Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (Nida), imeanza zoezi la kuchukua alama za vidole
vyote kumi, kupiga picha na kuweka saini ya kielektroniki kwa wakazi wa
Wilaya ya Temeke tayari kwa kutoa vitambulisho hivyo.
Kaimu Mkuu wa Mawasiliano na Machapisho, Thomas
William aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, kutokana na wingi wa
watu katika Jiji la Dar es Salaam, zoezi hilo limegawanywa katika ngazi
ya wilaya hadi wilaya.
“Hili zoezi tumelianza juzi, tunachukua alama za
vidole kumi, kupiga picha na kuweka saini za kielektroniki kwa wakazi wa
Temeke, tumeanzia Kigamboni na kutokana na ukubwa wake tumeigawanya kwa
kanda saba,” alisema.
William alisema, kanda ya kwanza inahusisha
mitaa yote katika kata za Kimbiji, Pemba Mnazi, Kigamboni, Vijibweni,
Kibada, Mji Mwema, Somangila, Kisarawe 11, Tungi na mitaa ya Mtoni
Kijichi, Mgeni nani na Misheni iliyoko katika Kata ya Kijichi.
Alisema, ili kuboresha mwonekano mzuri wa picha
kwenye kitambulisho hicho, mwombaji anashauriwa kutokuvaa nguo nyeupe,
kijivu, bluu mpauko, pinki na kofia au kapelo wakati wa kupiga picha.
Aidha, William aliwataka waajiri wa mashirika
mbalimbali kuwaruhusu watumishi kushiriki katika zoezi hilo siku
watakayokuwa wamepangiwa ili kurahisisha zoezi hilo na kuepuka usumbufu
wa kurudia eneo.
“Tunawaomba waajiri katika mashirika mbalimbali
nchini wawaruhusu watumishi wao kufika katika eneo muhimu kwa kuzingatia
tarehe aliyopangiwa ili kufanikisha zoezi. Hata wale ambao walikuwa
hawajajaza fomu za kujiandikisha wanatakiwa kufika katika kata zao ikiwa
zoezi linafanyika katika halmashauri hiyo,” alisema William.
Alisema, zoezi hilo limetoa kipaumbele kwa makundi
maalumu ya walemavu na wazee wasiojiweza na kuwa walemavu wa mikono
watapigwa picha bila kuchukuliwa alama za vidole.
Katika Jiji
la Dar es Salaam, zoezi hilo limeanzia Wilaya ya Temeke, likifuatiwa na Ilala na kumalizikia Kinondoni
la Dar es Salaam, zoezi hilo limeanzia Wilaya ya Temeke, likifuatiwa na Ilala na kumalizikia Kinondoni
0 comments:
Post a Comment