Pages

 

Sunday, July 21, 2013

WAENDA JELA KWA KUPOST NYAMA YA NGURUWE NA KEJELI KWENYE FACEBOOK WAKATI WA MFUNGO

0 comments
Alvin Tan na Vivian Lee wakiwa chini ya ulinzi
Wamiliki wa Blog moja inayojihusisha na masuala ya ngono Alvin Tan na Vivian Lee wamefunguliwa mashtaka na kuwekwa ndani bila ya dhamana nchini Malaysia baada ya kuweka picha inayowakosea waumini wa kiislam kwenye Facebook.Wanakabiliwa na adhabu ya kifungo cha miaka minane jela.

Alvin na Vivian kwenye picha iliyowaponza ambayo ina ujumbe unaotafsirika kama"Futari njema furahi na nyama ya nguruwe,harufu nzuri, tamu, inayotia hamu ya kula"
Picha iliyowaponza  ilikuwa ikiwaonesha wakila nyama ya nguruwe ikiwa na ujumbe wa kuwatakia waislam ramadhan njema.Mamlaka inayosimamia sheria nchini humo imelichukulia tuko hilo kuwa ni kosa kubwa,ikizingatiwa kuwa nyama ya nguruwe ni haram (hairuhusiwi) kwa waumini wa kiislam.Ingawa watu hao walijitetea kuwa walilenga katika kuonesha ucheshi wao,imechukuliwa kuwa inawavunjia heshima baadhi ya watu katika jamii na pia kuzingatia na kazi wanayojihusisha nayo wakosaji pia si nzuri ambapo wamekuwa wakiweka video za ngono kwenye ukurasa wao wa Youtube uitwao `Sexcussions with Alvin` na pia wanamiliki blog inayoegemea kwenye masuala ya ngono.

Picha za ngono ni marufuku kwenye nchi za Malaysia na Singapore,hivyo tukio hilo limesababisha Tan mwanafunzi wa sheria Chuo Kikuu cha Malaysia kunyang`nywa hati za masomo ya juu (Scholarship) ya nchi za ASEAN,baada ya malalamiko ya wananchi dhidi ya blog yao.

Tan na Lee wameshakana mashtaka yao na wamewekwa ndani bila dhamana hadi kesi yao itakapoanza kusikilizwa Agosti 23 mwaka huu.Baada ya tukio hilo waliomba radhi kwenye ukurasa wao wa Youtube kwa kusema:
 "Tunarekodi video hii ili kuwaomba radhi waumini wa kiislam kwa kuwa tumewakosea kwenye mwezi huu mtukufu wa Ramadhan"


Read more...

Wednesday, July 17, 2013

BREAKING NEWS:LUKUMAY WA KLABU MASAI AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI

0 comments
LUKUMAY  (kulia)enzi za uhai wake
Habari nilizozipata muda mchache uliopita ambazo zimethibitishwa na ndugu na jamaa wa karibu zinasema Benedict Charles Lukumay amefariki kwa ajali ya gari eneo la Mikumi mkoani Morogoro usiku huu.
 
Chanzo cha kifo chake kimeelezwa kuwa ni ajali ya gari iliyotokea eneo la Mikumi mkoani Morogoro majira ya saa mbili usiku. Meneja mkuu wa Meridian Hotel LTD Mzee Mponda amethibitisha juu ya kifo hicho, huku huku akisema kuwa ilitokana na ajali ya gari.

 "Wakiwa na mwenzake aliyefahamika kwa jina la Adrian na gari binafsi wakielekea mkoani Iringa gari aliyokuwamo marehemu iligonga nyuma ya roli lililokuwa limesimama njiani." alisema Mzee Mponda.

 Adrian ambaye ndiye aliyekuwa anaendesha gari alinusurika kwenye ajali hiyo.

 Benedict alikuwa ni mmoja kati ya Wakurugenzi watendaji wa kampuni ya Meridian Hotel LTD inayomiliki na kuendesha kumbi za burudani zikiwemo Masai Kinondoni, Masai Ilala na Masai Galapo Ilala.
Kifo chake kimeacha pengo kubwa si tu kwa familia bali hata wapenda burudani, akifahamika kimchango katika kusimamia na kuendeleza burudani na yakiwemo maonyesho mbalimbali ya wanamuziki wa bongo fleva na fani nyinginezo.

Mungu alaze Pema ROHO ya Marehemu Ben..
Read more...

PHOTOS:LADY JAY DEE`S MAKE-UP SESSION DURING THE VIDEO SHOOTING OF HER SINGLE HIT `YAHAYA`

0 comments

Read more...

MKONGWE GEORGE MASATU ALILIA KURUDI SIMBA

0 comments
Waliosimama kutoka kushoto.ni Rashid Msemakweli(Dokta)Abdallah Kibadeni,Often Martin,Razak Yusuf,George Lucas,Iddi Seleman,Damian Kimti,Abdul Mashine,George Masatu,Entienne Eshete,Mzee Abdulrahman Muchacho.

Waliochuchumaa kutoka kushoto ni.Kasongo Athuman,Selemani Pembe,Edward Chumila,Dua Said,Fikiri Magoso,Malota Soma na Mohamed Mwameja.
Hii ilikuwa ni mechi ya Simba na Yanga (Simba ilishinda 1-0 mfungaji Dua Said.)Nahodha wa Simba siku hii alikuwa ni Rashid Abdallah Magongo ambae hayupo  pichani, alikuwa na waamuzi pamoja na Nahodha wa Yanga Keneth Mkapa.

ALIYEKUWA  mchezaji wa Simba miaka kumi na tano iliyopita George Magere Masatu, amesema kuwa kwa sasa yuko tayari kurejea kwenye timu hiyo.
 

Masatu hivi sasa amerejea nchini akiwa tayari amestaafu soka lakini ana kadi ya uanachama wa timu hiyo yenye maskani yake Msimbazi jijini Dar es Salaam.

Masatu amesema kuwa yuko tayari kurejea kama kocha na siyo mchezaji tena kama ilivyokuwa awali Masatu alisema kuwa, ana uwezo na uzoefu kufundisha aliyoupatia katika shule ya soka ya Arsenal huko Indonesia alikokuwa akicheza soka la kulipwa kwa zaidi ya miaka mitano.
 

“Kweli nimerudi nyumbani kuendelea na maisha, lakini ukisema kuhusu Simba mimi ni mwanachama.Na kama wakisema nifanye nao kazi,niko tayari haina shida
 

“Nimekuwa kocha kwenye shule ya watoto ya Arsenal kule Indonesia kwa zaidi ya miaka mitatu. Ninajua kazi inavyofanyika na wakisema wanataka tufanye kazi, basi tutafanya hivyo,” alisema Masatu aliyekuwa beki kisiki wakati wa enzi zake.
 

Masatu alianza kufanya vizuri akiwa na Pamba ya Mwanza kabla ya kujiunga na Simba mwanzoni mwa miaka ya 1990.
Pamoja na kuwa na umbo dogo, Masatu alikuwa ndiye beki nyota na imara zaidi wa kati nchini na jina lake halijawahi kushuka chati pamoja na kuwa nje ya Tanzania kwa muda mrefu.

Read more...

BAN KI MOON ALAANI MAUAJI YA WANAJESHI WA TANZANIA DARFUR

0 comments


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UNO), Ban K-Moon(pichani), amesema amesikitishwa na kuhuzunishwa na mauaji ya askari saba wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), lililofanywa na waasi wa Sudan Julai 13, mwaka huu.
Askari hao wa JWTZ waliokuwa Darfur, Sudan ya Kusini kulinda amani kwa mujibu wa UNO, walishambuliwa na waasi hao karibu na kambi ya Manawashi eneo la Khor Abeche, mji wa Darfur Jimbo la Nyala ambapo pia askari wengine 17 walijeruhiwa baadhi yao vibaya.
Katika salamu zake hizo kupitia kwa Msemaji wake, Katibu Mkuu huyo wa Uno, ameelezea masikitiko yake kuhusiana na vifo hivyo na kutoa pole kwa familia za marehemu waliokuwa wakilinda amani, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Vikosi vya Umoja wa Afrika kwa Umoja wa Mataifa vya Kulinda Amani (Unamid).

Ban K-Moon amelaani shambulio hilo dhidi ya Unamid na kuelezea matumaini yake kwamba Serikali ya Sudan itachukua hatua zinazofaa kuhakikisha kwamba wahusika wanafikishwa mbele ya sheria.
Wakati huo huo, Taarifa iliyotolewa na Unamid juzi jioni ilisema wajumbe wa Baraza la Usalama wanalaani kwa nguvu zote mashumbulizi hayo dhidi ya askari wa vikosi vya Unamid.
"Wajumbe wa Baraza la Usalama wameelezea masikitiko yao na kutuma salamu za pole kwa familia za marehemu hao pamoja na kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Aidha, wameitaka Sudan kufanya upelelezi wa kina kuhusiana na tukio hilo na kuwafikisha wahalifu hao mbele ya mkono wa sheria.
Taarifa hiyo ya Unimad iliongeza kuwa shambulio lolote dhidi ya vikosi vya Unimad halikubaliki na kuonya kuwa lisitokee tena shambulio lingine la aina hiyo huku ikisisitiza pande zinazovutana Darfur kushirikiana kwa lengo la kufikia malengo yaliyokusudiwa.


Read more...

USHINDI WA ARSENAL WAFANYIWA PROPAGANDA ZA KISIASA INDONESIA

0 comments
Sege Gnaby wa Arsenal akikwepa daruga la mchezaji wa Indonesia, Roby
Mgombea urais katika uchaguzi wa Rais wa 2014 kupitia Chama cha Great Indonesia Movement Party (Gerindra) Jenerali mstahafu Prabowo Subianto ameutumia mchezo kati ya timu ya taifa ya nchi hiyo na Arsenal kuishambulia serikali iliyo madarakani katika hotuba ya mkutano wa Kampeni za uchaguzi wa Rais wa nchi hiyo wa mwaka 2014

Baada ya timu ya taifa ya Indonesia kupokea kipigo cha goili 7-0 kutoka Gunners mgombea Prabowo aliilaumu serikali kwa kutoisimamia vizuri timu hiyo  na kuahidi iwapo ataingia madarakani kama rais wa Indonesia atahakikisha kikosi cha timu ya taifa kinafanya vizuri katika mechi zake

"
 Iweje hata timu yetu ya taifa inashindwa kwenye mechi na wachezaji 11 wa ngazi ya klabu.Tutahakikisha tunalipa umuhimu wa pekee suala zima la timu ya taifa.Kwa hiyo ninachofikiri ni kwamba matatizo haya yanasababishwa na udhaifu katika uendeshaji,na uwezo mdogo wa kufikiri.Matatizo katika uongozi.Tunataka Indonesia iwe na timu ya taifa iliyo imara"
 Jenerali Prabowo ambaye aliwahi kuwa askari wa kikosi maalum,aliwahi kuwania kiti cha umakamu wa rais 2009 ambapo alibwagwa na mpinzani wake Megawati Sukamoputri.Ni mmoja kati ya wagombea wanaopewa nafasi kubwa ya kuingia ikulu ya nchi hiyo ya mashariki ya mbali 2014

Read more...

ASKARI POLISI AELEZEA KILICHOTOKEA KATIKA SHAMBULIO LA DARFUR

0 comments
Askari wa JWTZ walionusurika wakiwa Hospitali

WAKATI Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), likiwa bado halijatangaza rasmi majina ya wapiganaji wake waliofariki huko Sudan, askari polisi aliyeko huko ameeleza chanzo na mazingira ya tukio hilo. Wapiganaji saba na wengine 14 walijeruhiwa Jumamosi iliyopita.

Askari polisi huyo anayefanya kazi katika Mji wa Nyala uliopo Darfur, alisema mauaji hayo yalitokea wakati askari hao walipokuwa wakifuatilia magari yao yaliyokuwa yameporwa na kundi mojawapo la waasi.
Usalama katika Mji wa Nyala ambao ndiyo mkubwa zaidi katika eneo la Darfur, umekuwa mdogo katika siku za hivi karibuni. “Wale wanajeshi walikuwa doria ya kawaida, ila kama wiki moja iliyopita waasi walivamia tena doria ya wanajeshi wetu na kupora magari manne bila kuua mtu.
 
Miili ya askari wa JWTZ waliouawa Darfur ikipewa heshima za mwisho
“Siku ya mauaji hayo wanajeshi wetu wakiwa tena katika doria waliyaona yale magari yaliyoporwa kwa mbali yamepaki, waliyafuatilia, walipokaribia kumbe ulikuwa mtego, wakashambuliwa,” alisema askari huyo na kuongeza: “Mauaji hayo yametokea takriban kilometa 70 kutoka katika kambi niliyopo mimi, lakini wote tupo eneo la kusini na hiyo kambi ya Korabeche inaongozwa na jeshi letu.” Tofauti na chanzo chetu cha habari huko Darfur, Kanali Mgawe alisema wanajeshi hao walishambuliwa walipokuwa kwenye msafara wa kusindikiza walinzi wa amani.
Askari huyo aliyeko Darfur alisema: “Makundi yanayopambana huku yapo mengi ila makubwa yapo kama matano. Kuna moja linaitwa Jeshi la Ukombozi la Watu wa Sudan (SPLA), ambalo limegawanyika katika makundi mawili pia kuna mengine kama JEM, Janjaweed na mengineyo.”
 
Akizungumzia mshtuko walioupata baada ya mauaji hayo, askari huyo alisema wafanyakazi wote wanaohusika na ulinzi wa amani wamepatwa na ganzi… “Huku kwa kweli hali imekuwa chungu, tangu askari hao wauawe hali haitabiriki kabisa, tupo nje hapa (hospitali walimohifadhiwa), tunasubiri uhakika.”
 
“Hawa jamaa (waasi), wamesheheni silaha na wana vifaa vya kisasa kiasi kwamba hata ndugu zetu walizidiwa kutokana na wenzao kuwa na silaha nzito, nikija Tanzania nitakuonyesha picha za mapambano yao,” alisema. Akizungumzia kazi ambazo polisi wanazifanya huko, alisema hawaruhusiwi kushika silaha, bali kuwashirikisha wananchi katika masuala ya amani.
 
“Sisi majukumu yetu ni kuungana na jamii na kuwafundisha masuala mbalimbali, hivyo sisi tunawasiliana moja kwa moja na wananchi waliopoteza makazi kisha tunaandaa taarifa. Haturuhusiwi kushika silaha, wanajeshi wao wanatulinda na kusimamia usalama na kutusindikiza wakati wa doria,” alisema.
 
“Huku hali ya usalama haitabiriki. Mpaka sokoni tunakwenda chini ya ulinzi.”  Akizungumza kwa simu jana, Kanali Mgawe alikanusha uvumi wa majina yaliyosambaa mitandaoni huku akisema kwa utaratibu uliopo, jeshi haliwezi kutangaza majina hayo hadi ndugu watakapotaarifiwa. “Hayo majina yanayotajwa kwenye mitandao ni ya uongo. Kwa sasa mimi sijaletewa majina na utaratibu uliopo ni hadi ‘next of kin’ (ndugu) wao wajulishwe kwanza,” alidai Kanali Mgawe.
 
Hata hivyo, alisema Tanzania imewasilisha maombi ya kubadilisha kanuni za kulinda amani ikitaka kuruhusiwa kujihami kwa silaha za moto pale wanajeshi wake wanaposhambuliwa kwa kutumia kanuni namba saba ya Sheria za Majeshi ya Kulinda
Read more...

VITAMBULISHO VYA TAIFA:MAMLAKA YAANZA KUCHUKUA ALAMA ZA VIDOLE,SAINI NA PICHA

0 comments
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), imeanza zoezi la kuchukua alama za vidole vyote kumi, kupiga picha na kuweka saini ya kielektroniki kwa wakazi wa Wilaya ya Temeke tayari kwa kutoa vitambulisho hivyo.
Kaimu Mkuu wa Mawasiliano na Machapisho, Thomas William aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, kutokana na wingi wa watu katika Jiji la Dar es Salaam, zoezi hilo limegawanywa katika ngazi ya wilaya hadi wilaya.
“Hili zoezi tumelianza juzi, tunachukua alama za vidole kumi, kupiga picha na kuweka saini za kielektroniki kwa wakazi wa Temeke, tumeanzia Kigamboni na kutokana na ukubwa wake tumeigawanya kwa kanda saba,” alisema.
  William alisema,  kanda ya kwanza inahusisha mitaa yote katika kata za Kimbiji, Pemba Mnazi, Kigamboni, Vijibweni, Kibada, Mji Mwema, Somangila, Kisarawe 11, Tungi na mitaa ya Mtoni Kijichi, Mgeni nani na Misheni iliyoko katika Kata ya Kijichi.
Alisema, ili kuboresha mwonekano mzuri wa picha kwenye kitambulisho hicho, mwombaji anashauriwa kutokuvaa nguo nyeupe, kijivu, bluu mpauko, pinki na kofia au kapelo wakati wa kupiga picha.
Aidha, William aliwataka waajiri wa mashirika mbalimbali kuwaruhusu watumishi kushiriki katika zoezi hilo siku watakayokuwa wamepangiwa ili kurahisisha zoezi hilo na kuepuka usumbufu wa kurudia eneo.
“Tunawaomba waajiri katika mashirika mbalimbali nchini wawaruhusu watumishi wao kufika katika eneo muhimu kwa kuzingatia tarehe aliyopangiwa ili kufanikisha zoezi. Hata wale ambao walikuwa hawajajaza fomu za kujiandikisha wanatakiwa kufika katika kata zao ikiwa zoezi linafanyika katika halmashauri hiyo,” alisema William.
Alisema, zoezi hilo limetoa kipaumbele kwa makundi maalumu ya walemavu na wazee wasiojiweza na kuwa walemavu wa mikono watapigwa picha bila kuchukuliwa alama za vidole.
Katika Jiji
la Dar es Salaam, zoezi hilo limeanzia Wilaya ya Temeke, likifuatiwa na Ilala na kumalizikia Kinondoni
Read more...

Sunday, July 14, 2013

MUNGU KAINGILIA KATI?MALAIKA JIBRIL(GABRIEL)`AONEKANA KWENYE MAANDAMANO` MISRI

0 comments

Waandamanaji wanaomuunga mkono Rais Morsi,wamedai kuwa wameona mwanga wa aina yake..

Kwa mujibu wa gazeti la Al Arabia,taarifa hizi zimetolewa na muhubiri mmoja anayeegemea upande wa Morsi,wakati akiwahutubia wafuasi wa Morsi katika viwanja vya Rabia all-Adawiya jijini Kairo,

Katika hotuba hiyo iliyorushwa na vituo kadhaa vya televisheni vya Misri,muhubiri huyo amesema kuwa malaika Jibril ameonekana miongoni mwa wafuasi wa Morsi wanaoandamana

Muhubiri huyo Sheikh Ahmad Abdel Hadi kutoka kikundi cha Muslim Brotherhood amesisitiza kuwa watu wanaoheshimika kutoka Madina Al-Munawara, Saudi Arabia, wamemueleza kuhusu ndoto malaika Jibril alivyotokea na kuingia kwenye msikiti wa Rabia aL-Adawiya na kuwataka watu wanaoswali wakae kama walivyo.

Vile vile kuna taswira nyingine ilyotokea ya Mtume Muhammad(SAW)amejumuika na Bw Morsi na watu kadhaa.Katika taswira hiyo anasema muda wa swala ulipofika,watu walimuomba Muhammad(SAW)aongoze swala lakini Mtume alimteua Morsi aongoze swala

Muhubiri huyo amesema mtu mwingine wa kuaminika ametokewa na taswira inayoonesha ngamia wapatao 50,pamoja na vijana nawatoto kadhaa wakiwa jangwani.Baada ya muda wale ngamia,vijana na watoto wakaanza kusikia kiu kali.Walianzakuswali kumuomba Mungu awasaidie na papo hapo ardhi aligawanyika na che chem ya maji ikatokea.Baada ya kumaliza kiu yao,sauti ikasikika ikiwaambia vijana `watunzeni ngamia wa Rais Mohammed Morsi`


Wakati huo huo Sheikh Mosad Anwar wa Misri amemfananisha Morsi na Nabii Yusuf,kwa kuwa wote wametawala baada ya kupitia misukosuko kwa miaka mingi ikiwa pamoja na kuwekwa kizuizini mara kwa mara

Katika hatua nyingine Sheikh Shawki Abdel Latif mwakilishi wa Wizara ya Awqaf(Kusimamia Msaada ya Kijamii)ameibeza kauli ya muhubiri Abdel Hadi kwa kusema kuwa "..ndoto kama hizo zimelenga katika kuhalalisha vitu visivyofaa vionekane kuwa vinafaa,Wanaweka sumu kwenye asali kwa  kuongea uongo juu ya Mtume Muhammad,amani iwe juu yake"
Shekh huyo alipoulizwa zaidi na gazeti la Al Arabiya kuhusu uwezekano wa malaika Jibril kutokea katika msikiti wa Rabia al-Alawiya alijibu:"Huo ni uongo pia,Jibril ni Malaika na hutokea mbele ya Mtume wa Mungu tu"

"Maneno kama hayo ni njia ya kujaribu kutumia dini kwa manufaa ya kisiasa na kutaka kuhalalisha utawala wa Rais Morsi" Aliongeza Sheikh Abdel Latif
Sheikh Abdel Latif hakuishia hapo,alipendekeza kukamatwa kwa watu wanaoeneza habari kuhusu ndoto ya Mtume Muhammad akimwambia Morsi aongoze swala kwani kauli hiyo ni `tusi` kwa Uislam na Mtume mwenyewe

Makumi Elfu ya waandamanaji wanaomuunga mkono Rais Morsi walimiminika mitaani kwa wingi kuanzia juzi Ijumaa,wakiapa kupambana ili BwMorsi arejeshwe madarakani huku watu wanaounga mkono kupinduliwa kwa Rais Morsi wakiendelea na maandamano na kuweka pabaya mustakabali wa kisiasa wa Misri.

Chama cha Muslim Brotherhood,alikotokea Rais Morsi kinazidi kusambaratika kufuatia kukamatwa kwa viongozi waandamizi kadhaa na wengine kukimbilia kusikojulikana kufuatia mapinduzi ya Julai 3,ambayo chama hicho na wafuasi wake kimeyaita ni ya kijeshi.

Milio ya risasi katika eneo la jeshi jumatatu ya mwanzoni mwa wiki inayokwisha,imewaacha  makumi ya watu wakipoteza maisha yao na wengine makumi kujeruhiwa kulingana na takwimu za Wizara ya Afya ya nchi hiyo
 
Read more...
 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797