Vitendo vya ukatili dhidi
ya watoto na wanawake jijini mbeya vimeendelea chukua sura mpya baada ya dereva wa daladala jijini humo
kumzalisha mwanafunzi wa Masomo ya jioni kituo cha Juhudi kilichopo Ilomba.
Tukio hilo limetokea hivi karibuni eneo la mama John Mtaa wa Ihanga Kata ya
Ilomba ambapo dereva wa daladala aliyefahamika kwa jina la Aswile Mwalukoba (45
) kubwagiwa kichanga wa miezi saba ambaye alikwishafariki baada ya kuugua kwa muda
mfupi.
Akizungumzia tukio hilo Mwenyekiti Mtaa huo Ndugu Emanuel Mwasibata amesema kuwa mgogoro huo umetokana na dereva huyo kugoma kuuzika mwili huo kwa kile alichodai kuwa hivi sasa haishi na binti huyo kwa muda mrefu sasa.
Kwa upande wake binti huyo
aliyefahamika kwa jina la Calorina Kyando amedai kuwa uamuzi wa yeye
kuuchukua mwili wa mtoto huyo hadi kwa baba yake unatokana kutelekezwa na bwana huyo kisha kupigwa
marakwa mara na kusababishiwa ulemavu wa sikio la kushoto baada ya kung’atwa na
mwanaume huyo.
Mwili wa mtoto ukiwa umewekwa kwenye sofa nyumbani kwa Bw.Aswile |
Mwanamke huyo amefafanua kuwa
mara baada ya mtoto huyo kufariki wakati akipatiwa matibabu katika Hospital ya
Igawilo jijini humo aliamua kumpigia simu mzazi mwenzie kwa lengo la kumpa
taarifa za msiba huo.
Amesema mara baada ya kutoa
taarifa hiyo, mwanaume huyo alikubali na kumueleza mwanamke huyo kuwa yuko
tayari kumzika mtoto huyo na kwamba anafanya taratibu za kuwasiliana
na ndugu zake walioko Tukuyu Wilayani Rungwe
Carolina Kyando (kushoto)akiwa na dada yake wakiwa nyumbani kwa Bw.Aswile |
Amesema katika siku iliyofuata
mwanaume huyo hakupatikana kwa simu ya kiganjani na wala hakuwepo nyumbani
kwake anapoishi eneo la Mama John, hali iliyopelelekea baadhi ya majirani pamoja na
mwanamke huyo kutoka Uyole kusaidiana na kuutoa mwili huo Hospitalini hapo kwa
lengo la kufanya taratibu nyingine .
Baada ya kushauriana mwanamke huyo na majirani hao waliamua
kuchukua maiti hadi nyumbani kwa Mwalukoba ambapo waliiweka kwenye kiti
ndani ya nyumba yake huku wakiendelea kumsubiri mwalukoba arudi aliko ambapo baadaye alirudi nyumbani hapo
akisindikiazwa na Mdogo wake aliyefahamika kwa jina Gabriel Mwalukoba hadi
nyumbani hapo.
Wakazi wa Uyole wakijadiliana baada ya kumkosa Bw.Aswile |
Kitendo hicho cha kurejea kwa mwanaume huyo kilifanya mwenyekiti wa mtaa huo Ndugu Emanuel Mwasibata kuhoji juu ya kutoweka kwa nyumbani kwakwe kwa muda wa siku mbili huku kukiwa hakuna mawasiliano yoyote.
Bw.Aswile (aliyeshoka gongo)baada ya kurudi nyumbani |
Baada ya kikao cha muda mrefu kati ya pande zote mbili mwanaume huyo alikubali kuupokea mwili huo na hivyo kuanza kufanya taratibu za mazishi ambapo mazishi hayo yalifanyika katika makaburi ya Iyela mida saa 12 jioni na kuhudhuriwa na familia zote mbili pamoja na majirani wengine kutoka Uyole na Mama John
Majirani kutoka pande zote mbili wakisubiri muafaka wa kikao |
0 comments:
Post a Comment