Familia
ya mwanafunzi mtanzania aliyeuwa mjini washington DC, marehemu Omary
Sykes inatarajiwa kuingia nchini Marekani leo hii, swahili TV inaripoti.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu faimilia hiyo itaongozwa na baba wa marehemu
bwana Adamu Sykes na baba mkubwa wake bwana Ilyasa Sykes.
Marehemu
ambaye alikuwa na miaka 22, ni mjukuu wa mpigania uhuru maarufu wa
Tanzania mzee Kleist Abdulwakili sykes na pia ni ndugu wa msanii star
wa bongo Flava Dully Sykes.
Omar
aliuawa kwa shambulio la risasi karibu na maeneo ya chuo anachosoma
cha Howard University usiku wa alhamisi julai 4, 2013 akiwa na mwenziwe
katika mtaa wa Fairmont North West, kwa mujibu wa Polisi Washington DC
(MPDC) na Polisi wa chuo hicho (HPD), watu wawili ndio wanaoshukiwa
kuhusika na mauaji hayo.Wahusika bado hawajatiwa mbaroni.
Kwa
mujibu wa habari za ndani za jeshi hilo la Polisi, kitengo maalum cha
uchunguzi wa mauaji kilichaanza upelelezi mkali ukiongozwa na Bwana
Gabriel Truby wa MPDC na wameieleza Swahili TV*, licha ya upepelezi
wanaoendelea nao pia wanaomba ushirikiano wa wananchi kwajili ya
kufanikisha uchunguzi wao. zawadi ya dola 25,000 itatolewa kwa yeyote
atakayefanikisha kukamatwa kwa wauaji hao.
Maripota
wa Swahili TV wamefanikiwa kufanya mawasiliano na kitengo cha mauaji
cha MPDC, Howard University Polisi pamoja na familia ya marehemu Omar
Sykes, kwa mujibu wa maelezo yao mwili wa marehemu bado upo hospitalini
kwa ajili ya uchunguzi na swahili TV inaahidi kuwaletea habari zote
zinazohusiana na upelelezi huu.
0 comments:
Post a Comment