MSANII maarufu
wa filamu Tanzania ambae alikuwa ameenda India kwa ajili ya matibabu, Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’ameanza kupata nafuu na anaendelea na dozi ili aweze kupona kabisa.
Akiongea na waandishi wa magazeti ya kampuni ya Global Publishers siku ya Jumatatu nyumbani kwake Tabata jijini Dar Es Salaam,
msanii huyo alisema sasa hivi afya yake imeimarika kidogo tofauti na ilivyokuwa
awali na anawashukuru watu wote waliojitolea kwa namna yoyote ile kwa lengo la kumsaidia na kwamba yeye hana cha
kuwalipa ila Mungu atawalipa
.
“Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu kwani hali yangu inaendelea vizuri, kinachonisumbua ni ukali wa hizi dawa tu kwani kuna wakati mwingine nakosa nguvu lakini madaktari waliniambia nizitumie mpaka zitakapoisha,” alisema Sajuki na kuongeza:
“Pia niwashukuru Watanzania kwa michango yao, hakika wameonesha ubinadamu wa hali ya juu kwangu lakini pia ningependa nikanushe taarifa za kwamba nimerejea kama nilivyokwenda. Kwa aliyeniona wakati naondoka atakubaliana na mimi kuwa afya yangu imetengemaa kwa kiasi fulani.”

Mbali na shukrani kwa Watanzania, Sajuki amewashukuru pia madaktari wa
hospitali ya Saifee,mjini Mumbai,India kwa uangalizi waliompatia ikiwemo kumpa chakula
kizuri kilichokuwa kikihitajika kutokana na dawa anazotumia
.
“Nawashukuru sana wale madaktari kwani wamenitibu chini ya uangalizi mzuri kiasi cha kunifanya nipate nafuu hii,” alisema
“Nawashukuru sana wale madaktari kwani wamenitibu chini ya uangalizi mzuri kiasi cha kunifanya nipate nafuu hii,” alisema
.
Sajuki alianza kusumbuliwa na uvimbe mwaka jana ulioanzia mkononi kisha ndani ya mwili kwenye ini na baadae ikagundulika kuwa, siyo kwenye ini tu bali umesambaa hadi sehemu nyingine za tumboni.
..
Sajuki alianza kusumbuliwa na uvimbe mwaka jana ulioanzia mkononi kisha ndani ya mwili kwenye ini na baadae ikagundulika kuwa, siyo kwenye ini tu bali umesambaa hadi sehemu nyingine za tumboni.
..
WAKATI
afya ya Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’ ikiendelea
vizuri baada ya kupata matibabu habari kutoka huko huko nchini India zinasema kuna utata juu ya
maendeleo ya afya ya mchekeshaji maarufu nchini, Joseph Shamba ‘Vengu’
ambaye naye yuko nchini humo kwa matibabu,
Habari zinadai kuwa
hali ya msanii huyo wa kundi la wachekeshaji la Orijino Komedi imekuwa ya giza mbele
ambapo ndugu zake waishio Dar hawajui nini kinaendelea.
Katikati ya
mwezi Mei, ilidaiwa Vengu angerejea nchini wakati wowote baada ya afya
yake kutengemaa, lakini ndugu mmoja wa karibu amesema
ilishindikana kuruhusiwa baada ya hali ya msanii huyo kubadilika ghafla.
“Ilikuwa arudi nyumbani kweli, maana kidogo alikuwa anaridhisha, lakini ghafla hali ikabadilika tena, kwa hiyo hatarudi kwa sasa,” alisema ndugu huyo
.
Vengu aliwahi kulazwa kwa muda mrefu Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akikabiliwa na ugonjwa uitwayo Cerebral Atrophy. Ugonjwa huu husababisha seli za kichwani kukosa mawasiliano na sehemu nyingine na mgonjwa hupoteza fahamu mara kwa mara.
Akiwa hospitali ya Muhimbili, hali ilizidi kuwa mbaya hivyo mchekeshaji huyo alikimbizwa katika Hospitali ya Apolo iliyopo nchini India kwa matibabu zaidi.

Sajuki
alikwenda Mumbai, India katikati ya Mei mwaka huu kutibiwa matatizo ya
uvimbe tumboni kwenye Hospitali ya Saifee. Alirejea nchini Juni 6, mwaka huu, akiwa anaendelea
vizuri.
0 comments:
Post a Comment