|
Mheshimiwa John Mnyika |
Mbunge wa Jimbo la Ubungo
(Chadema), Mhe. John Mnyika ametolewa nje ya bunge mchana huu na Naibu
Spika, Job Ndugai baada ya kukataa kufuta kauli yake kuwa Rais Kikwete
ni dhaifu wakati alipotakiwa kufanya hivyo. Mnyika ametolewa nje ya
bunge wakati wabunge wakichangia mjadala wa bajeti ya serikali mwaka wa
fedha 2012/13 iliyowasilishwa bungeni hivi karibuni. Mnyika atarudi
bungeni kesho saa tatu asubuhi.
Muda mfupi baadae Twitter ikalipuka na baadhi ya meseji ni hizi:
Baadae Mbunge Mnyikaaliandika kwenye akaunti yake ya Facebook kuonesha msimamo wake kuhusu kauli aliyoitoa:
Msimamo wangu wa sasa juu ya Kauli yangu!
Nitatoa tamko la kina baadae kuhusu kilichotokea lakini kwa ufupi ubovu
wa bajeti hii ni matokeo ya udhaifu wa Rais Kikwete, yeye ndiye
aliyesaini Mpango wa Taifa wa miaka mitano kama Kiongozi Mkuu wa Nchi
tena kwa wino mwekundu kama Amiri Jeshi Mkuu. Na yeye ndiye Mwenyekiti
wa baraza la mawaziri, bajeti hii iliyoacha kuzingatia mpango wa Taifa
imepita k wenye baraza alilloliongoza, pia kushindwa kutekelezwa kwa bajeti iliyopita ni matokeo pia ya udhaifu wa taasisi ya Urais.
Pia kwa mujibu wa Katiba Rais ndiye ambaye anapeleka bajeti bungeni,
Waziri mwenye dhamana anapeleka tu kwa niaba. Rais amepewa mamlaka
makubwa juu ya bajeti ibara ya 99 imeweka mipaka kuhusu mambo ambayo
bunge lina mamlaka nayo huku ibara ya 90 inasema bunge likikataa bajeti
rais ana mamlaka ya kuvunja bunge. Hivyo Rais Kikwete anapaswa kuagiza
Waziri wa Fedha bajeti iondolewe irudi kwenye baraza la mawaziri
ikafanyiwe marekebisho.
0 comments:
Post a Comment