Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo,CHADEMA,Bw.Benson Kigaila leo mchana ametoa tamko la chama hicho juu ya utekwaji nyara wa Kiongozi wa Jumuia ya Madaktari Tanzania,Dk.Ulimboka Steven,ambae usiku wa kuamkia jana alitekwa nyara na watu wasiojulikana,kujeruhiwa na kutelekezwa katika maeneo ya Pandemabwe nje kidogo ya jiji la Dar Es Salaam.
Mbele ya waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya chama hicho Mtaa wa Ufipa,Kinondoni ,jijini Dar Es Salaam,Bw.Kigaila amesema:
"Suala
hili la kutekwa Dk ulimboka linatukumbusha miaka ya sabini wakati
wagombea haki walivyokuwa wakipotea katika hali za kutatanisha. Matukio
mengi ya kuuwawa wagombea haki nchini yanatuonyesha ni namna gani
serikali yetu ni dhaifu na bunge lina meno ya plastic.
Chadema tunadhani na ni ukweli ulio wazi kuwa tukio hili lina mkono wa
serikali, IGP Mwema mtaalamu wa kuoteshwa kutokea vurugu katika
maandamano ya chadema iwapi inteligensia yake katika hili?
Serikali haina nia thabiti ya kumaliza tatizo la madaktari maana imeamua
kuongeza mishahara kwa baadhi ya watendaji wa serikali mpaka kufikia
milioni kumi kwa mwezi, mfano ikulu inakarabatiwa kila mwaka kwa kutumia
bilioni 6, hii ni hatari. Halafu wanatuambia serikali haina fedha za
kumaliza tatizo la madaktari.. "
PICHA NA HABARI KWA HISANI YA HAFIDH KIDO (JEMBE)
Chadema tunadhani na ni ukweli ulio wazi kuwa tukio hili lina mkono wa serikali, IGP Mwema mtaalamu wa kuoteshwa kutokea vurugu katika maandamano ya chadema iwapi inteligensia yake katika hili?
Serikali haina nia thabiti ya kumaliza tatizo la madaktari maana imeamua kuongeza mishahara kwa baadhi ya watendaji wa serikali mpaka kufikia milioni kumi kwa mwezi, mfano ikulu inakarabatiwa kila mwaka kwa kutumia bilioni 6, hii ni hatari. Halafu wanatuambia serikali haina fedha za kumaliza tatizo la madaktari.. "
0 comments:
Post a Comment