Pages

 

Monday, July 8, 2013

TAHADHARI:USINYWE MAFUTA YA UBUYU NI HATARI

0 comments
  Mamlaka inayosimamia ubora wa Vyakula na Madawa nchini TFDA imeutahadharisha umma wa Watanzania juu ya hatari inayoweza kuwakuta watu wanaokunywa mafuta ya ubuyu kama tiba.

Mbuyu ambao kisayansi unajulikana kama Adansonia Digitata,Nimmea wa jamii ya miti na umetapakaa sehemu nyingi duniani na watu hutumia matunda ya mti huu kuburudisha mdomo,kuanda juisi na hivi karibuni umeingia kwenye dawa za asili zenye uwezo wa kutibu maradhi mbalimbali kwa wakati mmoja.

Pia mamlaka hiyo imeonya watu dhidi ya tabia ya kutumia dawa bila kupata ushauri wa kitaalam kutoka kwa mtaalam aliesomea mambo ya dawa za binadamu

Mamlaka hiyo iliyopewa dhamana ya kusimamia ubora wa chakula na dawa nchimi,imetahadharisha juu ya matumizi holela ya dawa za aina ya Diclopa na Diclofenac,ambazo watu wengi hutumia kukabiliana na maumivu,kwa kuwa huwa zinasababisha matatizo mwili kwa baadhi ya watumiaji.

TDFA pia imeshauri watanzania kuendelea kutumuia mafuta ya ubuyu kama vipodozi tu na sio kunywa.

Akiongea katika maonesho ya 37 ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar Es Salaam,msemaji wa TDFA Bi Gaudensia Simwanza amesema watanzani waache kunywa mafuta ya ubuyu

Baadhi ya wachuuzi wa mafuta hayo wanadai kuwa dozi ya mafuta hayo ambayo hupimwa kwa kijiko kidog cha chai inauwezo wa kutibu maradhi tofauti,ikiwemo Shinikizo kubwa la damu,kisukarina matatizo ya tumbo.

Bi Simwanza amesema baada ya kufanyia vipimo mafuta hayo,imegunduliwa kuwa yana kemikali hatari ambazo hazitakiwi ziingie ndani ya mwili wa binadamu na hivyo kufanya mafuta hayo yasifae kunywa hadi kemikali hizo zitakapokuwa zimeenguliwa kutoka kwenye mafuta hayo.

Amesema teknolojia ya kuondoa kemikali kutoka kwenye mafuta hayo kwa sasa haipo hapa nchini,hivyo watu waache kunywa mafuta hayo hadi teknolojia hiyo itakapopatikana

"Hivi karibuni taifa limekuwa likishuhudi a kukua kwa biashara ya mafuta ya ubuyu.Wafanyabiashara wamekuwa wakizunguka kila kona wakiyatangaza kuwa yana uwezo wa kutibu maradhi mengi kwa dozi moja.Tunataka umma utambue kuwa anaekunywa mafuta hayo ana hatarisha maisha yake..kuna aina ya acid ambayo ina chechembe zinazosababisha maradhi ya kansa."Alisema

Nae Naibu wa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr Seif Rashid amepemdekeza serikali ianzishe kampeni ya kuelimisha watu juu ya madhatra ya kutumia dawa bila ushauri wa wataalam.

"Matumizi ya Diclopa ,Diclofenac au na zingine zote zile lazima yafanywe kwa uangalifu mkubwa ,kwa kuwa hakuna dawa ambayo ni salama kwa asilimia 100"

Dr Rashid amesema taifa bado linakabiliwa na uhaba wa wataalam wa kutoa dawa na wahudumu ili dawa ziweze kusimamiwa na kutolewa kitaalam

Amesema juhudi zinaendelea kuhakikisha vituo vya kutoa dawa vilisajiliwa vinaongezeka nchi nzimaikiwa ni pamoja na kuwanoa vya kutosha wahudumu wa kwenye vituo hivyo.

Ni pale watanzania watakapozifahamu sheria na taratibu zinazosimamia uuzaji na ugawaji wa dawa,ndipo watakapokuwa makini na ununuzi na utumiaji wa dawa husika

0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797