Askari wa JWTZ walionusurika wakiwa Hospitali |
WAKATI Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), likiwa
bado halijatangaza rasmi majina ya wapiganaji wake waliofariki huko
Sudan, askari polisi aliyeko huko ameeleza chanzo na mazingira ya tukio
hilo. Wapiganaji saba na wengine 14 walijeruhiwa Jumamosi iliyopita.
Askari polisi huyo anayefanya kazi katika Mji wa Nyala uliopo Darfur, alisema mauaji hayo yalitokea wakati askari hao walipokuwa wakifuatilia magari yao yaliyokuwa yameporwa na kundi mojawapo la waasi.
Usalama katika Mji wa Nyala ambao ndiyo mkubwa zaidi katika eneo la Darfur, umekuwa mdogo katika siku za hivi karibuni. “Wale wanajeshi walikuwa doria ya kawaida, ila kama wiki moja iliyopita waasi walivamia tena doria ya wanajeshi wetu na kupora magari manne bila kuua mtu.

Miili ya askari wa JWTZ waliouawa Darfur ikipewa heshima za mwisho |
“Siku ya mauaji hayo wanajeshi wetu wakiwa tena katika doria
waliyaona yale magari yaliyoporwa kwa mbali yamepaki, waliyafuatilia,
walipokaribia kumbe ulikuwa mtego, wakashambuliwa,” alisema askari huyo
na kuongeza: “Mauaji hayo yametokea takriban kilometa 70 kutoka katika
kambi niliyopo mimi, lakini wote tupo eneo la kusini na hiyo kambi ya
Korabeche inaongozwa na jeshi letu.”
Tofauti na chanzo chetu cha habari huko Darfur, Kanali Mgawe alisema
wanajeshi hao walishambuliwa walipokuwa kwenye msafara wa kusindikiza
walinzi wa amani.
Askari huyo aliyeko Darfur alisema: “Makundi yanayopambana huku yapo mengi ila makubwa yapo kama matano. Kuna moja linaitwa Jeshi la Ukombozi la Watu wa Sudan (SPLA), ambalo limegawanyika katika makundi mawili pia kuna mengine kama JEM, Janjaweed na mengineyo.”

Akizungumzia mshtuko walioupata baada ya mauaji hayo, askari huyo
alisema wafanyakazi wote wanaohusika na ulinzi wa amani wamepatwa na
ganzi… “Huku kwa kweli hali imekuwa chungu, tangu askari hao wauawe hali
haitabiriki kabisa, tupo nje hapa (hospitali walimohifadhiwa),
tunasubiri uhakika.”
“Hawa jamaa (waasi), wamesheheni silaha na wana vifaa vya kisasa
kiasi kwamba hata ndugu zetu walizidiwa kutokana na wenzao kuwa na
silaha nzito, nikija Tanzania nitakuonyesha picha za mapambano yao,”
alisema.
Akizungumzia kazi ambazo polisi wanazifanya huko, alisema
hawaruhusiwi kushika silaha, bali kuwashirikisha wananchi katika masuala
ya amani.
“Sisi majukumu yetu ni kuungana na jamii na kuwafundisha masuala
mbalimbali, hivyo sisi tunawasiliana moja kwa moja na wananchi
waliopoteza makazi kisha tunaandaa taarifa. Haturuhusiwi kushika silaha,
wanajeshi wao wanatulinda na kusimamia usalama na kutusindikiza wakati
wa doria,” alisema.
“Huku hali ya usalama haitabiriki. Mpaka sokoni tunakwenda chini ya ulinzi.”
Akizungumza kwa simu jana, Kanali Mgawe alikanusha uvumi wa majina
yaliyosambaa mitandaoni huku akisema kwa utaratibu uliopo, jeshi
haliwezi kutangaza majina hayo hadi ndugu watakapotaarifiwa. “Hayo
majina yanayotajwa kwenye mitandao ni ya uongo. Kwa sasa mimi sijaletewa
majina na utaratibu uliopo ni hadi ‘next of kin’ (ndugu) wao wajulishwe
kwanza,” alidai Kanali Mgawe.
Hata hivyo, alisema Tanzania imewasilisha maombi ya kubadilisha
kanuni za kulinda amani ikitaka kuruhusiwa kujihami kwa silaha za moto
pale wanajeshi wake wanaposhambuliwa kwa kutumia kanuni namba saba ya
Sheria za Majeshi ya Kulinda
0 comments:
Post a Comment