Pages

 

Friday, June 15, 2012

SABABU ZA ULINZI MKALI KWA LULU ZATAJWA

0 comments

Lulu akiingia Mahakama Kuu siku ya Jumatatu
Siri ya kumwekea ulinzi mkali Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye anakabiliwa na mashitaka ya kifo cha Steven Kanumba imebainika.

 Siri hiyo,kwa mujibu wa gazeti la IJUMAA, ilitolewa Jumatatu iliyopita na askari polisi mmoja ambaye hakuwa tayari kutajwa. Askari huyo siku hiyo ndie alikuwa na kazi ya kukagua watu wanaoingia kwenye Jengo la Mahakama ya Kuu kwa ajili kusikiliza kesi ya msanii huyo iliyokuwa ikitoa maamuzi ya kujadili umri wa Lulu.

Tangu kesi yake ilipoanza kutajwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,msafara wa Lulu kwenda na kutoka mahaklamani umekuwa na ulinzi mkali wa askari wenye silaha nzito na Jumatatu wakati anafikushwa Mahakama Kuu hali ilikuwa hivyo hivyo,na pia kila aliyeingia Mahakamani alikuwa akipekuliwa vilivyo na askari wenye uzoefu wa kazi hiyo.Waandishi wa habari na wapigapicha walipekuliwa hata baada ya kuwa wameonesha vitambulisho vya kazi zao

Askari huyo alitoa mlolongo wa maelezo baada ya mwandishi mmoja kutaka kujua ni kwanini ulinzi umekuwa mkali kiasi hicho wakati anaelindwa ni msichana mdogo ambae haonekani kuwa anaweza kuwazidi nguvu na kutoroka.




Alisema kesi ya Lulu ni tofauti kidogo na zingine, na kwamba ulinzi huo si kwamaba Lulu anaweza kututoroka, isipokuwa kuna taarifa kuwa kuna kundi la watu linataka kumdhuru na hata kumuua

Alipouliza iwapo kuna taarifa ambazo zinafafanua kundi hilo ni la watu gani alisema taarifa hizo ni za kipolisi na si sahihi kuziweka hadharani.

“Hiyo ni siri ya ndani, lakini sisi tunasema ole wake mtu yeyote atakayenaswa akiwa katika mpango wa kutaka kutekeleza mpango huo au atakayethubutu, yaani naapa atakiona kilichomtoa kanga manyoya.”

 Lulu amekuwa kwenye ulinzi mkali mahakamani hata anapokwenda msalani. Na kuhusu hilo askari huyo alifafanua kuwa wamepewa amri ya kuimarisha ulinzi na kwa maana hiyo popote mshitakiwa anapokwenda ulinzi haulegezwi.Na hali hiyo ipo hata Segerea anapohifadhiwa mshitakiwa kwa sasa.

,",,,,,lengo ni kuimarisha ulinzi, hatuwezi kulegeza ulinzi mahali popote na hivi ninavyokwambia hata ulinzi wa Gereza la Segerea umeongezwa kwa ajili yake, kuna askari wametolewa magereza mbalimbali wameongezwa"

Inasemekana ulinzi wa Lulu mahakamani,pamoja na askari wa kawaida, pia kuna askari zaidi ya 20 waliovalia kofia za chuma na nguo maalum za kuzuia risasi bunduki aina ya SMG  20 zenye risasi 60 ndani , kila moja pembeni ikiwa na mkanda wa risasi 60 za ziada.

Alipoulizwa iwapo hilo kundi alilolitaja lina nguvu inayostaili kudhibitiwa kwa ulinzi uliopo,alisema kuwa kwa kawaida unapojiandaa kupambana na adui lengo ni kumshinda,kwa hiyo ni vyema kujkamilisha kwa kila kitu,na si vyema kukadiria nguvu ya adui yako

 
"...... ni lazima ujikamilishe, huwezi kujua mwenzio amejiandaa vipi, cha msingi sisi tumejiandaa vya kutosha, si unaona huu msafara wa magari matatu na askari zaidi ya 30, tena wenye silaha unazoziona na nyingine huzioni tumetoka Segerea kuja hapa kwa ajili ya mtu mmoja.Ni gharama kubwa kwa serikali maana kuna askari walitakiwa kwenda likizo lakini wamelipwa kwa ajili ya kusitishiwa likizo zao kwa sababu ya huyu Lulu,” alisema askari huyo.

Taarifa zilizopo zinadai kuwa hali ya wasiwasi wa usalama wa Lulu ilianza tangu yuko kituoni Oysterbay.Vyombo kadhaa vya habari viliripoti kuwa kundi la watu waliotoka kwenye mazishi ya Steven Kanumba lilielekea kituoni hapo katika staili ya mchakamchaka na nyimbo, wakidai wakabidhiwe Lulu.  


UNAWEZA KUCHUNGULIA NA HIZI:








0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797