skip to main |
skip to sidebar
JESHI
la Polisi jijini Dar es Salaam, jana lililazimika kutumia mabomu ya
machozi maeneo ya Manzese, kuwatawanya wafanyabiashara wadogowadogo
(Machinga) waliogoma kupisha ujenzi unaoendelea wa mabasi yaendayo kasi
(DART).
Polisi wakiwa katika magari yao waliwatawanya
wafanyabiashara hao waliokuwa wamegoma kutoka kutokana na kudai kuwa
eneo hilo ni muhimu kwao kwa ajili ya kuendeshea biashara.
Wakiwa na silaha mbalimbali, ikiwemo za moto, walifanikiwa
kuwatawanya wafanyabiashara hao kwa kutumia mabomu ya machozi.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa operasheni hiyo ilianza tangu wiki
iliyopita, kutokana na ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama, pamoja
na familia yake.
Operesheni ya kuwaondoa wafanyabiashara hao ilianza jana asubuhi
na ilikwenda vizuri, baadaye baadhi ya askari walipungua na kubaki
wachache, hapo ndipo wafanyabiashara walipopata mwanya wa kurudi
barabarani na kufunga barabara kwa kuweka mawe ili magari yasipite.
“Kosa lilikuwa ni kupunguza askari, hapo ndipo wafanyabiashara
tulijikusanya na kuweka mawe ili askari wasipite kuja kutuzuia wala
magari yasipite,” alisema askari aliyeshudia.
Mtu mwingine aliyejitambulisha kwa jina
Juma Mohamed, alisema wanashangaa askari kuendelea na operasheni hiyo
kwa kuwa kama ni ujio wa Obama ulishapita, hivyo waruhusiwe kurudi
katika maeneo hayo.
Magari ya Makamanda wa Polisi (OCD) wa
vituo mbalimbali, ikiwemo Kimara na Kinondoni, yakiwa na
Makamanda wao, yalikuja kuongeza nguvu, huku gari jingine la polisi
likiwasomba waliokamatwa katika oparesheni hiyo.
Aidha, maeneo
ya kuanzia Darajani mpaka soko la Manzese kulikuwa kumewekwa mawe
barabarani, huku barabara inayojengwa ikiwa imevunjwa katika baadhi ya
maeneo kutokana na vurugu hizo.
Maeneo hayo yote palikuwa
kimya, tofauti na siku zote ambapo kunakuwa na biashara mbalimbali
zikiendelea, huku polisi wakiwaaamuru watu wanaopita kutembea kwa mwendo
wa haraka pamoja na kutosogelea eneo la tukio.
Pia maduka yote
katika maeneo hayo yalikuwa yamefungwa na baada ya muda wa mapambano
hali ilianza kutulia kuanzia saa 9:00 alasiri.
Operasheni hiyo
inaelezwa kulenga kuwaondoa wafanyabiashara wadogowadogo ili kuweza
kupisha ukamilishaji wa ujenzi wa Barabara ya Morogoro, inayojengwa kwa
ajili ya mabasi yaendayo kasi (DART).
0 comments:
Post a Comment