Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UNO), Ban K-Moon(pichani), amesema
amesikitishwa na kuhuzunishwa na mauaji ya askari saba wa Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ), lililofanywa na waasi wa Sudan Julai 13, mwaka huu.
Askari
hao wa JWTZ waliokuwa Darfur, Sudan ya Kusini kulinda amani kwa mujibu
wa UNO, walishambuliwa na waasi hao karibu na kambi ya Manawashi eneo la
Khor Abeche, mji wa Darfur Jimbo la Nyala ambapo pia askari wengine 17
walijeruhiwa baadhi yao vibaya.
Katika
salamu zake hizo kupitia kwa Msemaji wake, Katibu Mkuu huyo wa Uno,
ameelezea masikitiko yake kuhusiana na vifo hivyo na kutoa pole kwa
familia za marehemu waliokuwa wakilinda amani, Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Vikosi vya Umoja wa Afrika kwa Umoja wa Mataifa vya Kulinda
Amani (Unamid).
Ban
K-Moon amelaani shambulio hilo dhidi ya Unamid na kuelezea matumaini
yake kwamba Serikali ya Sudan itachukua hatua zinazofaa kuhakikisha
kwamba wahusika wanafikishwa mbele ya sheria.
Wakati
huo huo, Taarifa iliyotolewa na Unamid juzi jioni ilisema wajumbe wa
Baraza la Usalama wanalaani kwa nguvu zote mashumbulizi hayo dhidi ya
askari wa vikosi vya Unamid.
"Wajumbe
wa Baraza la Usalama wameelezea masikitiko yao na kutuma salamu za pole
kwa familia za marehemu hao pamoja na kwa Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Aidha, wameitaka Sudan kufanya upelelezi wa kina kuhusiana na tukio hilo na kuwafikisha wahalifu hao mbele ya mkono wa sheria.
Taarifa hiyo ya Unimad
iliongeza kuwa shambulio lolote dhidi ya vikosi vya Unimad halikubaliki
na kuonya kuwa lisitokee tena shambulio lingine la aina hiyo huku
ikisisitiza pande zinazovutana Darfur kushirikiana kwa lengo la kufikia
malengo yaliyokusudiwa.
0 comments:
Post a Comment