilities and connecting Zanzibar political problems with christianity.
Senior leaders of  Uamsho denying direct involvement in violence

"We,islams,know the history of Al-Shabaab.They set out by ignoring islamic teachings and installed their own ideas for their own interests under the shadow of islam."


He revealed that his foundation once had advised authorities to scrutinize movements of  Uamsho which they claimed was sowing discriminations within muslims in mosques.His foundation requested that government appoint a special committee to closely investigate the group, but the request had fallen into deaf ears.So they rested their case, warning that if anything serious happened,the government should not seek any excuse

Peace was restored in the island and tourists were back inthe streets of Zanzibar



Now the group has taken it all to the streets of  Zanzibar,chanting against Muungano while burning churches and looting along the way,shooing  mainlanders off the island, ignoring all constitutional principles set for any citizen to demonstrate their itching issues.

Sun is setting in Zanzibar
TIPF has also condemned individuals who have positioned themselves against Muungano citing that God Himself does not allow discrimination,racism and disunities.And that God also has implemented His own principles for people of different knowledges,colors,faiths and backgrounds to preserve respect amongst themselves.
Civilians were back to work few days after violence

The foundation urged muslims to live by principles of God while abiding with constitutional laws


Read more...

Friday, June 1, 2012

MAUAJI YA KUTISHA! VIFURUSHI VYENYE VIPANDE VYA MWILI VYAOKOTWA

0 comments
Kijana Lin Jun katiaka picha yake ya facebook,Jun alitoweka Mei 24 na kuripotiwa kupotea kwake Mei 29


Polisi nchini Kanada wanahangaika kumsaka mtu aliehusika na mauaji ya kinyama ya kijana raia wa China aliekuwa masomoni nchini humo.Kamanda wa Polisi wa jiji la Montreal Ian Lafreniere amesema wapelelezi wanaamini kuwa mauaji hayo yalifanyika siku ya Alhamisi au Ijumaa ya wiki iliyopita.


Lin Jun kijana kutoka China aliekuwa akisoma katika chuo kikuu cha Concordia alitoweka tangu Mei 24, na Mei 25 video ya kutisha inayoonyesha mauaji ya Lin iliwekwa kwenye internet.

Tarehe 26 Mei mtuhumiwa wa mauaji hayo Locco Luka Magnotto aliondoka jijini Montreal kwa  ndege kwenye uwanja wa Trudeau,lakini polisi wameshindwa kujthibitisha alielekea wapi,lakini polisim wanasema kuna uwezekano alirudi jijini humo na kujibadilisha


Tarehe 29 Mei ubalozi mdogo wa China  jijini Montreal uliweka tangazo  juu ya kutoweka kwa Lin kwenye mtandao wao na siku hiyo hiyo vifurushi vyenye vipande vya mwili wa Lin viliokotwa huko Ottawa na baadae sanduku lenye vipande vingine vya Lin lilikutwa nje ya  jengo la apartment mjini Montreal

Kwa mujibu wa taarifa za ubalozi huo Lin Jun ni mwenyeji wa jiji laWuhan nchni China, na alifika Kanada mwezi Julai mwaka jana kwa ajili ya kuchukua masomo ya uinjinia na sayansi ya kompyuta katika chuo kikuu cha Concordia.

Kwa mujibu wa watu waliomfahamu jijini Montreal, Lin mara nyingi alipenda kutumia majina ya Justin au Patrick kama ya ukoo muda wote aliokaa Kanada.


Msako wa kimataifa umeanzia nchini Ufaransa kumsaka mcheza picha za ngono Locco Luka Magnotto ambae inahisiwa kuwa ndie alieukatakata mwili wa mwanafunzi huyo na kisha kutuma vipande  vya mwili posta katika vifurushi


Nchini Ufaransa polisi wamesema wana uhakika Magnotto ametua nchini humo akitokea Montreal mwisho wa wiki iliyopita.Tayari kikosi maalum chenye wataalam wa kusaka wahalifu kimepewa amri ya kumsaka Magnotto.

Polisi jijini Montreal wanaamini Magnotto ndie aliemuua Lin,mtu ambae alikuwa na mahusiano nae,na kisha kuukatakata mwili wake na kuutia kwenye vifurushi kabla hajavituma vifurushi hivyo kwa njia ya posta hadi kwenye ofisi za vyama vikubwa viwili vya siasa nchini Kanada.


Polisi walitumia picha ya Lin kuwauliza watu wanaoishi kuzunguka jengo aliloishi Magnotto iwapo waliwahi kumuona Lin hapo.


Nao polisi wa kimataifa Interpol wameweka picha ya Magnotto kwenye mtandao wao juzi Alhamisi,ikiambatanishwa na picha za wahalifu wengine wa kimataifa wanaotafutwa kwa makosa ya mauaji,utekaji nyara na  kujihusisha na makundi ya uhalifu.

Interpol imekuja kushirikishwa katika sakata hili baada ya polisi wa Montreal kutoa kibali dunia nzima cha kukamatwa Magnotto.Ushahidi uliopatikana kutoka eneo la mauaji mjini Montreal umefanya polisi wapanue wigo wa msako kuwa wa kimataifa

Kamanda wa polisi wa Montreal, Ian Lafreniere.amesema "Kuna ushahidi tumeupata.Na pia tumepata barua ambayo iliwekwa kwenye mtandao wa kompyuta ambayo inatufanya moja kwa moja tuamini kuwa muhalifu amekimbilia nje ya nchi"



Kamanda Lafreniere pia amesema polisi wamekuwa wakishirikiana na maafisa wa uwanja wa ndege wa Montreal kupata taarifa zaidi, lakini amekataa kuweka wazi taarifa hizo."Hakuna nchi duniani ambayo hajatajwa" Lafreniere aliongeza,"Kwa hiyo ni lazima awe kwenye wakati mgumu"
Huyu ndie Locco Luka Magnotto mshukiwa wa mauaji ya Lin Jun
Read more...

DIAMOND NA NYUMBA YA MILIONI 69

0 comments

Hapa ni kwenye nyumba aliyopanga Sinza
.
Inawezekana ukawa una taarifa kwamba Diamond Platnums ni msanii mwenye mkwanja sana hapa Tanzania kutokana na show za bei gali na nyingi anazozifanya.
Inawezekana ukawa unataarifa kwamba Diamond Platnums ndio msanii ambae yuko juu kwa sasa Tanzania, na kwamba ndio msanii aliepiga show nyingi za bei ghali mwaka jana.
siyo hayo tu… kuna uwezekano ukawa una taarifa zake nyingi tu lakini hili ninalotaka kukwambia mimi ndio kwanza unalisoma kutoka hapa.
Kwenye show ya Big Brother Stargame Afrika Kusini akiimba wimbo wake `MAWAZO`
Akiongea na millardayo,Platnums amekubali kuzungumzia nyumba yake anayoijenga Tegeta Dar es salaam kutokana na pesa za muziki.
Amesema 
“ninapopata huwa najaribu kutengeneza vibanda vyangu vinisitiri manake ninazo nyumba tofauti tofauti, nyumba ya Tegeta nimetumia milioni 69 mpaka sasa, leo wanapiga plasta nyumba imekaribia kuisha kabisa, ni ya vyumba vinne; vitatu ni Master, kuna jiko kubwa tu, choo cha public, studio, dining room, sitting room… ni nyumba ya kisasa.Kiwanja nilikinunua mwezi wa tisa, 2011. Zipo nyingine ninazojenga, ila huwa sipendi kuzizungumzia”


Read more...

Thursday, May 31, 2012

OKWI ANA THAMANI YA SHILINGI BILIONI 2-SIMBA

0 comments
 Klabu ya Simba imewataka baadhi ya timu kuacha tabia ya kutaka
kutangaza kuwa wanamchukua mchezaji Emmanuel Okwi wakati wakijua ni mchezaji halali wa klabu hiyo.
 
Ofisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga, alisema kuwa kuna baadhi ya watu wameanza kutumia jina la Okwi kama njia ya kupata uongozi au kuonekana bora katika klabu zao huku zikiwa hazijawahi hata siku moja kufanya maongezi na klabu ya Simba.
 
Alisema kama kuna klabu inataka kumsajili mchezaji huyo ifuate utaratibu wa kuongea na viongozi wake kwa kuwa mchezaji huyo bado ni mali ya Simba.

Aliongeza kuwa kama kuna  klabu inataka imsajili Okwi inatakiwa kutumia zaidi ya bilioni 2 ili iweze kumchukua.
 

Alisema mchezaji huyo anatakiwa katika barani  Ulaya na iwapo kuna timu Tanzania inauwezo wa kutoa fedha hiyo, klabu ya Simba ipo tayari kumuuza kwa pesa hiyo.
"Tupo tayari kumuuza.Na kama kuna klabu hapa nchini ina bilioni 2, sisi tunamuachia, kwa kuwa bado mchezaji wetu na anaendelea kuitumikia klabu yetu ya Simba kwa zaidi ya miaka miwili"alisema Kamwaga.
Klabu ya Yanga kupitia wadau wake ilitangaza nia yake ya kumchukua mchezaji huyo raia wa Uganda kwa ajili ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.
Read more...

Wednesday, May 30, 2012

MTOTO ALIYEHARIBIWA MUHIMBILI BADO HOI INDIA

0 comments

 MTOTO Imrani Mwerangi (3) ambaye alipelekwa nchini India kwa matibabu baada ya kudungwa sindano iliyomsababishia mtindio wa ubongo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Dar es Salaam, bado amelazwa katika Kitengo cha Wagonjwa Mahututi (ICU) cha Hospitali ya Hyderabad, India.

Taarifa iliyotolewa jana na wazazi wa mtoto huyo kutoka nchini India, ilisema hali ya Imrani bado ni mbaya.

Machi mwaka huu Imrani alipelekwa nchini India na Serikali baada ya kulazwa katika ICU ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tangu Julai 28, 2011.

“ Tangu kipindi hicho madaktari wamekuwa wakipigania kuokoa maisha yake lakini bado amelazwa katika ICU ya Hospitali ya Hyderabad,India,” ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilisema madaktari wanaomhudumia wamesema mtoto huyo ataendelea kutegemea matibabu katika  maisha yake yote.

“ Asante Mungu kwa kuendelea kumpigania mtoto wetu Imrani, leo anatimiza miezi kumi tangu alazwe katika ICU za Muhimbili na hapa India,” ilisema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo ya wazazi ilisema maisha kwao yamekuwa yenye changamoto kubwa lakini jambo kubwa sasa ni kutanguliza maombi kwa Mungu.

Kwa mara ya kwanza mtoto huyo alifikishwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Julai 28, 2011 kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa nyama zilizokuwa puani ambapo alipokewa na kufunguliwa jalada IP.No.A586301.

Kesho yake Julai 29, 2011 mtoto huyo aliingizwa katika chumba cha upasuaji mdogo wa nyama za puani lakini kabla ya upasuaji huo alidungwa sindano ya usingizi ambayo ndiyo iliyomsababishia matatizo mtindio wa ubongo.
Read more...

Friday, May 25, 2012

SIR ALEX FERGUSON KUSTAAFU MWISHONI MWA MSIMU UJAO

0 comments
Kocha wa timu ya soka ya Manchester United, Sir Alex Ferguson  huenda akaachana na kazi yake ya ukocha mara tu baada ya kuisha kwa msimu wa 2012/2013,kutokana na kuanza kusumbuliwa na matatizo ya kiafya.


Kwa mujibu wa rafiki yake wa karibu ambae pia ni mmiliki wa timu ya Wigan Athletic,Dave Whelan,Ferguson anafikria kuachana na ukocha baada ya kupata matatizo ya kiafya Ijumaa iliyopita,amabapo alipatwa ghafla na ugonjwa wa kutoka damu puani mfululizo bila kuacha na kusababisha akimbizwe Hospitali ya Glasgow


Whelan alikuwa alikiambia kituo cha televisheni cha  ESPN:
"Baada ya msimu ujao,Sir Alex atabwaga manyanga.Msukumo wa mambo unataka iwe hivyo,hasa unapokuwa uko juu kwa muda mrefu.Umri unapokuwa umeshakwenda inakuwa ngumu kupambana namsukumo wa majukumu,na ipo siku lazima itakuathiri.Sir Alex ni mgumu kukubali kushindwa na najua atataka aendelee na hadi siku atakayodondoka na pia naheshimu mafanikio aliyofikia kama wengine wanavyoheshimu.Najua lengo lake lilikuwa kuendelea kwa miaka miwili au mitatu zaidi,pengine zaidi ya hapo,lakini alipata matatizo kidogo ya kiafya wiki iliyopita,hiyo inaniambia kuwa lazima afikirie kwa kina maamuzi yake na atagundua kuwa hakuna ulazima wa kuendelea kwa miaka mingine mitano na kujiweka katika hatari.Ningependa niseme yeye ni kocha bora kabisa kupata kutokea.Kama ataamua kweli kufunga virago, basi litakuwa ni pigo kubwa katika mchezo wa soka.Nina hakika.Jinsi mafanikio yake yasivyo lingana na ya mtu (kocha) yeyote,jinsi anavyochagua wachezaji kwa usahihi na kupata mavuno zaidi kutoka kwao,inamfanya awe kocha bora kabisa,bora zaidi ya tuliowahi kuwaona"
Read more...
 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797