“ Ndugu Wananchi;
Napenda
kutumia nafasi hii kutoa pongezi na shukrani nyingi kwa ndugu zetu wa
Arusha kwa kuwapokea vizuri na kuwakarimu vyema wageni wetu hao.
Nawaomba waendelee na moyo huo mpaka watakapoondoka wote. Naomba kuwepo
kwa mkutano huu kuwakumbushe umuhimu wa mji wenu kuwa tulivu. Miaka
miwili iliyopita isingekuwa rahisi kwa watu au shirika kubwa la
kimataifa kama Benki hii kuamua kufanya mkutano wake Arusha. Isitoshe
hata sisi wenyewe tusingeshawishika kuomba au kukubali maombi ya namna
hiyo. Lakini sasa imewezekana. Naomba kila mmoja wetu aweke azimio
moyoni mwake la kuhakikisha kuwa hali ile haijirudii tena. Nyota ya
Geneva ya Afrika lazima iendelee kuangaza. Yaliyopita si ndwele tugange
yajayo . ( J.K . KIKWETE.)
“Narudia tena , IKULU iliingilia kesi yangu ya Ubunge”.
Mh
Rais nimekusikiliza kwa makini sana ila nakupa pole kwani bado unafikiri
unaongea na Tanzania ya mwaka 1961 , umesema sasa Arusha ni shwari
tofauti na miaka miwili iliyopita kwani sasa kuna amani na utulivu wa
kutosha ndio maana hata mkutano wa AFDB umefanyika Arusha .
Mh
Rais , najua IKULU iliingilia kesi yangu kama ilivyoonekana na ndio
sababu hata Mkuu wa Mkoa wa Arusha wakati anaapisha Wakuu wa Wilaya
alimpongeza Jaji kwa hukumu nzuri aliyowafurahisha wakati kesi hiyo iko
mahakama ya Rufaa , lakini jambo moja la msingi ambalo huwezi kulitambua
kwa sasa ni kuwa Haki na Ukweli haviwezi kushindwa na dhuluma, ubaya
wala mamlaka , natambua wewe ni Rais na unayo mamalaka makubwa katika
Taifa hili lakini vile vile nataka utambue kuwa huna mamlaka makubwa
dhidi ya haki , utu na ukweli.
Mh
Rais hakuna Amani Duniani inayozidi Haki na usawa ,utu na ukweli , haipo
na wala haitakuwepo , ndio maana kila siku nasema ni “Afadhali Vita
Inayotafuta Haki na usawa kuliko Amani inayopumbaza na kudhalilisha utu
wa Mwanadamu “ umefurahia sana mkutano uliokupa fursa ya kutoa maneno ya
kebehi na kudhihirisha ila chafu iliyofanywa na Serikali yako na
kujaribu kuhadaa Umma kama ilivyo kawaida ya Serikali yako na Chama
chako , hata hivyo wakati huu kuna mambo ya msingi yakushughulikia zaidi
ya kebehi na hadaa , Uchumi wa Nchi umeyumba, huduma za msingi za jamii
zimepuuzwa, Mpasuko katika suala la Muungano na vururugu zinazoendelea
Zanzibar , mfumuko wa bei hizi ni sababu chache ambazo haziwezi kuruhusu
wakati huu kuwa wakati wa kebehi na mizaha isipokuwa kazi .
Mh
Rais , Mama Theresa , Nelson Mandela , Martin Luther Jr na Malcom X
hawakuwa Wabunge kupigania haki za Nchi yao na watu wao , sihitaji
Ubunge kupigania ukweli, haki na utu , nahitaji dhamira safi , nia njema
na huu utakuwa wajibu wangu mpaka nakwenda kaburini , nitakapomaliza
mbio hizi najua nitapata fursa ya kutazama nyuma yangu nione nini
nilifanya , ukweli nisingependa kuona vituo vya mafuta , magorofa ,
magari na viwanja vingi kila kona ya Nchi bali Haki ,Usawa na utu vikiwa
kama nguzo ya imani ya watawala wetu watakaokuwepo, pengine sitaishi
miaka mingi sana kama utachukizwa sana na waraka wangu huu kwani Polisi ,
Usalama wa Taifa na Jeshi la Wananchi wanakutii wewe , hata hivyo
siogopi kufa kwani nisipokufa kesho , nitakufa siku moja ambayo siijui ,
napenda kuishi maisha marefu nimwone mke wa mtoto wangu kama
itawezekana , lakini kuliko iwezekane kwa kuishi kwa hofu ni bora
ishindakane kwa kuthamini haki , kwa hiyo kama utakuwa umekasirika sana ,
unaweza kufanya jambo lolote baya kwa kutumia mamlaka yako , niko
tiyari sio kesho wala leo isipokuwa sasa hivi, najua IKULU imewazulumu
watu wa Arusha Mbunge wao.
Mh
Rais ninajua wazi njama zote na hasira hizi zinaweza kuwa zimetokana
hasa na mkutano tuliokaa Osterbay Dar mimi na wewe kabla ya uchaguzi
mkuu wa mwaka 2010 hata hivyo sikupuuza maongezi yetu isipokuwa
nilichagua kufuata dhamira yangu na wito wangu wa utumishi wa kweli
katika Jimbo langu na Nchi yangu.
Mh
Rais nimekuelewa na Wananchi wamekuelewa kila mahali , wewe ni Rais
unayo mamlaka makubwa na mimi ni mwananchi mamlaka yangu makubwa ni kwa
mke wangu tu , sina Polisi wala Usalama wa Taifa lakini nitawaomba
wanyonge wafunge na kusali tuone kama mamlaka yako inaweza kushindana na
haki na ukweli .
Mh
Rais “Mtu anaweza kuzini kwa siri lakini hawezi kuugua ukimwi kwa siri”
Serikali na Chama cha Mapinduzi kimepuuza watu na haki zao kwa muda
mrefu , lakini wakati umefika ambapo hawatapuuzwa tena hata hivyo kwa
kauli yako hii naamnini haiwezi kuwafundisha kazi majaji wa mahakama ya
rufaa .
“ ONLY TIME WILL TELL”.
GODBLESS .J. LEMA.
0 comments:
Post a Comment