Hayati George Saitoti |
Hayati Joshua Ojode |
Waziri wa Usalama wa ndani wa Kenya
Profesa George Saitoti na Naibu wake Orwa Ojode wamefariki dunia katika
ajali ya helikopta ya polisi iliyotokea leo asubuhi katika eneo la
Kibiku, karibu na mji wa Ngong takriban kilometa ishirini kutoka mji
mkuu wa Nairobi.
Abiria wote sita, wakiwemo marubani wawili na
walinzi wa mawaziri hao waliokuwa kwenye helikopta hiyo wamefariki
dunia na miili yao kuteketezwa kwa kiasi cha kutoweza kutambulika.Kilichosababisha ajali hiyo bado hakijajulikana
Kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Habari la Uingerza BBC waziri Saitoti na maafisa wengine wa juu katika wizara ya usalama wa ndani walikuwa wakielekea katika eneo la Sotik kwa mkutano unaohusu mambo ya usalama.
Saitoti alikuwa miongoni mwa wanasiasa mashuhuri nchini Kenya waliokuwa wakipania kugombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao.
Walioshuhudia ajali hiyo wamesema waliona helikopta hiyo ikizunguka angani kabla ya kuanguka katika msitu wa Ngong.
Polisi wamezingira eneo la ajali hiyo na kamishna wa polisi Mathew Iteere aliyepo katika eneo la ajali anatarajiwa kutoa taarifa kamili kuhusiana na ajali hiyo.
Ajali hiyo ya helikopta imetokea katika siku ambapo Kenya inaadhimisha miaka minne tangu kutokea ajali ya ndege iliyowauwa mawaziri wengine wa serikali, Kipkalya Kones na Lorna Laboso
SOURCE: BBC.http://www.bbc.co.uk/swahili/habari
0 comments:
Post a Comment