Pages

 

Friday, April 20, 2012

WOLPER ABADILI DINI

0 comments
Katika picha ni Jacqueline Wolper na aina ya usafiri anaotembelea sasa
Staa wa kike anaekamata kwenye kiwanda cha muvi za kibongo Jacqueline Wolper ametajwa kuwa amebadili dini kutoka kwenye ukristo na kuhamia kwenye uislam.Staa huyo amenukuliwa na gazeti moja akikiri kuwa amefanya zoezi hilo wiki mbili zilizopita katika Masjid Kichangani pale Magomeni Mapipa na kuwa hivi sasa anakwenda kwa jina la Ilham.
Inadaiwa kuwa Wolper amechukuwa hatua hiyo baada ya kupata mchumba wa kiislam ambae kwa mujibu wa habari inadaiwa kuwa anatarajiwa kufunga nae ndoa karibu.Mchumba wake huyo ambaye ametajwa kuwa anakwenda kwa jina la Dulla au Dallas inadaiwa ameshajitambulisha kwa wazazi wa Wolper na kuwa Wolper mwenyewe alishaonana na wazazi wa Dallas
"Nimekuwa nikimchunguza Dallas kwa muda sasa na nimeridhika na nia yake ya kuishi na mimi kama mke na mume"
 Msanii huyo amesema kuwa sasa anajulikana kwa majina ya Ilham Wolper Dallas.Habari zinaendelea kusema kuwa baada ya Wolper kukubali kufunga ndoa na kuslim,mchumba wake huyo alitoa zawadi kwa mkewe mtarajiwa ambayo ni gari ya bei mbaya aina ya BMW X6 kama inayoonekana pichani
Read more...

THIBITISHO KUWA HABARI ZA MIONZI HATARI NI UZUSHI!!!!

0 comments
Picha hii inaonekana kama ya tukio la kutisha juu ya anga la jiji la Moscow, ilipigwa usiku wa tarehe 28 mwezi uliopita na jopo la wanasayansi wanaoishi kwenye kituo cha kimataifa cha angani wakati chombo chao cha kusafiri kikipita umbali wa maili 240 kutoka uso wa dunia.Kipande cha kunasa nishati ya jua(solar array panel)inayotumiwa kuendesha kituo hicho kinaonekana kushoto mwa picha hii....Hapa  upinde wa mwanga,taa za jiji na mwanga wa jua la afajiri vimepamba anga

Jana kulikuwa na mshikemshike dunia nzima wakati binadamu walipopata taarifa za kushtua za kushuka kwa mionzi hatari kutoka anga za mbali(COSMO RAYS).Watu walioathirika na taarifa hizo za uongo ni watumiaji wa mawasiliano ya kompyuta (INTERNET) na simu

Watu walitembeza ujumbe kupitia Internet na simu kutarifu kuwa kuanzi usiku wa manane hadi saa 9.30 usiku watu wote wanashauriwa kuzima simu zao za mkononi na kuzuwe ka mbali nao   kwa kuwa mionzi hatari inayotokea sayari ya Mars itatua kwenye uso wa dunia,,,kwa maana kwamba watakaokaidi ushauri huo watakumbwa na mtatizo yatakayosababishwa na mionzi hiyo 

Uongo huu ni kama marejeo ya ule uliowahi kusambazwa miaka michachae iliyopita na kuzusha tafrani duniani.Ujumbe  kwenye mtandao mmoja wa kijamii ulikuwa:


"2nite 1230 a.m to 330a.m Cosmo rays entering earth frm Mars, So switch off ur mobile at nite,don't keep ur cell with u & put it away while ur slping bcos thy are quite dangerous rays.NASA BBC NEWS."
Lakini taarifa za uhakika zinakanusha kuwa si NASA wala BBC waliowahi kutoa tahadhari kama hiyo.Uchunguzi wangu unaonesha kuwa habari hizi zilianza kidogo kidogo wiki tatu zilizopita katika nchi nyingi za Asia.Mtu mmoja aliandika katika internet kukanusha habari hizo:

 

"I searched ON NASA web page and on latest space and science news, the Cosmo rays is indeed a rumor. Someone received this message from a friend on a blackberry messenger and he or she wanted to know if its true,so they posted the news on the internet.I am replying from Windhoek ,Namibia and this rumor seems to be everywhere.I also received the message. I have a theory to present.Here is my hypothesis:Someone send the Cosmo rays message on the 1st of April to a friend,they didn’t want to make it obvious since 1st April is a fools Day,to make this believable, they make a joke three day after April Fools Day(1st of April 2012). My dad just calls me and orders i switch off my phone this night (April 3). No reason given. I then stumble on this cosmic rays thing on a friend’s FB page and deside to google, not out of doubt but for more information. Now i know better….. Information is key!"
Mtu mwingine kutoka Japan aliandika:
" WHY THE HELL ARE THEY SPREADING THIS STUPID RUMOR????
Mars doesn’t produce cosmic rays.
  THIS IS JUST A RUMOR"


Na mwingine kutoka hapa nchini aliyejitambulisha kwa jina la Hija aliandika:

 
.."I JUST RECEIVED SMS HERE IN TANZANIA WITH THE SAME CONTENT, BUT I WENT ALL OVER THE WEB – NOTHING SEEMS TO SUPPORT THIS STUPID RUMOR.
P/S STOP IT !"

Na huyu nae alichangia kwa kusema:


"AHAHAHA…BELATED APRIL FOOL’S DAY!!!!!!!!!!!!!!! LOL!!!"









 
Read more...

Thursday, April 19, 2012

MTOTO WA AJABU AZALIWA PAKISTAN!

0 comments
Mtoto mwenye miguu sita amezaliwa mjini Sukkur nchini Pakistan wiki iliyopita na amelazwa kwa uangalizi kwenye Taasisi ya Taifa Inayoshughulika na Afya ya  Watoto ya nchi hiyo,NICH,jijini Karachi.
Mkurugenzi wa taasisi hiyo Dr. Jamal Raza,amefafanua kuwa katika hali isiyokuwa ya kawaida  ya mtoto huyo kuwa na miguu sita,mtoto huyo si mmoja kama anavyoonekana,bali ni watoto wawili katika mwili mmoja na kati yao mmoja bado hajakomaa.Amesema kuwa hali hii husababishwa na matatizo ya vinasaba(genetic desease) na kuwa matatizo hayo huwapata binadamu kwa uwiano wa kihesabu wa mtoto 1 kati ya watoto milioni 0.1.Amesema jopo la wataalam wa upasuaji watamfanyia uchunguzi wa kina mtoto huyo ili kuangalia namna ya kumsaidia na kwamba madaktari  bingwa kutoka nchi mbalimbali ikibidi wataitwa ili kusaidia
Read more...

Monday, April 16, 2012

MUAMBA ARUHUSIWA RASMI KUTOKA HOSPITALINI

0 comments
Fabrice Muamba akipeana mkono wa kuagana na madaktari Andrew Deaner na Sam Mohsin kutoka Kituo Cha Afya Cha Bart






                        
Read more...

EL HADJI DIOUF AKAMATWA NA POLISI

0 comments
Mwanasoka raia wa Senegal anaecheza mpira wa kulipwa nchini Uingereza katika klabu ya Blackburn Rovers El Hadji Diouf amekamatwa na polisi wa jiji la Manchester jana kwa tuhuma za kuhusika na fujo zilizotokea kwenye klabu moja ya usiku jijini humo
Katika fujo hizo ambazo zilitokea alfajiri ya kuamkia jana jumapili mtu mmoja anaetajwa kuwa na umri wamiaka 33 alijeruhiwa kichwani na shingoni
Diouf na watu wengine watano walikamatwa kwa tuhuma za kuhusika na fujo hizo na waliachiwa baadae kwa dhamana hadi kesi yao itakaposomwa hapo Mei 23 mwaka huu wakati uchunguzi juu ya tukio hilo unaendelea
Miaka 14 ya maisha ya soka la kulipwa ya Diouf imegubikwa na na matukioo ya utata kutokana natabia yake ya ukorofi.Hivi sasa mchezaji huyo amefungiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Senegal kucheza soka kwa muda wa miaka 5 baada ya kubwatuka mbele ya waandishi wa habari kuwa maafisa washirikisho hilo wanaendesha shughuli za shirikisho kama nyani
Read more...

MWENYEKITI WA VIJANA CCM ARUSHA AJITOA CCM

0 comments
         
Mwenyekiti waUmoja Wa Vijana Wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa Wa Arusha Bw.James Ole Millya ametangaza kujiondoa kwenye chama hicho leo mchana .Habari zaidi ungana nami baadae
Read more...

Sunday, April 15, 2012

REAL MADRID YAFANYA MABADILIKO KWA KUHESHIMU UISLAM

0 comments
Timu ya soka ya Hispania Real Madrid wamefanya mabadiliko kwenye nembo(logo) yao ya sasa kwa kuheshimu matakwa ya kiimani ya mashabiki wao wa kiislam.Miamba hiyo ya Hispania inatarajiwa kuondoa alama ya msalaba ambayo ipo kwenye nembo hiyo kwa karibu karne moja sasa
Timu nyingine ya Hispania ambayo ilifanya zoezi hilo ni miamba wengine wa Hispania Barcelona ambao waliamua kuondoa alama ya msalaba kwenye nembo yao
Read more...

MUVI ZA KANUMBA ZAANZA KURUSHWA NA DSTV MWEZI MZIMA KUANZIA JANA

0 comments

 Kuanzia jana Jumamosi kampuni ya televisheni ya kulipia kwa njia ya satellite, DSTV,kupitia chaneli yao ya Africa Magic Swahili, imeanza kurusha filam zilizochezwa na msanii maarufu wa tasnia ya filam nchini Tanzania, Marehemu Steven Kanumba aliyefariki ghafla nyumbani kwake Sinza usiku wa  kuamkia Jumamosi ya tarehe 7 Aprili
 Ikiwa ni sehemu ya kumuenzi Kanumba chaneli hiyo jana ilirusha filam ya UNCLE JJ kuanzia saa 1.30  usiku na leo jumapili kuanzia saa 2.00 usiku chaneli hiyo itarusha filam ya iitwayo THIS IS IT (Part1 na 2)

Jumamosi ijayo tarehe 21 April watarusha filam  MORE THAN PAIN kuanzia saa1.30 usiku ikifuatiwa na YOUNG BILLIONAIRE  (Part 1 na 2)itakayorushwa Jumapili kuanzia saa 2.00 usiku nautratibu huo utakamilishwa Jumamosi ya terehe 28 kwa filam BLACK SUNDAY ambayo itakuwa kwenye skrini saa 3.20 usiku wa siku hiyo

Mkurugenzi mwendeshaji wa M-Net Africa Bi Biola Abi alimwelezea msanii huyo kuwa alikuwa ni mwenye kipaji, uwezo na malengo.
"Ni lazima tumfurahie kijana huyu mwenye mambo makubwa, ambaye alizichangamsha skrini zetu na kukonga nyoyo za wengi.Kifo chake ni pigo kubwa kwenye tasnia ya burudani Afrika,tunapenda kuwapa pole nyingi familia marafiki na wote waliompenda"

Marehemu Steven Kanumba akitaka kujua wasanii wa Afrika Mashariki watanufaika vipi na mpango wa DSTV wa kurusha filam zao.Hii ilikuwa siku ya uzinduzi wa chaneli ya Africa Magic Swahili

Read more...

TUZO ZA KILI AWARDS NCHINI TANZANIA

0 comments
Vijana wa THT wakishambulia jukwaa jana wakati wa sherehe za kukabidhi tuzo za Kili Awards hapa jijini Dar Es Salaam
Msanii wa Bongoflava, Diamond akipokea tuzo yake
Mama Khadija Kopa akitoa mchango wake kuchangamsha sherehe
Khadija Kopa,mumewe na watoto wao katika  pozibaada ya kupokea tuzo
Mchekeshaji Steve Nyerere na msanii wa maigizo Sinta wakifuatili utoaji wa tuzo
Diamond Platinum janaaliwafunika wasanii wenzake wa muziki baada ya kujinyakulia tuzo tatu za Kilimanjaro Music Awards maarufu kama Kili Awards.Diamond alishinda tuzo kwa kuchaguliwa na washabiki wa muziki nchini kwa njia ya kura na alijizolea tuzo ya video bora ya mwaka kwa video ya wimbo `Moyo Wangu`,mtumbuizaji bora wa mwaka na mtunzi bora wa mwaka.Msanii kutoka Tanga Roma alipata tuzo mbili zikiwa ni Wimbo Bora Wa Hip hop(Mathematics) na Msanii Bora Wa Hip hop

Msanii anaechipukia ambaye alishiriki kuimba wimbo wa Nai Nai, Ommy Dimpozi ameweza kujinyakulia tuzo mbili,msanii bora chipukuzi na Wimbo Bora Wa Kushirikiana (Collabo) kwa wimbo wa `Nai Nai` ambayo amegawana na mshiriki mwenza kwenye wimbo huo  Ally Kiba ambae nae amepata tuzo nyingine ya Wimbo Bora wa Rhumba/Zouk kwa wimbo wake wa `Dushelele`
Tuzo zilikuwa hivi:
                  KILI TZ MUSIC AWARD (KTMA) 2012
1. Wimbo Bora Wa Reggae- Arusha Gold , Warriors from East

2. Wimbo Bora wa Dancehall- Maneno Maneno , Queen Darlin'
 
3. Wimbo Bora Zouk Rhumba- Dushelele By Ally Kiba
 
4. Wimbo bora wenye vionjo vya asili- Vifuu Tundu By A.T
 
5. Wimbo Bora wa Taarab- Nani kama Mama By Isha Mashauzi
 
6. Wimbo Bora wa Kiswahili(Bendi)- Dunia Daraja By Twanga Pepeta
 
7. wimbo Bora wa Afro Pop- Hakunaga By Suma Lee
 
8. Wimbo Bora wa R&B- My Number 1 Fan By Ben Pol
 
9. Wimbo Bora wa Hip Hop- Mathematics By Roma
 
10. Msanii Bora Anayechipukia- Ommy Dimpoz
 
11. Rapa Bora wa Bendi-Kitokololo
 
12. Msanii Bora wa Hip Hop- ROMA
 
13. Wimbo Bora wa Kushirikiana- Nai Nai By Ommy dimpoz ft Ally Kiba
 
14. Wimbo Bora Afrika Mashariki- Kigeugeu By Jaguar
 
15. Mtumbuizaji Bora wa kike- Khadija Koppa
 
16. Mtumbuizaji Bora wa Kiume- Diamond Platnumz
 
17. Mtunzi Bora wa kiume-Diamond Platnumz
Read more...
 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797