Pages

 

Monday, July 8, 2013

NYATI WA AJABU AONEKANA NGORONGORO

0 comments
Wakati magwiji wa Sayansi ya Maisha ya Viumbe hai duniani wakidhani wametegua vitendawili vyote kuhusu maisha ya Viumbe hai vya msituni,kimetokea kitendawili kingine katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro,ambako ameonekana aina ya nyati isiyowahi kuonekana  hapa duniani,mwenye rangi isiyozoeleka miongoni mwa nyati waliozoeleka

Kwa kawaida nyati huwa na rangi nyeusi,lakini huyu alieonekana Ngorongoro amepambwa kwa rangi nyeupe -maziwa,akiranda randa katika maeneo ya bonde maarufu duniani la Ngorongoro,na tayari ameshawavuta wanaharakati wa mazingira,wanasayansi wa maisha ya viumbe hai na watafiti wa tabia za wanyamapori ambao wako Ngorongoro kumfuatilia.

"Kwa kweli  aina hii ni adimu sana na ni tukio la ajabu kwa upande wa watu wanaoshughulika na maisha ya viumbe vya misituni,kwa hapa Ngorongoro na nchi nzima kama ninavyojua."Alikiri kiongozi wa watafiti wa maisha ya viumbe hai katika Hifadhi ya Ngorongoro Bw Patrice Mattay
 
Watu wa kwanza kumuona nyati huyo katika hifadhi ya Ngorongoro ni maafisa wa Polisi wa kituo cha hapo Ngorongoro,ambao mwanzo walidai mara kwa mara kuona aina ya wanyama wa ajabu katika eneo lao la kazi,hasa nyakati za alfajiri.

Afisa Polisi JJ Paul ambae alikuwa zamu amethibitisha kukiona kiumbe hicho,"mwanzo nilipata habari zakuonekana kwa mnyama wa ajabu kutoka kwa maafisa polisi wenzangu,na hivi karibuni nilimshuhudia huyu nyati akila majani akiwa amejichanganya na wanyama wengine kwenye ukingo wa bonde"

Inasemekana kuwa eneo la Hifadhi ya Ngorongoro ina idadi ya nyati wa kawaida wapatao350 kati ya wanyama wapatao laki 3 wanaoishi ndani au kuzunguka bonde hilo kubwa na maarufu duniani.Lakini  huyu nyati mweupe ni aina ambayo haijazoeleka kuonekana katika jamii ya nyati ndani ya hifadhi hiyo.

Meneja anaehusika na hifadhi katika Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro Bw Amiyo T. Amiyo amesema kwamba ugunduzi huu wa nyati mwenye rangi nyeupe unahitaji wito wa kuanzisha aina mpya ya utafiti juu ya tabia za maisha ya wanyamapori.

Kawaida watafiti wengi waliegemea kwa jamii ya wanyama wanaokula nyama (carnivores) kama vile simba, mbwa-mwitu na cheetah,lakini sasa nyati wanaweza kuingia kwenye listi

0 comments:

Post a Comment

 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797