Pages

 

Wednesday, July 10, 2013

"MANDELA SASA ANAFUNGUA MACHO NA KUTABASAM"-WAJUKUU

0 comments
Swati Dlamini (kushoto) na Zaziwe Dlamini-Manaway (kulia)
Wajukuu wawili wa Rais Mweusi wa Kwanza wa Afrika Kusini Nelson Mandela,waliuvamia mtandao wa Twitter na kudumu humo kwa masaa tisa wakijibu maswali juu ya maendeleo ya afya ya kiongozi huyo wa zamani. na mzozo wa kiukoo unaofukuta juu  ya eneo la maziko

Zaziwe Dlamini-Manaway na Swati Dlamini wamesema babu yao sasa anweza kutabasam na kuwa ukoo bado umefungamana

Wajukuu hao walikuwa wakishiriki katika kipindi cha Tv kinachohusu maisha halisi (Reality Tv)kiitwacho `Being Mandela` ambacho kimeanza kuoneshwa nchini Marekani.

Bw.Mandela amelazwa hospitali akiwa mahututi katika mji mkuu wa Afrika Kusni, Pretoria.

Alikimbizwa hospitalini zaidi ya mwezi mmoja uliopita kutokana na kusumbuliwa na maradhi yaliyoshambulia mapafu yake

Taarifa iliyotolewa jana na Ofisi ya Rais wa nchi hiyo ilisema Bw. Mandela bado hali yake si shwari ila imeimarika.

Mandela aliwekwa kizuizini kwa miaka 27 kutokana na harakati zake za kupinga utawala wa kikandamizaji wa wazungu wachache,kabla hajachiwa mwaka1990, na miaka minne baadae alichaguliwa kuwa Rais wa Afrika Kusini.Aliachia ngazi baada ya kutawala kwa miaka mitano.

Wiki mbili zilizopita mzozo uliibuka katika ukoo wa Bw.Mandela juu ya eneo la kuzikia na masalia ya watoto wake watatu ambao walifariki katika miaka ya 1947,1969 na 2005.

Mahakama iliamuru masalia ya watoto hao wa Mandela yahamishwe kutoka Mvezo,mji aliozaliwa Bw.Mandela ,na yapelekwe yakazikwe Qunu,katika Jimbo la Eastern Cape, anapoishi baada ya kustaafu.

Kesi ilifunguliwa na jamaa 16 wa ukoo huo ambao walipinga kitendo cha mjukuu wa kiume wa Bw.Mandela, Mandla. kufukua masalia ya watoto hao wa Bw. Mandela na kuyahamisha na kuyapeleka Mvelo bila kufuata taratibu, akitegemea Bw.Mandela azikwe huko pia.

Katika kujibu maswali waliyoulizwa wajukuu hao wawili wa Mandela walisema hawajivunii kuona jinsi mambo yalivyogeukia kuwa hivyo.

"Yameshatokea,ila mwisho wa siku bado tuko kama watu wa ukoo mmoja" waliandika kwenye mtiririko wa ujumbe katika ukurasa wa Twitter wa kipindi hicho cha  `Being Mandela`


Walipotakiwa kuelezea mipango ya ukoo katika kurudisha umoja wao,walijibu,"Tunawaruhusu wazee wa ukoo watuongoze.Umoja wetu haujapotea moja kwa moja,ni mwenzetu tu aliamua kufanya mabo tofauti,ila siku zote tutaendelea kumpenda binamu yetu (Mandla)"

Walipotakiwa kuzungumzia maendeleo ya afya ya Bw .Mandela walisema anafungua macho na kutabasam.

Mabinti hawa ni watot wa binti waNelson Mandela,Zenani kutoka katika ndoa yake na mkewe wa zamani Winnie Madikizela-Mandela.

Bw.Mandela alioa na kuacha mara mbili na sasa amemuoa aliekuwa mke wa Rais wa zamani wa Msumbiji Samora Machel,Graca.


0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797