Pages

 

Monday, July 22, 2013

MJANE WA MWANAJESHII ALIEUAWA DARFUR `ATOLEWA NDUKI`

0 comments
Hata kabla ya maziko askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), waliouawa Darfur, Sudan hayajafanyika, mchumba wa mmoja wa wapiganaji hao, Amina Juma ameonja chungu nyingine baada ya kutimuliwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi na marehemu mwenza wake.
Amina ambaye inadaiwa kuwa alikuwa akiishi na Fortunatus Msofe aliyekuwa askari katika Kambi ya Msangani, 36KJ Pwani alisema jana: “Kumekuwa na mzozo wa hali ya juu na ndiyo maana tumeshindwa hata kufika Uwanja wa Ndege kuupokea mwili na hata kesho (leo) sidhani kama nitakwenda... kuna mtafaruku mkubwa wa kifamilia.”
Amina Juma
Baada ya kutimuliwa, Amina ambaye hawakuwahi kupata mtoto na marehemu Msofe, alilazimika kuondoka kwenye nyumba hiyo na kwenda Mlandizi kwa wazazi wake.
“Nimeishi na Msofe kwa miaka mitatu, akiwa kambini mimi niko hapa na wakati mwingine alikuwa analala huku... lakini leo wamenitimua,” alisema huku akilia.
Habari zilizothibitishwa na baadhi ya waombolezaji waliokuwa nyumbani kwa marehemu Visiga, Kibaha zinasema baadhi ya wanandugu walimkana Amina siku chache baada ya kutangazwa vifo hivyo.
Ilidaiwa kwamba Amina alitimuliwa katika nyumba hiyo Ijumaa iliyopita, saa saba mchana baada ya ndugu watatu wa marehemu kufika hapo wakitokea Tanga.
Walipofika inadaiwa kuwa walitangaza kusitishwa msiba huo katika nyumba hiyo na kutangaza kutomtambua mke huyo.
Watu hao waliwaeleza waombolezaji kuwa walitumwa na baba mzazi wa marehemu, Willbad Msofe kutoka Kange, Tanga kufika Kibaha kusitisha msiba uliokuwa ukiendelea nyumbani kwa mtoto wake huyo.
Inadaiwa pia kuwa katika msafara huo,  alikuwapo mdogo wa marehemu ambaye aliwahi kuishi kwa miaka miwili na Amina hapo Visiga.
Ilidaiwa kuwa walipofika nyumbani hapo walionana na mfiwa, Amina na wazazi wake ambao pamoja na majirani na watu wengine wengi, walikuwa wakimfariji binti yao huyo.
Mmoja wa waombolezaji alisema baada ya salamu wanandugu hao walianza kuulizia mali za marehemu na walikuwa wakimuuliza Amina ambaye aliwaleza kila kitu kilipo na baada ya hapo ndipo walipomweleza kuwa wametumwa na baba wa marehemu kuwa watu hawatakiwi kuomboleza kwenye eneo hilo kwani msiba upo Tanga tu ambako ndiko iliko familia yake.
Alipoulizwa baba wa marehemu, Mzee Msofe alisema: “Mimi ndiye niliyeagiza nyumba ifungwe na ukweli ninamfahamu Amina, lakini simtambui kama mkewe kwa kuwa hawajafunga ndoa... Hata wewe si unayafahamu haya? Uchumba si ndoa na ukifunga ndoa ndipo unatambulika rasmi,” alisema

Akiwa kwa wazazi wake Mlandizi jana, Amina alisema:
“Namwachia Mungu maana hayo yote nashangaa yanatokea wakati huu mume wangu ‘Fortu’ amekufa, mbona kipindi chote cha miaka mitatu iliyopita familia ya Tanga dada zake na mdogo wake tuliishi nao vizuri kwangu nilipokuwa na marehemu? Nimeishi na ndugu wote lakini hawakuwahi kuhoji, hata nilipokwenda na mume wangu Kange baba na mama Msofe nilikaa nao zaidi ya wiki na hawakunikana, ila nashangaa,” alisema na kulia kwa uchungu.
Akizungumzia kitendo hicho, baba yake Amina, Juma Juma alisema: “Nimeshangaa hizi taarifa. Tulikuwa tunajiandaa kupokea msiba wa mwanetu, lakini leo yanakuja mengine kwa kweli imetushangaza sana.”
“Nasubiri baada ya kumzika marehemu, nitazungumza nao... Kinachonishangaza ni kwamba walituandikia barua ya kumposa binti yangu na tukawajibu na gharama zilikuwa Sh1.2 milioni... Tutazungumza, ngoja hili lipite kwanza,” alisema mzee Juma.

WALIVYOISHI NA MAREHEMU
Akisimulia maisha yao, Amina alisema: “Tulianza kuishi Mbezi Luis mwaka 2010 katika nyumba ya kupanga na nikamshawishi tununue kiwanja na kwa kuwa mimi ni mwenyeji wa Kibaha, niliwatumia marafiki wa familia yangu Mlandizi wakatafutia eneo na mwaka 2011 tulipata na tukaanza ujenzi.
“Tukiwa Mbezi, tulianza kufyatua matofali kisha ujenzi ukaanza Visiga mwaka 2012 mwanzoni na  Septemba mwaka huo tulihamia kwenye nyumba yetu na hapo ndiyo ilikuwa makazi yetu hadi marehemu anaondoka kwenda Darfur.
“Wakati wote huo ‘Fortu’ alikuwa keshaniposa na hata barua zote za posa zipo na tulikuwa tukisubiri utaratibu wa kijeshi marehemu kukamilisha miaka sita ya kukaa kambini kisheria ndipo aruhusiwe kuoa.
“Fortu alikamilisha miaka hiyo mwaka 2012 mwishoni na wakati akijiandaa kwa kufunga ndoa ndipo ikatokea safari ya Darfur mwanzoni mwa mwaka huu na tukakubaliana tusitishe kwanza akirudi tukamilishe, lakini haikuwa.... Halafu wananifukuza wanasema hawanijui,” alieleza huku akiangua kilio.

CHANZO:GAZETI LA MWANANCHI
Read more...

Sunday, July 21, 2013

SHILOLE AFANYA MAHOJIANO NA `TAKE ONE` NYUMBANI KWA DIAMOND

1 comments
Mtangazaji wa Clouds Tv, Zamaradi Mketema, alikuwa nyumbani kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongoflava)Nasib Abdul (Diamond Platinumz) ambako msanii huyo alikuwa akifuturisha.Bi Mketema alipata wasaa wa kumhoji msanii mwingine katika tasnia hiyo ya muziki Zuwena Mohamed`Shilole`.Mahhojiano hayo yalikuwa mahsusi kwa kipindi cha TAKE ONE cha Clouds Tv kinachoendeshwa na Bi Mketema.Watu hao wawili walikuwa ni sehemu ya watu kadhaa walioalikwa kwa ajili ya kufuturu nyumbani kwa Diamond.
 Katika mahojiano hayo ambayo yanatarajiwa kurushwa hewani na Clouds Tv siku ya Jumanne hii saa 3.30 usiku,Shilole amelezea faida alizopata kama msanii katika safari yake nchini Marekani,na pia matarajio yake baada ya safari hiyo,ikiwamo ya kufanya kazi na msanii mmoja mkubwa wa nchi hiyo.
 

Read more...

NUSU YA WAZAZI WA KIUME NCHINI WANALEA WATOTO WA KUBAMBIKIWA

0 comments

Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali nchini imesema karibu nusu ya watu waliojitokeza kupima vinasaba (DNA) ili kubaini uhalali wa watoto wao, vipimo vimeonesha si wazazi halisi wa watoto waliopimwa.
 
Takwimu hizo ni kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2010, ikionesha kuwa, asilimia 48.32 ya wazazi 'wanalea' watoto wasio wa kwao wakati asilimia 51.68 ndio wazazi halali.
Hayo yameelezwa jana na Mkuu wa Kitengo cha Makosa ya Jinai, Vinasaba na Baiolojia wa ofisi hiyo, Gloria Machuve katika mkutano na wanahabari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dar es Salaam.
 
Ingawa hakutaja idadi kamili ya waliojitokeza kupima DNA, alisema idadi hutofautiana mwaka hadi mwaka. Ili kufanya vipimo vya DNA, wazazi hulazimika kulipia Sh 100,000.

Machuve alisema kazi ya DNA si kutambua watoto halali na wasio halali pekee, bali vipimo hivyo vina umuhimu mkubwa kwa jamii. 
 
Alitoa mfano kuwa, matumizi ya Teknolojia ya vinasaba vya binadamu yamewezesha kesi mbili za mauaji ya vikongwe na albino kutolewa hukumu katika mikoa ya Shinyanga, Kagera na Sumbawanga baada ya kufanyika kwa uchunguzi katika matukio manane.

Aidha, alisema katika majanga mbalimbali yaliyokumba nchi ikiwa pamoja na milipuko ya mabomu yaliyotokea Mbagala, Dar es Salaam mwaka 2010 walitambua mabaki ya askari sita ambao baadaye walichukuliwa na ndugu zao na kuzikwa.
 
Alitolea pia mfano wa tukio la moto katika Shule ya wasichana ya Idodi mkoani Iringa ambako licha ya kuungua vibaya, miili ya wanafunzi 12 ilitambuliwa hivyo makaburi yao kutambuliwa. Katika Jengo la ghorofa lililoporomoka mtaa wa Kisutu mwaka huu, marehemu 23 walitambulika. 

Aidha, katika ajali ya Ndege ya Comoro mwaka 2010 mabaki ya miili ya marehemu 25 ilitambuliwa huku katika masuala ya uhamiaji teknolojia hiyo ilitumika kudhihirisha hawana uhusiano na wananchi wa Tanzania.

Machuve alisema katika masuala ya ubakaji na mimba za utotoni  teknolojia hiyo imesaidia kuwa fikisha wahusika mahakamani pamoja na katika wizi wa kutumia silaha.
Read more...

WAENDA JELA KWA KUPOST NYAMA YA NGURUWE NA KEJELI KWENYE FACEBOOK WAKATI WA MFUNGO

0 comments
Alvin Tan na Vivian Lee wakiwa chini ya ulinzi
Wamiliki wa Blog moja inayojihusisha na masuala ya ngono Alvin Tan na Vivian Lee wamefunguliwa mashtaka na kuwekwa ndani bila ya dhamana nchini Malaysia baada ya kuweka picha inayowakosea waumini wa kiislam kwenye Facebook.Wanakabiliwa na adhabu ya kifungo cha miaka minane jela.

Alvin na Vivian kwenye picha iliyowaponza ambayo ina ujumbe unaotafsirika kama"Futari njema furahi na nyama ya nguruwe,harufu nzuri, tamu, inayotia hamu ya kula"
Picha iliyowaponza  ilikuwa ikiwaonesha wakila nyama ya nguruwe ikiwa na ujumbe wa kuwatakia waislam ramadhan njema.Mamlaka inayosimamia sheria nchini humo imelichukulia tuko hilo kuwa ni kosa kubwa,ikizingatiwa kuwa nyama ya nguruwe ni haram (hairuhusiwi) kwa waumini wa kiislam.Ingawa watu hao walijitetea kuwa walilenga katika kuonesha ucheshi wao,imechukuliwa kuwa inawavunjia heshima baadhi ya watu katika jamii na pia kuzingatia na kazi wanayojihusisha nayo wakosaji pia si nzuri ambapo wamekuwa wakiweka video za ngono kwenye ukurasa wao wa Youtube uitwao `Sexcussions with Alvin` na pia wanamiliki blog inayoegemea kwenye masuala ya ngono.

Picha za ngono ni marufuku kwenye nchi za Malaysia na Singapore,hivyo tukio hilo limesababisha Tan mwanafunzi wa sheria Chuo Kikuu cha Malaysia kunyang`nywa hati za masomo ya juu (Scholarship) ya nchi za ASEAN,baada ya malalamiko ya wananchi dhidi ya blog yao.

Tan na Lee wameshakana mashtaka yao na wamewekwa ndani bila dhamana hadi kesi yao itakapoanza kusikilizwa Agosti 23 mwaka huu.Baada ya tukio hilo waliomba radhi kwenye ukurasa wao wa Youtube kwa kusema:
 "Tunarekodi video hii ili kuwaomba radhi waumini wa kiislam kwa kuwa tumewakosea kwenye mwezi huu mtukufu wa Ramadhan"


Read more...

Wednesday, July 17, 2013

BREAKING NEWS:LUKUMAY WA KLABU MASAI AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI

0 comments
LUKUMAY  (kulia)enzi za uhai wake
Habari nilizozipata muda mchache uliopita ambazo zimethibitishwa na ndugu na jamaa wa karibu zinasema Benedict Charles Lukumay amefariki kwa ajali ya gari eneo la Mikumi mkoani Morogoro usiku huu.
 
Chanzo cha kifo chake kimeelezwa kuwa ni ajali ya gari iliyotokea eneo la Mikumi mkoani Morogoro majira ya saa mbili usiku. Meneja mkuu wa Meridian Hotel LTD Mzee Mponda amethibitisha juu ya kifo hicho, huku huku akisema kuwa ilitokana na ajali ya gari.

 "Wakiwa na mwenzake aliyefahamika kwa jina la Adrian na gari binafsi wakielekea mkoani Iringa gari aliyokuwamo marehemu iligonga nyuma ya roli lililokuwa limesimama njiani." alisema Mzee Mponda.

 Adrian ambaye ndiye aliyekuwa anaendesha gari alinusurika kwenye ajali hiyo.

 Benedict alikuwa ni mmoja kati ya Wakurugenzi watendaji wa kampuni ya Meridian Hotel LTD inayomiliki na kuendesha kumbi za burudani zikiwemo Masai Kinondoni, Masai Ilala na Masai Galapo Ilala.
Kifo chake kimeacha pengo kubwa si tu kwa familia bali hata wapenda burudani, akifahamika kimchango katika kusimamia na kuendeleza burudani na yakiwemo maonyesho mbalimbali ya wanamuziki wa bongo fleva na fani nyinginezo.

Mungu alaze Pema ROHO ya Marehemu Ben..
Read more...

PHOTOS:LADY JAY DEE`S MAKE-UP SESSION DURING THE VIDEO SHOOTING OF HER SINGLE HIT `YAHAYA`

0 comments

Read more...

MKONGWE GEORGE MASATU ALILIA KURUDI SIMBA

0 comments
Waliosimama kutoka kushoto.ni Rashid Msemakweli(Dokta)Abdallah Kibadeni,Often Martin,Razak Yusuf,George Lucas,Iddi Seleman,Damian Kimti,Abdul Mashine,George Masatu,Entienne Eshete,Mzee Abdulrahman Muchacho.

Waliochuchumaa kutoka kushoto ni.Kasongo Athuman,Selemani Pembe,Edward Chumila,Dua Said,Fikiri Magoso,Malota Soma na Mohamed Mwameja.
Hii ilikuwa ni mechi ya Simba na Yanga (Simba ilishinda 1-0 mfungaji Dua Said.)Nahodha wa Simba siku hii alikuwa ni Rashid Abdallah Magongo ambae hayupo  pichani, alikuwa na waamuzi pamoja na Nahodha wa Yanga Keneth Mkapa.

ALIYEKUWA  mchezaji wa Simba miaka kumi na tano iliyopita George Magere Masatu, amesema kuwa kwa sasa yuko tayari kurejea kwenye timu hiyo.
 

Masatu hivi sasa amerejea nchini akiwa tayari amestaafu soka lakini ana kadi ya uanachama wa timu hiyo yenye maskani yake Msimbazi jijini Dar es Salaam.

Masatu amesema kuwa yuko tayari kurejea kama kocha na siyo mchezaji tena kama ilivyokuwa awali Masatu alisema kuwa, ana uwezo na uzoefu kufundisha aliyoupatia katika shule ya soka ya Arsenal huko Indonesia alikokuwa akicheza soka la kulipwa kwa zaidi ya miaka mitano.
 

“Kweli nimerudi nyumbani kuendelea na maisha, lakini ukisema kuhusu Simba mimi ni mwanachama.Na kama wakisema nifanye nao kazi,niko tayari haina shida
 

“Nimekuwa kocha kwenye shule ya watoto ya Arsenal kule Indonesia kwa zaidi ya miaka mitatu. Ninajua kazi inavyofanyika na wakisema wanataka tufanye kazi, basi tutafanya hivyo,” alisema Masatu aliyekuwa beki kisiki wakati wa enzi zake.
 

Masatu alianza kufanya vizuri akiwa na Pamba ya Mwanza kabla ya kujiunga na Simba mwanzoni mwa miaka ya 1990.
Pamoja na kuwa na umbo dogo, Masatu alikuwa ndiye beki nyota na imara zaidi wa kati nchini na jina lake halijawahi kushuka chati pamoja na kuwa nje ya Tanzania kwa muda mrefu.

Read more...

BAN KI MOON ALAANI MAUAJI YA WANAJESHI WA TANZANIA DARFUR

0 comments


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UNO), Ban K-Moon(pichani), amesema amesikitishwa na kuhuzunishwa na mauaji ya askari saba wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), lililofanywa na waasi wa Sudan Julai 13, mwaka huu.
Askari hao wa JWTZ waliokuwa Darfur, Sudan ya Kusini kulinda amani kwa mujibu wa UNO, walishambuliwa na waasi hao karibu na kambi ya Manawashi eneo la Khor Abeche, mji wa Darfur Jimbo la Nyala ambapo pia askari wengine 17 walijeruhiwa baadhi yao vibaya.
Katika salamu zake hizo kupitia kwa Msemaji wake, Katibu Mkuu huyo wa Uno, ameelezea masikitiko yake kuhusiana na vifo hivyo na kutoa pole kwa familia za marehemu waliokuwa wakilinda amani, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Vikosi vya Umoja wa Afrika kwa Umoja wa Mataifa vya Kulinda Amani (Unamid).

Ban K-Moon amelaani shambulio hilo dhidi ya Unamid na kuelezea matumaini yake kwamba Serikali ya Sudan itachukua hatua zinazofaa kuhakikisha kwamba wahusika wanafikishwa mbele ya sheria.
Wakati huo huo, Taarifa iliyotolewa na Unamid juzi jioni ilisema wajumbe wa Baraza la Usalama wanalaani kwa nguvu zote mashumbulizi hayo dhidi ya askari wa vikosi vya Unamid.
"Wajumbe wa Baraza la Usalama wameelezea masikitiko yao na kutuma salamu za pole kwa familia za marehemu hao pamoja na kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Aidha, wameitaka Sudan kufanya upelelezi wa kina kuhusiana na tukio hilo na kuwafikisha wahalifu hao mbele ya mkono wa sheria.
Taarifa hiyo ya Unimad iliongeza kuwa shambulio lolote dhidi ya vikosi vya Unimad halikubaliki na kuonya kuwa lisitokee tena shambulio lingine la aina hiyo huku ikisisitiza pande zinazovutana Darfur kushirikiana kwa lengo la kufikia malengo yaliyokusudiwa.


Read more...

USHINDI WA ARSENAL WAFANYIWA PROPAGANDA ZA KISIASA INDONESIA

0 comments
Sege Gnaby wa Arsenal akikwepa daruga la mchezaji wa Indonesia, Roby
Mgombea urais katika uchaguzi wa Rais wa 2014 kupitia Chama cha Great Indonesia Movement Party (Gerindra) Jenerali mstahafu Prabowo Subianto ameutumia mchezo kati ya timu ya taifa ya nchi hiyo na Arsenal kuishambulia serikali iliyo madarakani katika hotuba ya mkutano wa Kampeni za uchaguzi wa Rais wa nchi hiyo wa mwaka 2014

Baada ya timu ya taifa ya Indonesia kupokea kipigo cha goili 7-0 kutoka Gunners mgombea Prabowo aliilaumu serikali kwa kutoisimamia vizuri timu hiyo  na kuahidi iwapo ataingia madarakani kama rais wa Indonesia atahakikisha kikosi cha timu ya taifa kinafanya vizuri katika mechi zake

"
 Iweje hata timu yetu ya taifa inashindwa kwenye mechi na wachezaji 11 wa ngazi ya klabu.Tutahakikisha tunalipa umuhimu wa pekee suala zima la timu ya taifa.Kwa hiyo ninachofikiri ni kwamba matatizo haya yanasababishwa na udhaifu katika uendeshaji,na uwezo mdogo wa kufikiri.Matatizo katika uongozi.Tunataka Indonesia iwe na timu ya taifa iliyo imara"
 Jenerali Prabowo ambaye aliwahi kuwa askari wa kikosi maalum,aliwahi kuwania kiti cha umakamu wa rais 2009 ambapo alibwagwa na mpinzani wake Megawati Sukamoputri.Ni mmoja kati ya wagombea wanaopewa nafasi kubwa ya kuingia ikulu ya nchi hiyo ya mashariki ya mbali 2014

Read more...
 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797