Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudi Arabia |
Mtu mmoja amekatwa kichwa leo kwa kosa la kushiriki mambo ya uchawi nchini Saudi Arabia,mtandao wa Arab News limeandika likinukuu taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo.
Taarifa zingine za vyombo vya habari nchini humo zinasema kuwa,mtu huyo,Muree bin Ali Al-Asiri,pia amekiri kufanya zinaa na wanawake wawili.Amehukumiwa kwa kukatwa kichwa chake katika jimbo la Najran lililoko kusini mwa nchi hiyo.
Katika ripoti ya Shirika la Habari la Uingereza BBC linasema kuwa mwezi Disemba mwaka uliopita mwanamke mmoja alihukumiwa adhabu kama hiyo baada ya kukutwa na kosa la uchawi,na mwezi Septemba raia mmoja wa Sudan alihukumiwa kukatwa kichwa licha ya kupigiwa kelele na Taasisi ya Kimataifa ya Haki za Binadamu,Amnesty International,kutaka waachiwe.
Mhariri wa BBC mambo ya Uarabuni,Sebastian Usher amesema kuwa viongozi wa kidini wenye nguvu kubwa na msimamo mkali nchini humo wanaunga mkono adhabu hizo kutolewa kwa mtu yeyote anaekutwa na kosa la kufanya uganga ikiwamo kupiga ramli na kutibu kwa njia za kiimani
Kwa mujibu wa mtandao wa Arab News watu wengine wawili mtu na dada yake, rai wa Misri,walihukumiwa na mahakama moja mjini Madinah baada ya kupatikana na hatia ya kuteka nyara na kubaka
Mohammed bin Nafe na dada yake Jamalat bint Nafe walikutwa na kosa la kumteka nyara binti wa miaka 9 kutoka Msikiti wa Mtume Madinah, kumtesa na kumweka kifungoni ndani ya nyumba wanayoishi kwa miaka mitatu na miezi sita.Inasemekana Mohammed alikuwa akimbaka binti huyo kwa muda wote huon na walikuwa na mpango wa kumtorosha nje ya nchi
Kosa lingine walilokutwa nalo ni kuwatelekeza na kuwatesa watoto wao kuwapiga na kutojali afya zao,jambo ambalo lilipelekea watoto wawili wa Mohammed kupoteza maisha.
Hukumu nyingine ya kuchinjwa iliyotolewa leo nchini humo ni ya mtu mwingine aitwae Ali bin Mohammed Al-Qahtani ambae alipatikana na hatia ya kumpiga risasi Msaudia mwenzie na kumuua.
0 comments:
Post a Comment