Pages

 

Tuesday, May 1, 2012

MATOKEO YA KIDATO CHA SITA HAYA HAPA

0 comments


0 comments:



Read more...

MWEZI KUSOGEA KARIBU NA DUNIA JUMAMOSI HII

0 comments


Taswira kubwa kabisa ya uso wa mwezi kwa 2012 itaonekana Jumamosi hii.Kwa mujibu wa wataalam wa mambo ya anga za mbali mwezi utaonekana kuwa karibu zaidi usiku wa tarehe 5 mwezi huu na  kwa sababu
Read more...

BINGWA WA DUNIA WA KUOGELEA AKUTWA AMEKUFA BAFUNI

0 comments
Bingwa wa dunia wa mchezo wa kuogelea Mnorway Alexander Dale Oen amefariki dunia akiwa katika kambi ya mazoezi mjini  Flagstaff,Arizona nchini Marekani

Rais wa Shirikisho la Michezo ya Kuogelea la Norway Per Rune Eknes ametangaza  kuwa bingwa wa dunia  wa michezo hiyo kwa umbali wa mita 100,Mnorway Alexander Dale Oen amefariki dunia jana  kwa ugonjwa wa moyo akiwa na umri wa miaka 26.

Muogeleaji huyo alikutwa ameanguka bafuni jana na alikimbzwa katika Hospitali ya Flagstaff ambako ilithibitishwa kuwa tayari alikuwa ameshakufa .Starla Collins msemaji wa hospitali hiyo alitangaza rasmi kifo cha muogeleaji huyo,lakini hakutoa maelezo zaidi

Oen alishinda katika mashindano ya mjini Shanghai  mwaka jana,siku tatu tu baada ya Andres Breivik kufanya mauaji ya kinyama ya watu 77 nchini Norway na aliutunukia ushndi huo kwa wahanga wa mauaji hayo huku akiinyooshea kidole bendera ya Norway iliyobandikwa kwenye kofia aliyovaa.

Timu ya Norway itakayoshiriki michezo ya olimpiki imeweka kambi mjini Flagstaff.Wachezaji wengine walisema kuwa kabla ya tukio Dale Oen alifanya mazoezi mepesi tu na  kucheza gofu,lakini baadae walipata wasiwasi walipogundua kuwa mwenzao ameshatumia muda mrefu bafuni na walipokwenda kugonga alikuwa hajibu.Walipoingia walimkuta amelala mwili nusu ya mwili ukiwa sakafuni na nusu nyingine kwenye jakuzi.Daktari wa timu alianzakumpatia huduma ya kwanza mara moja kabla gari la wagonjwa halijafika.Oen alikuwa ni moja ya tegemeo la Norway katika michezo ijayo ya olimpiki
Read more...
 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797