Pages

 

Friday, June 1, 2012

MAUAJI YA KUTISHA! VIFURUSHI VYENYE VIPANDE VYA MWILI VYAOKOTWA

0 comments
Kijana Lin Jun katiaka picha yake ya facebook,Jun alitoweka Mei 24 na kuripotiwa kupotea kwake Mei 29


Polisi nchini Kanada wanahangaika kumsaka mtu aliehusika na mauaji ya kinyama ya kijana raia wa China aliekuwa masomoni nchini humo.Kamanda wa Polisi wa jiji la Montreal Ian Lafreniere amesema wapelelezi wanaamini kuwa mauaji hayo yalifanyika siku ya Alhamisi au Ijumaa ya wiki iliyopita.


Lin Jun kijana kutoka China aliekuwa akisoma katika chuo kikuu cha Concordia alitoweka tangu Mei 24, na Mei 25 video ya kutisha inayoonyesha mauaji ya Lin iliwekwa kwenye internet.

Tarehe 26 Mei mtuhumiwa wa mauaji hayo Locco Luka Magnotto aliondoka jijini Montreal kwa  ndege kwenye uwanja wa Trudeau,lakini polisi wameshindwa kujthibitisha alielekea wapi,lakini polisim wanasema kuna uwezekano alirudi jijini humo na kujibadilisha


Tarehe 29 Mei ubalozi mdogo wa China  jijini Montreal uliweka tangazo  juu ya kutoweka kwa Lin kwenye mtandao wao na siku hiyo hiyo vifurushi vyenye vipande vya mwili wa Lin viliokotwa huko Ottawa na baadae sanduku lenye vipande vingine vya Lin lilikutwa nje ya  jengo la apartment mjini Montreal

Kwa mujibu wa taarifa za ubalozi huo Lin Jun ni mwenyeji wa jiji laWuhan nchni China, na alifika Kanada mwezi Julai mwaka jana kwa ajili ya kuchukua masomo ya uinjinia na sayansi ya kompyuta katika chuo kikuu cha Concordia.

Kwa mujibu wa watu waliomfahamu jijini Montreal, Lin mara nyingi alipenda kutumia majina ya Justin au Patrick kama ya ukoo muda wote aliokaa Kanada.


Msako wa kimataifa umeanzia nchini Ufaransa kumsaka mcheza picha za ngono Locco Luka Magnotto ambae inahisiwa kuwa ndie alieukatakata mwili wa mwanafunzi huyo na kisha kutuma vipande  vya mwili posta katika vifurushi


Nchini Ufaransa polisi wamesema wana uhakika Magnotto ametua nchini humo akitokea Montreal mwisho wa wiki iliyopita.Tayari kikosi maalum chenye wataalam wa kusaka wahalifu kimepewa amri ya kumsaka Magnotto.

Polisi jijini Montreal wanaamini Magnotto ndie aliemuua Lin,mtu ambae alikuwa na mahusiano nae,na kisha kuukatakata mwili wake na kuutia kwenye vifurushi kabla hajavituma vifurushi hivyo kwa njia ya posta hadi kwenye ofisi za vyama vikubwa viwili vya siasa nchini Kanada.


Polisi walitumia picha ya Lin kuwauliza watu wanaoishi kuzunguka jengo aliloishi Magnotto iwapo waliwahi kumuona Lin hapo.


Nao polisi wa kimataifa Interpol wameweka picha ya Magnotto kwenye mtandao wao juzi Alhamisi,ikiambatanishwa na picha za wahalifu wengine wa kimataifa wanaotafutwa kwa makosa ya mauaji,utekaji nyara na  kujihusisha na makundi ya uhalifu.

Interpol imekuja kushirikishwa katika sakata hili baada ya polisi wa Montreal kutoa kibali dunia nzima cha kukamatwa Magnotto.Ushahidi uliopatikana kutoka eneo la mauaji mjini Montreal umefanya polisi wapanue wigo wa msako kuwa wa kimataifa

Kamanda wa polisi wa Montreal, Ian Lafreniere.amesema "Kuna ushahidi tumeupata.Na pia tumepata barua ambayo iliwekwa kwenye mtandao wa kompyuta ambayo inatufanya moja kwa moja tuamini kuwa muhalifu amekimbilia nje ya nchi"



Kamanda Lafreniere pia amesema polisi wamekuwa wakishirikiana na maafisa wa uwanja wa ndege wa Montreal kupata taarifa zaidi, lakini amekataa kuweka wazi taarifa hizo."Hakuna nchi duniani ambayo hajatajwa" Lafreniere aliongeza,"Kwa hiyo ni lazima awe kwenye wakati mgumu"
Huyu ndie Locco Luka Magnotto mshukiwa wa mauaji ya Lin Jun

0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797