Aliyekuwa kiongozi wa vugu vugu la vijana la chama
tawala nchini Afrika Kusini cha ANC, Julius Malema amezindua kundi la
kisiasa litakalojulikana kama Wapiganiaji wa Uhuru wa Kiuchumi au
Economic Freedom Fighters, EFF.
Malema, ambaye alitimuliwa kutoka kwa chama cha
ANC, mwaka wa 2012, amesema chama chake cha EFF kinataka zoezi la
kugawanya mashamba kuanzisha upya na pia kutaifishwa kwa migodi yote ya
madini.
''Tutagawana
ardhi sisi zote ukiwa mweusi au mweupe. Lakini ukikataa kugawanya
itamaanisha kuwa utalazimishwa kufanya hivyo'' Alisema Bwana Malema.
Ametaja dhamira kuu ya vugu vugu hilo kuwa kupamabana mfumo wa kipebari.
Akiwa amevalia kofia nyekundu iliyo na maandishi
''Amirijeshi Mkuu wa EFF'' Bwana Malema amewaambia waandishi wa habari
kuwa chama chake kimebuniwa ili kutetea maslahi ya raia wanaoteseka
katika maeneo ya mashinani.
Malema ambaye alikuwa mmoja wa washirika wa
karibu wa rais Zuma, kwa sasa ni mmoja wa wakosoaji wakubwa na aliongoza
mikakati ya kumuondoa kama kiongozi wa chama cha ANC wakati wa mkutano
wa baraza kuu la chama hicho mwaka wa 2012.
Malema ameshutumu rais Zuma kwa kutoimarisha juhudi za kuwasaidia raia weusi wa nchi hiyo ambao ni masikini na waliompigia kura.
Hata hivyo haijabainika ikiwa atawania kiti
chochote katika uchaguzi mkuu utakaoandaliwa mwaka ujao, akisema kuwa
uamuzi huo utatolewa baada ya mkutano wa baraza kuu la chama hicho cha
EFF utakaofanyika mwisho wa mwezi huu.
Wachanganuzi wa kisiasa wanasema idadi kubwa ya
raia wa Afrika Kusini, wamepoteza imani na chama cha ANC, ambacho
kimekuwa madarakani tangu mwaka wa 1994.
Rais wanasema maafisa wengi wa chama hicho ni wafisadi na hawana nia ya kuimarisha hali ya maisha
0 comments:
Post a Comment