Pages

 

Friday, June 22, 2012

MGOMO TENA!....MGOMO MKUBWA WA MADAKTARI KUANZA KESHO NCHI NZIMA

0 comments
Wauguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wakiwa nje ya sehemu zao za kazi wakati wa mgomo uliopita
Madaktari wa Tanzania wametangaza rasmi kuanza kwa mgomo usio na kikomo kuanzia kesho, na kudai kuwa Serikali imekataa kutekeleza madai yao yote yaliyowasilishwa katika kamati ya majadiliano iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Mwenyekiti wa Jumuia ya Madaktari Tanzania,Dk Stephen Ulimbo
 Pinda jana aliliambia Bunge  wakati akijibu Maswali ya Papo kwa Papo, kuwa mgomo huo ni batili na haukubaliki, na saa chache baada ya onyo hilo lililorushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni na redio kutoka Dodoma, madaktari hao wakiwa jijini Dares Salaam walitangaza mgomo huo wenye lengo la kushinikiza Serikali kutekeleza madai yao.

Mgomo huo ulitangazwa kwa waandishi wa habari na Dk Stephen Ulimboka, muda mfupi baada ya kukamilika kwa mkutano wa ndani wa madaktari, uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la Utamaduni la Watu wa Urusi.

Dk Ulimboka alisema mgomo huo usio na kikomo utawahusu madaktari wa kada zote nchini, na unatarajiwa kuanza kesho, baada ya wiki mbili walizotoa kwa Serikali kumalizika bila ya makubaliano yoyote.

“Madaktari kwa ujumla wao wamekubaliana kuwa watarejea katika mgomo usio na kikomo, hii ni kutokana na kugundua kuwa hakuna dhamira ya dhati ya Serikali, kumaliza mgogoro kati yetu na Serikali, uliodumu kwa muda mrefu sasa,” alisema Dk Ulimboka na kuongeza,

“Serikali imetupilia mbali madai yote yaliyofikishwa katika meza ya majadiliano baina ya wawakilishi wa Serikali na madaktari na taarifa iliyotolewa bungeni na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi na pia majibu ya Waziri Mkuu leo (jana), yamepotosha kila kilichomo katika taarifa tuliyonayo sisi.”

Alifafanua kwamba Serikali imetupilia mbali madai yote ambayo kabla ya kukubali kurudi katika meza ya majadiliano yalionekana kuelekea kupata mwafaka.

Dk Ulimboka alisema kuwa kauli iliyotolewa na Pinda bungeni, kwamba walikubaliana, si ya kweli na hata posho zilizotajwa kwenye taarifa za kamati hiyo ni za dharura kabla ya kuanza kwa vikao vya majadiliano.

Alisema msimamo wao ni kuanzisha mgomo usio na kikomo na hakuna njia ya mkato ya kuuzuia, njia pekee ni Serikali kurudi katika meza ya majadiliano.

Kuhusu ushauri uliotolewa na Pinda kuwataka waende mahakamani, Dk Ulimboka alisema jumuiya yao haiko tayari kwenda na kwamba itaendelea na utaratibu wake wa kushinikiza madai hayo kwa njia ya mgomo.

“Sisi hatuendi mahakamani na hakuna njia yoyote ya kuuzima mgomo zaidi ya kurudi kwenye meza ya majadiliano yenye lengo la kufikia mwafaka wa yale tunayotaka kukubaliana," alisisitiza.

Alisema katika madai yao ya msingi waliyotoa serikalini, hadi sasa limetekelezwa moja tu, huku wakishangazwa na Serikali kuongeza posho ya uchunguzi wa maiti kutoka Sh10,000 za awali hadi Sh100,000 kwa madai kuwa posho hiyo haikuwa miongoni mwa madai yao.

“Sisi katika madai yetu hatukuliweka dai hili la posho ya uchunguzi wa maiti, kwa sababu hilo siyo dai letu la msingi. Kazi ya uchunguzi wa maiti siyo ya kila wakati, hufanywa tu pale watu wanapokuwa na mashaka na kifo cha mtu husika, lakini pia haifanywi na madaktari wote,” alisema Dk Ulimboka.

Naye Katibu wa Jumuiya hiyo, Dk Edwin Chitega alitaja madai yaliyowasilishwa katika kamati hiyo kuwa ni hali bora ya mazingira ya utoaji afya nchini, ongezeko la mishahara, posho za kufanya kazi katika mazingira magumu, posho za kufanya kazi katika mazingira hatarishi na posho za kuitwa kazini.
Hali ilinyokuwa katika mahospitali wakati wa mgomo uliopita

Akizungumzia dai la hali bora ya mazingira ya kazi, alisema hadi sasa hakuna kilichotekelezwa huku hali ya utoaji huduma kwa wagonjwa ikizidi kuwa mbaya.

“Tunaweza kusema tangu tukubali kuingia kwenye meza ya majadiliano hali imezidi kuwa mbaya. Katika hospitali kubwa kama Muhimbili inakosa vitendea kazi, dawa, wagonjwa kulazwa chini huku rufaa za wagonjwa kwenda nje ikiongezeka,” alisema Dk Chitega na kuongeza:

“Tunachotaka sisi ni huduma za afya ziboreshwe ili kuwezesha wananchi kupata huduma bora za afya na kupunguza rufaa za kwenda nje kutibiwa.”

Dk Chitega alitoa mfano wa gharama zilizotumika kwa mwaka wa fedha wa 2010/11, kuwa ni Sh7 bilioni, ilhali fedha zilizotumika kwa kipindi cha mwaka huu kwa ajili ya uendeshaji hospitali kubwa sita za hapa nchini kuwa Sh5 bilioni.

“Tulipendekeza pia mchakato wa rufaa uboreshwe kwa kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda nje kwa kuboresha huduma za ndani, Serikali ilianzisha Taasisi ya Mifupa (MOI), ikapeleka madaktari kwenda kusoma India, wamekuja kufanya kazi wamekosa vifaa wameondoka. Sisi lengo letu ni kuona fedha za nchi zinatumika kuwasaidia Watanzania,” alisema Chitega.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Dk Godbles Charles alisema taarifa zilizotolewa bungeni na Pinda na Dk Mwinyi zimepotoshwa na zina lengo la kuwarejesha kwenye mgomo.


DODOMA WAUNGA MKONO MGOMO
Jumuiya ya Madaktari na Wahudumu wa Afya mkoani Dodoma imetangaza mgogoro na serikali na kwamba wako tayari kuungana na wenzao kugoma kesho.
Mwenyekiti wa Jumuiya wa madaktari mkoani Dodoma, Dk. Kassian Mkuwa, alitoa msimamo huo jana katika kikao cha madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Dk. Mkuwa alisema hatua hiyo ni kuunga mkono maamuzi ya kikao cha madaktari na wahudumu wa afya kilichofanyika mwanzoni mwa mwezi huu kilichoukataa ufafanuzi uliotolewa na serikali juu ya madai yao ya msingi.
Alisema ufafanuzi huo wa serikali hauna nia ya dhati ya kuleta suluhisho la kudumu katika sekta ya afya.
Aliongeza kuwa wanaitaka serikali iache mara moja jitihada zake za kuwagawa wahudumu wa sekta ya afya kwani kwa kuwa kufanya hivyo kutazorotesha ufanisi wa utoaji wa huduma za afya nchini.
Hata hivyo, aliitaka serikali kuwalipa mara moja watumishi wa afya posho mpya za kuitwa kazini.
Kwa upande wake Katibu wa Jumuiya hiyo, Gustavos Deusdedith, alisema: “Tatizo ni kuwa serikali imekuwa ikitufanya sisi kama watoto, kwa maana hiyo imeshishindwa kutekeleza makubaliano kama walivyotuahidi katika madai yetu.”
Walichofanya serikali katika madai yetu ni kuongeza posho ya madaktari wanaofanya uchunguzi wa maiti kutoka Sh. 10,000 hadi Sh.100,000 wakati madaktari wenyewe hawazidi 10, sijui ndiyo njia ya kutatua madai yetu?” alihoji.
Alisema ukimya huo wa serikali utawafanya kuungana na madaktari wengine kwenye mgomo wa nchi nzima kuanzia kesho kutokana na kutoridhishwa na majibu ya serikali kwenye madai mbalimbali.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Dk. Emmanuel Mpuya, alisema hana taarifa za madaktari hao kugoma, bali anachofahamu kwa sasa ni kuwa wako katika majadiliano na serikali.
Wananchi wakitoa maoni yao wakati wa mgomo uliopita ammbao ulidumu kwa muda wa wiki 3
Dk. Mpuya alisema haungi mkono mgomo huo kwa kuwa unaweza kuwaumiza wananchi wasio na uwezo.
Madaktari wa Hospitali za Rufani za Bugando ya mkoani Mwanza na KCMC wamekwisha kutoa taarifa ya kuunga mkono mgomo huo.
 Jana bungeni Mjini Dodoma,Waziri Mkuu Mizengo Pinda alitoa taarifa  kwamba suala hilo liko Mahakama ya Kazi na kuonya kwamba mgomo huo ni batili, wakati akijibu swali la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.

Mbowe alitaka kujua hatua zilizofikiwa na Serikali katika kutatua mgogoro wa madaktari na walimu nchini, na sababu za kutotekelezwa makubaliano yaliyofikiwa katika majadiliano.

Akijibu swali hilo, Pinda alisema Serikali iliunda tume kushughulikia mgogoro wa madaktari ambapo kulikuwa na madai 10 yaliyojadiliwa na kati ya hayo, madai matano yalifikiwa mwafaka na madai mengine matano bado yanaleta mvutano.

“Ni kweli tumekuwa na mgogoro na madaktari lakini tumekuwa tukizungumza nao kwa kipindi chote cha tatizo hili, ili kupata mwafaka na kwa kama mwezi mmoja tume iliyoundwa ilimaliza kazi na kuwasilisha taarifa serikalini kwa ajili ya kufikia maamuzi,” alisema Pinda.
 
Pia alisema Dk Mwinyi alijitahidi kuonana na madaktari lakini haikuwezekana, ndipo akamshauri awaandikie barua ambayo madaktari walimjibu kuwa, hawaoni haja ya kuendelea na mazungumzo, kwani wamekuwa wakifanya kwa karibu miezi mitatu bila mafanikio.

Waziri mkuu alisema, baada ya Serikali kufikia hatua hiyo, ikaona ni vyema sasa irudi kwenye Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) kwa kuwa hawakuafikiana.

Alisema kwenda CMA si mara ya kwanza, kwani awali walikwenda lakini Serikali ikashauri ni kwa nini wasijadiliane nje na kufikia mwafaka, na baadaye kurudi CMA ili kuandikisha makubaliano waliyofikia.

“Hivyo tumerudi tena CMA kutoa taarifa na sasa suala hili limepelekwa mahakamani, lakini kama Jumamosi wakianza mgomo ni kinyume cha sheria… mimi nina wasihi sana, bado ipo nafasi ya kufikia mwafaka,” alisema Pinda.

Alisema mambo matano ambayo wamefikia mwafaka ni kuongeza malipo ya uchunguzi wa mwili wa marehemu kwa madakari ambapo wasaidizi sasa watalipwa Sh50,000 na madaktari Sh100,000.

Pia alisema Serikali ilikubali kuwaondoa mawaziri na watendaji wengine wa wizara hiyo, imeongeza malipo ya kuitwa kwa dharura na mengine kadhaa.

Waziri Mkuu alisema mambo ambayo hawajafikia mwafaka ni pamoja na ongezeko la mishahara ya madaktari, posho ya usafiri na nyumba na  posho za kufanya kazi katika mazingira magumu.

Kuhusu walimu, Pinda alisema hatua iliyofikiwa hivi sasa ni nzuri kwani tayari chombo cha majadiliano ambacho kilikuwa bado, sasa kimeundwa.

Alisema tayari Katibu Mkuu, Utumishi, amempatia taarifa za kukamilika kwa chombo hicho ambacho sasa kitawezesha kufikiwa makubaliano ya msingi na hivyo kutatua matatizo ya walimu.

Waziri Mkuu, alitoa angalizo kutokana na ujumbe wa simu unaosambazwa, ambao hata hivyo hakuufafanua, na kuomba kusiharakishwe kufikia huko kwani baada ya muda mfupi mwafaka wa madai ya walimu utapatikana.

Ujumbe huo ambao umesambazwa katika mitandao ya kijamii, unasomeka: “Hebu tizama tofauti hii ya kutisha ya viwango vya mishahara kwa watumishi wa umma wa TZ (Tanzania); (Ajira mpya cheti) mwalimu Sh244,400, Afya Sh472,000, Kilimo/Mifugo Sh959,400, Sheria Sh630,000.
Diploma: Mwalimu Sh325,700,  Afya Sh682,000, Kilimo/Mifugo Sh1,133,600, Sheria Sh871,500.

“Degree (shahada) Mwalimu Sh469,200, Afya Sh802,200, Kilimo/Mifugo Sh1,354,000,  Sheria Sh1,166,000. Je upo tayari kuvumilia kunyanyaswa hivyo katika utumishi wa umma wa taifa moja lenye soko la bidhaa lililo na mfumuko wa bei wa kutisha? Ungana na CWT kudai nyongeza ya mishahara 100%, Teaching allowance (posho ya kufundisha), hardship allowance (posho ya mazingira magumu). Wape sms hii walimu 20 tu! Mshikamano daima.”
Read more...

KWAMBA LULU NI MKUBWA MAWAKILI WA SERIKALI WAWASILISHA VIELELEZO MAHAKAMA KUU

0 comments
Lulu alipofikishwa mahakama kuu Juni 11 mwaka huu
MAWAKILI wa Serikali jana waliwasilisha vielelezo Mahakama kuu kupinga maelezo ya upande wa utetezi kuwa umri wa msanii wa kike wa filamu  Tanzania Elizabeth Michael ni mdogo

Habari zinasema kuwa vielelezo hivyo vya Jamhuri ni Mkanda wa video aina ya CD, yenye mahohjiano kati ya mshtakiwa huyo na mtangazaji mmoja nchini. Vingine ni maelezo ya mshtakiwa huyo aliyoyatoa polisi wakati alipohojiwa kuhusu tuhuma zinazomkabili, maombi ya hati ya kusafiria (Passport) na maombi ya leseni ya udereva.

 Awali vielelezo hivyo walitakiwa kuviwasilishwa juzi, lakini ilishindikana na badala yake vikawasilishwa jana na kesi itaendelea kusikilizwa Jumatatu ijayo, Juni 25.

Msanii Elizabeth Michael ambae hujulikana zaidi kwa jina la Lulu anakabiliwa na kesi ya mauaji katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akituhumiwa kumuua msanii mwenzake, Marehemu Steven Kanumba aliyefariki dunia nyumbani kwake Sinza, April 7, 2012.

Hata hivyo katika hatua za awali za kesi hiyo, umri wake ulizua utata baada ya mawakili wanaomtetea Lulu kudai kuwa bado ni mtoto kwa kuwa ana umri wa miaka 17 na si 18 kama hati ya mashtaka inavyoonesha.

Hivyo mawakili hao walilazimika kuwasilisha maombi mahakamani kuiomba mahakama iruhusu ufanyike uchunguzi wa umri sahihi wa mshtakiwa huyo na ikiridhika kuwa ni mtoto basi kesi yake iendeshwe kwa misingi ya kesi za watoto kisheria ili kulinda maslahi yake.

 Juni 11, 2012 Mahakama Kuu ilikubali  kufanya uchunguzi huo yenyewe kwa lengo la kubaini usahihi wa umri wa mshtakiwa huyo na ikaziagiza na kuzipangia tarehe pande zote katika kesi hiyo kuwasilisha mahakamani hapo vielelezo watakavyovitumia katika hoja zao.

 Jopo la mawakili wanaomtetea Lulu likiongozwa na Kennedy Fungamtama Juni 13 waliwasilisha mahakamani hati za viapo vya wazazi wake na vielelezo vingine kikiwemo cheti cha kuzaliwa na cha ubatizo vinavyoonesha kuwa bado ni mtoto.

 Lakini taarifa zilizopatikana mahakamani hapo zinaeleza kuwa vielelezo vilivyowasilishwa na Jamhuri vinaonesha kuwa mshtakiwa huyo ni mtu mzima kwa kuwa kwa mujibu wa vielezo hivyo ana umri zaidi ya miaka 18.

Viapo vya wazazi wa mshtakiwa huyo vilivyowasilishwa mahakamani hapo na Makamu wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Peter Kibatala ambaye ni mmoja wa mawakili wanaomtetea Lulu vinaeleza kuwa mshtakiwa huyo ana umri wa miaka 17.

Viapo hivyo ni kiapo cha mama yake Lulu Lucresia Augustin Kalugila, mkazi wa  Dar eS Salaam na kiapo cha baba mzazi Michael Kimemeta, mkazi wa Moshi.

Viapo  vyote vinaeleza kuwa mshtakiwa huyo alizaliwa April 16, 1995  katika kituo cha Afya Muhimbili na kupewa cheti cha kuzaliwa namba B.0318479 cha Julai 23, 2004.
 
Pia viapo hivyo vinaeleza kuwa baada ya kuzaliwa mshtakiwa,  mama yake alimpa jina la Diana Michael Kimemeta, lakini alimpeleka mtoto huyo Moshi mkoani Kilimanjaro kwa ndugu zake, walimpa jina la Elizabeth, jina la bibi yake Elizabeth Shikana.

Viapo hivyo vinaendelea kueleza kuwa baada ya majadiliano wote, yeye mama, baba na ndugu wengine walikubaliana kuwa wamuite Diana Elizabeth Michael Kimemeta .

“ Elizabeth Michael Kimemeta alibatizwa katika Kanisa la Katoliki  Chang’ombe Septemba 28, 1997 na alichukua majina ya ubatizo Diana Elizabeth Michael Kimemeta;” inasomeka sehemu nyingine ya kiapo hicho cha mama wa mshtakiwa.

Utata wa umri wa mshtakiwa huyo uliibuka Mei 7, 2012 katika  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya wakili wake Fungamtama kudai kuwa ana miaka 17 na hivyo kuomba kesi yake isikilizwe katika mahakama ya watoto.

Hata hivyo Mahakama ya Kisutu iliyakataa maombi hayo ikisema kuwa haina mamlaka ya kuyashughulikia na kushauri maombi hayo yawasilishwe Mahamaka Kuu.

Ndipo Mei 15 wakili Kibatala aliwasilisha maombi hayo mahakama kuu wakiomba mahakama hiyo iamuru kwamba Mahakama ya Kisutu ina uwezo wa kisheria kushughulikia maombi hayo.
Katika maombi hayo namba 46 ya mwaka 2012,  pia mawakili hao waliomba Mahakama Kuu kama itaridhika kuwa mahakama ya Kisutu haina uwezo wa kufanya wala kuagiza uchunguzi huo ufanyike, basi Mahakama Kuu yenyewe ama iagize au ifanye uchunguzi huo.

Sambamba na hayo pia waliomba Mahakama Kuu iamuru mwenendo wa kesi ya msingi katika Mahakama ya Kisutu usimamishwe hadi suala la umri litakapopatiwa ufumbuzi.

Katika uamuzi wake Jaji Dk. Fauz Twaib alisema kuwa Mahakama ya Kisutu ina mamlaka ya kushughulikia maombi hayo na kwamba ilikosea kukataa kuyashughulikia.

Pia Jaji Dk. Twaib  alikubaliana na hoja za pingamizi la awali la wajibu Maombi(Jamhuri) kupitia kwa Wakili wa Serikali Shadrack Kimaro akisaidiana na Wakili Elizabeth Kaganda, walizozitoa wakati wa usikilizwaji wa maombi hayo, Mei 28,2012.

 Wakili Kimaro alidai kuwa maombi hayo yamewasilishwa mahakamani hapo kinyume cha sheria na kwamba hata vifungu vilivyotumika katika madai hayo haviipi Mahakama Kuu uwezo wa kuyashughulikia.
 
 Hata hivyo licha ya kukubali kuwa maombi hayo yaliwasilishwa mahamakani isivyo sahihi, lakini Jaji Dk. Twaib alisema bado Mahakama hiyo ina mamlaka ya kuyashughulikia.

 Chini ya kifungu cha 44 cha Sheria ya Mahakama za Hakimu Mkazi, Jaji Dk. Twaib aliuagiza upande wa mwombaji(mawakili wanaomtetea mshtakiwa), kuwasilisha mahakamani hati hizo za viapo na vielelezo vya umri wa mshtakiwa huyo juzi Jumatano.



Read more...

Thursday, June 21, 2012

WOLPER AANGUSHA KILIO AKIJITETEA KUHUSU GARI `ALILONYANG`ANYWA`

0 comments
Hivi karibuni kulikuwa na uvumi kuwa nyota wa filamu za  Bongo, Jacqueline Wolper Masawe amenyang’anywa lile gari alilokuwa akitanua nalo hivi karibuni aina ya BMW X6, lenye namba za usajili T 574 BXF na kwamba, sasa nyota huyo anatembelea gari lake la zamani Toyota Noah.Taarifa zinazsema
chanzo cha kuenea kwa tetesi hizo kilianzia kwenye mitandao ya kijamii na blog  ambapo wadau mbalimbali waliandika kuwa Wolper alinyang’anywa gari hilo na mwanaume aliyemnunulia.Wengine  wakitaja hata jina la Frank ambaye ni mtoto wa mfanyabiashara maarufu jijini Dar kuwa ndiye mmiliki wa gari hilo kwa sasa.Kwa mujibu wa mwandishi wa tabloids za Global Publishers ambae alikutana na Wolper Jumatatu ya wiki hii ,Wolper mwenyewe alikiri kusikia taarifa hizo huku akikanusha kuwa si za kweli.


“Na mimi nimesikia lakini si kweli jamani. Hivi mtu anaweza kunyang’anywa nguo yake ya ndani au shati lake? Si itakuwa kichekesho, gari ni mali yangu na hakuna mwenye uwezo wa kuja kuninyang’anya kwani nalimiliki kihalali,” alinukuliwa Wolper akisema.
Wolper alisema amelifungia gari hilo nyumbani kwake, Mbezi Beach, Dar  Es Salaam kwa sababu "lina matatizo kidogo".
Ili kujiridhishana hatimaye kuifahamisha dunia ukweli Wolper aliombwa kuongozana na waandishi  kwenda Mbezi kuliona gari hilo kama lipo kweli auikbidi alifuate na kulifikisha ofisi za Global Publishers.
: “Nisikuongopee kuwa naweza kuja nalo hapo ofisini wakati tatizo lake nalifahamu mimi, nakuja kuwachukua twendeni nyumbani mkalione.” Ndio jibu alilolitoa Wolper baada ya kutakiwa kulileta gari kwa uthibitisho


Saa 2:16 usiku, Wolper aliongozana na waandishi hadi nyumbani kwake na walilikuta gari hilo likiwa ndani ya geti.
Anaonesha kadi ya umiliki

Huku akilionesha  gari hilo Wolper aliangusha kilio na kusema:
“Watu wananionea sana, wananichafua. Sijui lengo lao ni nini hasa? Kila kukicha nasingiziwa jambo, mara Jack kafanya hivi, mara vile.Mbaya zaidi, hata waigizaji wenzangu wapo wanaonichukia, au kwa kuwa nimepata maendeleo kidogo? Walitaka niporomoke kimaisha?”


Kuhakikisha kuwa Wolper hajanyang’anywa gari hilo, pia alionesha kadi yake ya umiliki.
SOURCE:GLOBAL PUBLISHERS

  ZINAZO HUSIANA NA HII:
 

Read more...

TAARIFA: KAGAWA KUFANYIWA VIPIMO OLD TRAFFORD KESHO

0 comments
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana,Shinji Kagawa anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya kesho Ijumaa pale Old Trafford ili dili lake la kujiunga na Manchester United kwa paundi milioni 17 liweze kukamilika.

Endapo Kagawa atathibitishwa kuwa fiti,Manchester United watakuwa na jukumu la kumtafutia kibali cha kufanya kazi nchini Uingereza,na baada ya hapo kila kitu kitakuwa kimekamilika.

 Lakini, ili kibali kipatikane, Kagawa anatakiwa awe ameshaichezea Japan asilimia 75 ya mechi za kimataifa kwa mwaka uliopita,lakini Kagawa hana sifa hiyo,hivyo basi sifa pekee ambayo Manchester United wanaweza kuitumia kupata kibali ni ile ya kipaji cha ziada,ambayo hata Arsenal waliitumia kwa Miyachi,mchezaji mwingine kutoka Japan.

Shinji Kagawa amaepata mafanikio katika misimu miwili iliyocheza kwenye ligi kuu ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga.Ameichezea Borussia Dortmund mechi 71 na kufunga magoli 29,amechangia magoli 15,amebeba kombe la ligi kuu (Bundesliga) mara mbili na kombe la Ujerumani mara moja. 

Read more...

Wednesday, June 20, 2012

SIKILIZA MANENO YAILIYOMPONZA MNYIKA HADI AKATOLEWA NJE YA BUNGE

0 comments

Mh John Mnyika akisindkizwa na askari wawili wa bunge jana baada ya kutolewa nje kwa utovu wa nidhamu
Read more...

Tuesday, June 19, 2012

`MCHAWI` AHUKUMIWA KUCHINJWA SAUDI ARABIA

0 comments
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudi Arabia
Mtu mmoja amekatwa kichwa leo kwa kosa la kushiriki mambo ya uchawi nchini Saudi Arabia,mtandao wa Arab News limeandika likinukuu taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo.

Taarifa zingine za vyombo vya habari nchini humo zinasema kuwa,mtu huyo,Muree bin Ali Al-Asiri,pia amekiri kufanya zinaa na wanawake wawili.Amehukumiwa kwa kukatwa kichwa chake katika jimbo la Najran lililoko kusini mwa nchi hiyo.

Katika ripoti ya Shirika la Habari la Uingereza BBC linasema kuwa mwezi Disemba mwaka uliopita mwanamke mmoja alihukumiwa adhabu kama hiyo baada ya kukutwa na kosa la uchawi,na mwezi Septemba raia mmoja wa Sudan alihukumiwa kukatwa kichwa licha ya kupigiwa kelele na Taasisi ya Kimataifa ya Haki za Binadamu,Amnesty International,kutaka waachiwe.

Mhariri wa BBC mambo ya Uarabuni,Sebastian Usher amesema kuwa viongozi wa kidini wenye nguvu kubwa na msimamo mkali nchini humo wanaunga mkono adhabu hizo kutolewa kwa mtu yeyote anaekutwa na kosa la kufanya uganga ikiwamo kupiga ramli na kutibu kwa njia za kiimani

Kwa mujibu wa mtandao wa Arab News watu wengine wawili mtu na dada yake, rai wa Misri,walihukumiwa na mahakama moja mjini Madinah baada ya kupatikana na hatia ya kuteka nyara na kubaka
Mohammed bin Nafe na dada yake Jamalat bint Nafe walikutwa na kosa la kumteka nyara binti wa miaka 9 kutoka Msikiti wa Mtume Madinah, kumtesa na kumweka kifungoni ndani ya nyumba wanayoishi kwa miaka mitatu na miezi sita.Inasemekana Mohammed alikuwa akimbaka binti huyo kwa muda wote huon na walikuwa na mpango wa kumtorosha nje ya nchi

Kosa lingine walilokutwa nalo ni kuwatelekeza na kuwatesa watoto wao kuwapiga na kutojali afya zao,jambo ambalo lilipelekea watoto wawili wa Mohammed kupoteza maisha.

Hukumu nyingine ya kuchinjwa iliyotolewa leo nchini humo ni ya mtu mwingine aitwae Ali bin Mohammed Al-Qahtani ambae alipatikana na hatia ya kumpiga risasi Msaudia mwenzie na kumuua.

 
Read more...

NAPE, ZITTO WAFEDHEHESHWA NA MNYIKA.. MNYIKA ATOA MSIMAMO WAKE BAADA YA KUTOLEWA BUNGENI...

0 comments

Mheshimiwa John Mnyika
Mbunge wa Jimbo la Ubungo (Chadema), Mhe. John Mnyika ametolewa nje ya bunge mchana huu na Naibu Spika, Job Ndugai baada ya kukataa kufuta kauli yake kuwa Rais Kikwete ni dhaifu wakati alipotakiwa kufanya hivyo. Mnyika ametolewa nje ya bunge wakati wabunge wakichangia mjadala wa bajeti ya serikali mwaka wa fedha 2012/13 iliyowasilishwa bungeni hivi karibuni. Mnyika atarudi bungeni kesho saa tatu asubuhi.

Muda mfupi baadae Twitter ikalipuka na baadhi ya meseji ni hizi:




Baadae Mbunge Mnyikaaliandika kwenye akaunti yake ya Facebook kuonesha msimamo wake kuhusu kauli aliyoitoa:

Msimamo wangu wa sasa juu ya Kauli yangu!

Nitatoa tamko la kina baadae kuhusu kilichotokea lakini kwa ufupi ubovu wa bajeti hii ni matokeo ya udhaifu wa Rais Kikwete, yeye ndiye aliyesaini Mpango wa Taifa wa miaka mitano kama Kiongozi Mkuu wa Nchi tena kwa wino mwekundu kama Amiri Jeshi Mkuu. Na yeye ndiye Mwenyekiti wa baraza la mawaziri, bajeti hii iliyoacha kuzingatia mpango wa Taifa imepita k
wenye baraza alilloliongoza, pia kushindwa kutekelezwa kwa bajeti iliyopita ni matokeo pia ya udhaifu wa taasisi ya Urais.

Pia kwa mujibu wa Katiba Rais ndiye ambaye anapeleka bajeti bungeni, Waziri mwenye dhamana anapeleka tu kwa niaba. Rais amepewa mamlaka makubwa juu ya bajeti ibara ya 99 imeweka mipaka kuhusu mambo ambayo bunge lina mamlaka nayo huku ibara ya 90 inasema bunge likikataa bajeti rais ana mamlaka ya kuvunja bunge. Hivyo Rais Kikwete anapaswa kuagiza Waziri wa Fedha bajeti iondolewe irudi kwenye baraza la mawaziri ikafanyiwe marekebish
o.
Read more...

INGIA HUMU UONE KOMPYUTA MPYA YA KIGANJANI ILIYOZINDULIWA LEO NA MICROSOFT

0 comments



Kampuni ya Microsoft leo imezindua kompyuta yake ndogo ya kiganjani katika jitahada za kuipiku iPad inayotengenezwa na kampuni ya Apple.Kompyuta hiyo wanayoiita Surface inatumika kwa kugusa kwenye kioo cha kompyuta hiyo kama ilivyo kwa iPad


Kompyuta ya Surface ina muundo ambao una kifuniko kinachokunjuka na kuunda keyboard na kioo chake ni cha widescreen.Kio hicho cha Touchscreen kinaendeshwa na mfumo mpya wa kompyuta Windows 8 ambao Microsoft wanatarajiwa kutoa hivi karibuni,na pia mtumiaji wakompyuta hiyo anaweza kutumia processor yoyote kati ya Intel au ARM
Microsoft hawajataja bei ya kompyuta hiyo wala tarehe ya kuingia sokoni
Read more...

Friday, June 15, 2012

MEET AN 84 YEAR-OLD KENYAN,THE OLDEST PRIMARY SCHOOL STUDENT IN THE WORLD

1 comments




















STEPHEN Kimani Ng'ang'a Maruge ( 1920 - August 14, 2009) holds the Guinness World Record for being the oldest person to start primary school—he enrolled in the first grade on January 12th 2004, aged 84. Although he had no papers to prove his age, Maruge believed he was born in 1920.

Maruge attended Kapkenduiywo Primary School in Eldoret, Kenya; citing that the government's announcement of universal and free elementary education in 2003 prompted him to enroll.

In 2005 Maruge, who was a model student, was elected head boy of his school.And in September 2005, Maruge boarded a plane for the first time in his life, and headed to New York City to address the United Nations Millennium Development Summit on the importance of free primary education.


Maruge's property was stolen during the 2007-2008 post-election violence, and he contemplated quitting school.During early 2008 he lived in a refugee camp, where he was reportedly a minor celebrity, four kilometers from his school, but still attended classes every day.In June 2008, he relocated to the capital Nairobi.

In June 2008, Maruge was forced to withdraw from school and relocate to a retirement home for senior citizens.However, soon after, on June 10, 2008, Maruge enrolled once again into grade 6 at the Marura primary school, located in the Kariobangi area of Nairobi.

 A feature film about Kimani Maruge, starring Oliver Litondo and Naomie Harris titled The First Grader, was released on May 13, 2011. The British-produced film was shot on location in the Rift Valley in Kenya, despite earlier reports that it would be filmed in South Africa.

Director Justin Chadwick said: "We could have shot it in South Africa, but Kenya has this unbelievable, inexplicable energy - inherent in the children, and the people we were making the film about"
.
On Sunday May 24, 2009, Maruge was baptised at Holy Trinity Catholic Church in Kariobangi and took a Christian name, Stephen.He was then using a wheelchair.

Maruge was a widower, and a great-grandfather (two of his 30 grandchildren attend the same school). He was a combatant in the Mau Mau Uprising against the British colonizers in the 1950s.
 He died on August 14, 2009 of stomach cancer, at the Cheshire Home for the Aged in Nairobi and was buried at his farm in Subukia.

NOW WATCH THIS VIDEO ABOUT STEPHEN KIMANI NG`ANG`A MARUGE



Read more...
 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797