Hapa alikuwa akilishwa chakula na Bwana Harusi Mtarajiwa aliyetajwa kuwa ni Kasisi Masawe wakati wa tafrija ya kuagana na familia maarufu kama SEND-OFF |
Kifo hicho kilichotokea Jumamosi mwishoni mwa wiki
iliyopita, kimekuwa gumzo mjini Handeni hukufamilia ya marehemu aliyejitambulisha
kwa jina la Firmin Mrimasha, alisema kuwa chanzo cha kifo cha Levinwananchi wakisema kuwa ni
tukio ambalo halijawahi kutokea katika wilaya hiyo.
Msemaji wa a
ambaye alijifungua mwanzoni mwa wiki iliyopita,ilikuwa ni homa
aliyoipata ghafla siku ya Alhamisi na kupelekwa katika Hospitali ya
Wilaya ya Handeni na kukutwa na malaria na kisha kulazwa kwa matibu.
“Huyu bibi harusi alikuwa ametoka kujifungua,
alikuwa na mtoto wa kiume kutokana na ujauzito wa miezi saba, ndipo
ghafla Alhamisi akapata homa tukampeleka hospitali alikolazwa na baada
ya kupata nafuu, aliruhusiwa Ijumaa.
“Baada ya kuruhusiwa akaanza maandalizi ya harusi
na Jumamosi ambayo ndiyo siku ya ndoa yake, alijiandaa lakini ilipofika
saa 8.05 akafariki dunia akiwa nyumbani akisubiriwa kwenda kanisani
kufunga ndoa ambayo ilikuwa ifungwe saa 9.00,” alisema Mrimasha.
Alisema, “Inasikitisha sana ila imeshatokea yaani
marehemu amefariki saa moja kabla ya ndoa yake na baada ya kifo hicho,
mtoto wake naye alifariki muda mfupi baada ya mama yake kufariki dunia,”
alisema Mrimasha.
Akizungumzia mkasa huo, Mwenyekiti wa Kamati ya
Harusi hiyo iliyogharimu Sh7.7 milioni, Abdi Kipacha alisema kuwa kwake
ni tukio la kwanza kutokea tangu kuzaliwa kwake na kamwe hawezi
kulisahau.
“Nilishazipangia kazi kamati za maandalizi, lakini
ghafla tukapewa taarifa kuwa bibi harusi amefariki...Hatukuamini,
ikabidi niwatangazie wanakamati wenzangu kuwa hakuna tena shughuli, bibi
harusi amefariki,” alisema mwenyekiti huyo wa kamati na kuongeza:
“Kitu tulichokuwa tukisubiri ni kuambiwa bibi
harusi angefika saa ngapi, lakini ghafla tukapewa taarifa za kifo,
ilikuwa ni vigumu kuamini lakini ni kweli imetokea na inasikitisha kwani
si jambo la kawaida,” alisema Kipacha.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na wanandugu ni
kuwa marehemu alikuwa Mwalimu wa Shule ya Msingi Nndawa mkoani Lindi na
kwamba alikuwa katika kundi la walimu wa ajira mpya ambayo hadi mauti
yanamkuta alikuwa hajapokea hata mshahara wake wa awali.
Akizungumzia hali hiyo, Padri aliyekuwa afungishe
ndoa hiyo, Max Sabuni wa kanisa hilo Katoliki Handeni alisema:
“Nimesikitishwa na tukio hili kwa kuwa halikuwahi
kunitokea...Kilichobaki ni wanandugu kuwa watulivu kwa kuwa Mungu
amechukua kiumbe wake kwa muda alioupanga.”
Aliwataka ndugu, jamaa na marafiki kuwa na subira katika kipindi hiki cha majonzi
0 comments:
Post a Comment