Pages

 

Saturday, May 5, 2012

SAGNA AVUNJIKA TENA MGUU,ATAIKOSA MICHUANO YA EURO 2012

0 comments
Beki wa kulia wa timu ya taifa ya Ufaransa anaechezea klabu ya Arsenal amevunjika mguu katika  mechi ya sare ya 3-3 dhidi ya Norwich City na atazikosa fainali zaKombe la Mataifa ya Ulaya yanayoanza tarehe 8 mwezi ujao.Sagna mwenye umri wa miaka 29 alivunjika mguu huo huo mwezi Oktoba na kuwa nje kwa miezi mitatu.

"Amevunjika mfupa wa nyuma ya ugoko.kwemye mguu ule ule ..ni lazima atakuwa amepigwa daruga sio hivi hivi tu.Kuna mchezaji amemwangusha na kisha akaukanyaga mguu wake...sijui ni bahati mbaya au vipi"Kocha wa Arsenal amewaambia waandishi wa habari.

 Yalikuwa ni matarajio ya wengi Sagna angejumuishwa katika kikosi kitakachokwenda kwenye fainali za Euro zitakazofanyika  kwenye nchi za Ukraine na Poland.Sagna hajachezea `Les Bleus` tangu mechi waliyotoka sare ya bila ya kufungana dhidi ya Romania mwezi Septemba wakati wa mchujo wa mashindano hayo makubwa  kabisa ya kimataifa barani ulaya.

Lakini kocha Laurent Blanc ana uchaguzi mpana wa mchezaji atakaeziba pengo la Sagna .Anthony Reveillere wa Olympique Lyon uwezo wa kucheza pande zote,kulia au kushoto na Mathieu Debuchy alionyesha kiwango kikubwa kwenye mechi dhidi ya Ujerumani mjini Bremen mwezi February.Blanc anatarajiwa kutaja vikosi viwili vya awali kabla hajachagua watakaounda timu. itakayoenda Euro.

Katika kikosi atakachokitangaza Jumatano hii,kitajumuisha wachezaji wanaocheza nje ya Ufaransa tu na Mei 15 atatangaza kikosi chenye wachezaji wanaocheza kwenye ligi za nyumbani

Blanc tayari alishamkosa beki wake wa kushoto Eric Abidal ambaye alifanyiwa upasuaji wa kubadilisha ini na pia kiungo Abou Duiaby naye ameumia nyama ya kiazi cha mguu

Ufaransa imepangwa kundi D pamoja na Uingereza,wenyeji Ukraine na Sweden
Read more...

MWANASOKA RASHID YEKINI AFARIKI DUNIA

0 comments
Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria Rashid Yekini amefariki dunia jana jioni kwa ugonjwa ambao taarifa zinasema ni wa ajabu, mjini Iraa, jimbo la Kwara,Nigeria.

Yekini alirejea kutoka nje ya nchi katikati ya wiki hii alikokuwa akipata matibabu,mchezaji mwenzake wa zamani Mutiu Adepoju aliwaambia wanahabari

Ndugu wa marehemu Yekini wamesema kuwa Yekini alikuwa akisumbuliwa na maradhi ambayo hawakuyaelewa.Yekini inasemekana alikuwa akiishi maisha ya kawaida sana tangu alipostaafu kucheza soka mwaka 2005 na kurudi Nigeria akitokea kucheza soka ulaya.

Alipokuwa ulaya alichezea timu za Vitoria Setubal yaUreno,Sporting Gijon ya Hispania na Olympiakos ya Ugiriki.Aliporudi Nigeria aliendelea na soka kwa kucheza katika ligi ya nyumbani ,NPL.Aliogopa umaarufu na hakupenda kujiweka mbele ya kamera na kalamu za waandishi wa habari na mara kadhaa alikataa vyeo mbali  mbali alivyopewa katika soka la Nigeria.

Wakati wa pilika pilika za kombe la dunia 2010 alikataa alipoombwa kuwa balozi wa Nigeria katika michuano hiyo na nafasi yake alikabidhiwa golikipa wa zamani wa Nigeria Ike Shorunmu

Mwezi uliopitan mchezaji mwenzake ambae walichezea timu ya taifa pamoja,kiungo Segun Odegbemi alikanusha taarifa juu ya hali mbaya ya afya mbaya Yekini.Na katika makala yake kwenye gazeti moja la nchi hiyo,Odegbemi aliwahakikishi wasomaji wake kuwa amefanya mazungumzo na Yekini na yuko mbioni kurudi katika ulimwerngu wa soka na mradi wa kuendeleza vipaji vya vijana katika soka

Mwandishi wa habari ambaye alifika ilipo nyumba ya Yekini mjini Ibadan, alielezwa kuwa mama wa Yekini ambae ni mtu mzima sana na mke wa pili wa Yekini walifika Ibadan kumchukua wiki mbili zilizopita, baada ya kupata taarifa kutoka kwa majirani kuwa Yekini alikuwa akifanya mambo ya ajabu

Nyumbani kwake kulikuwa kimya wakati huo na hakukuwa na dalili ya kuishi mtu kwani geti lilikuwa limefungwa na uwanjani zilipo nyumba zake nne kila kitu kilionekana ovyo na majani marefu yameota.Magari yake yalikuwa yameondolewa, na wapangaji wa Yekini waliokuwa wakiishi katika nyumba tatu walishahama kwa kile kilichoelezwa kuwa waliondolewa na Yekini mwenyewe.Watu wa kanisa lililopakana na nyumba ya Yekini walisema kuwa hawajamuona Yekini kwa mwezi mzima.

Yekini ambaye mwezi Oktoba angetimiza miaka 49 ya kuzaliwa  aliisaidia Nigeria katika michuano ya kombe la dunia 1994 Marekani.Goli lake ndio lilipeleka Nigeria kwenye hatua ya robo fainali,ikiwa ni mara ya kwanza kwa nchi hiyo kufikia mafanikio hayo.Na alitunukiwa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Afrika
Yekini anazikwa  kijijini kwao Offa leo Jumamosi kwa taratibu zote za kiislam
Read more...

Friday, May 4, 2012

RAIS KIKWETE ATANGAZA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI

0 comments
Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete




Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Jakaya Mrisho Kikwete amefanya marekebisho baraza la mawaziri na kulitangaza leo jioni huko ikulu.Na hii ni orodha ya baraza zima la mawaziri alilolitangaza 

 OFISI YA RAIS
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu)
Ndugu Stephen M. Wasira, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora)
Ndugu George Mkuchika, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (UTUMISHI)
Ndugu Celina Kombani, Mb.,
Ikulu

OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MUUNGANO)
Ndugu Samia H.  Suluhu, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MAZINGIRA)
Dr. Terezya P.L. Huvisa, Mb.,

OFISI  YA WAZIRI MKUU
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri  Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji)
Ndugu Mary M. Nagu, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi  ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Hawa Ghasia, Mb.,

Dr. Cyril Chami  (kaachwa)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge)
Ndugu William V. Lukuvi, Mb.,

WIZARA
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Ndugu Samuel J. Sitta, Mb.,

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Ndugu Shamsi Vuai Nahodha, Mb.,

Waziri wa Ujenzi
Dr.  John P. Magufuli, Mb.,

William Ngeleja (kaachwa)
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
Dr. Hussein A.H. Mwinyi, Mb.,

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Dr. Shukuru J. Kawambwa, Mb.,

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Ndugu Sophia M. Simba, Mb.,

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Ndugu Bernard K. Membe, Mb.,

Waziri wa Katiba na Sheria
Ndugu Mathias M. Chikawe, Mb.,
Dr Hadji Mponda (kaachwa)

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Ndugu Emmanuel Nchimbi, Mb.,

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Dr. David M. David, Mb.,

Waziri wa Kazi na Ajira
Ndugu Gaudentia M. Kabaka, Mb.,

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Prof.  Makame M. Mbarawa, Mb.,

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Prof.  Anna K. Tibaijuka, Mb.,
Mustafa Mkulo (kaachwa)

Waziri wa Maji
Prof. Jumanne Maghembe,  Mb.,

Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum
Prof. Mark Mwandosya, Mb.,

Waziri wa  Kilimo, Chakula na Ushirika
Eng. Christopher Chiza, Mb.,

Waziri wa Uchukuzi
Dr. Harrison Mwakyembe, Mb.,

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Dr. Fenella E. Mukangara, Mb.,

Waziri wa Maliasili na Utalii
Dr Lucy Nkya (kaachwa)
Ndugu Khamis Kagasheki, Mb.,

Waziri wa Viwanda na Biashara
Dr. Abdallah O. Kigoda, Mb.,

Waziri wa Fedha
Dr. William Mgimwa, Mb.,

Waziri wa Nishati na Madini
Prof. Sospeter Muhongo, Mb.,


Hii ni orodha ya Manaibu Waziri:

OFISI YA RAIS
Omari Nundu (kaachwa)
HAKUNA NAIBU WAZIRI

OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais
Ndugu Charles Kitwanga, Mb.,

OFISI YA WAZIRI MKUU
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi  ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Majaliwa K. Majaliwa, Mb.,

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi  ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Aggrey Mwanry, Mb.,

WIZARA MBALIMBALI
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira
Dr. Makongoro M. Mahanga, Mb.,

Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
Ndugu Adam Malima, Mb.,

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Ndugu Pereira A. Silima, Mb.,

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara
Ndugu Gregory G. Teu, Mb.,

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Ndugu Benedict N. Ole-Nangoro, Mb.,

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Ndugu Mahadhi J. Maalim, Mb.,

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo  ya Makazi,
Ndugu Goodluck J. Ole-Medeye, Mb.,

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Ndugu Ummy A. Mwalimu, Mb.,

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Ndugu Philipo A. Mulugo, Mb.,

Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dr. Abdulla Juma Abdulla, Mb.,

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
Ndugu Lazaro Nyalandu, Mb.,

Naibu Waziri wa Ujenzi
Ndugu Gerson Lwenge, Mb.,

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,
Dr. Seif Suleiman Rashid, Mb.,

Naibu Waziri wa Nishati na Madini
Ndugu George Simbachawene, Mb.,

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Ndugu January Makamba, Mb.,

Naibu Waziri wa Uchukuzi
Dr. Charles J. Tizeba, Mb.,

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Ndugu Amos Makala, Mb.,

Naibu Waziri wa Maji
Eng. Dr. Binilith Mahenge, Mb.,

Naibu Waziri Nishati na Madini
Ndugu Stephen Maselle, Mb.,

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
Ndugu Angela Jasmine Kairuki, Mb.,

Naibu Waziri wa Fedha
Ndugu Janet Mbene, Mb.,

Naibu Waziri wa Fedha
Ndugu Saada Mkuya Salum, Mb.
Read more...

NANI KASEMA KAMANDA KOVA LEGELEGE?MCHEKI AKIPITA JUU YA MOTO BILA VIATU MAZOEZINI JANA

0 comments
Hii ilikuwa jana kwenye maeneo ya Bwalo la Polisi Oyster bay. Zoezi lilifanyika baada ya makamanda kupata mafunzo ya kujenga ujasiri na kujiamini katika utendaji wa kila siku.
Read more...

RIPOTI ILYOKWENDA SHULE;MADHARA YA KUTUMIA OVYO FACEBOOK HAYA HAPA:

0 comments
Watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii hawajui madhara ya matumizi holela ya mitandao hiyo au hawataki kujihadhari na hatari zinazowakabili,ripoti imetolewa jana mjini Washington katika jarida la taasisi isiyo ya kiserikali, Consumer Reports

Ripoti hiyo inasema watumiaji wapatao 13 milioni wa Marekani hawajui au hawataki kutumia nyenzo za kujiweka salama kwenye mtandao wa facebook.Uchunguzi unaonesha kuwa wamarekani wapatao 4.5 milioni huwa wanaandika kwenye facebook wapi watakwenda na muda gani katika siku fulani na hii ni njia mojawapo ya kuwataarifu watu wabaya wanaoweza kudhuru,na pia kuna idadi nyingine ya wamarekani 4.7 milioni ambao wame `like` page zinazohusu mambo ya afya na tiba na kutoa taarifa za afya zao,bila ya kutambua kuwa kufanya hivyo ni kuyanufaisha makampuni ya bima.

Ripoti inaendelea kudokeza kuwa ni asilimia 37 tu ya watumiaji wa facebook ndio waotumia nyenzo za usalama wa taarifa zao kwenye facebook
"Facebook kwa kweli ni mtandao ambao kwa kiasi kikubwa umebadilisha namna watu wanavyoweza kuwasiliana duniani, na imekuwa huduma ambayo inafanikisha kwa kiwamgo kikubwa usambaaji wa taarifa binafsi za mtumiaji kwa umbali ambao hata mtumiaji mwenyewe hawezi kuamini"
Ripoti hiyo inaendelea kusema kuwa mwaka jana familia zipatazo 7 milioni zinazotumia mtandao wa facebook zimeripotiwa kuingia kwenye matatizo kutokana na facebook,matatizo kama vile watu wengine kuingia kwenye akaunti zao bila wao kujua,kusumbuliwa na kutishwa

"Uchunguzi wetu umegundua mambo ya kustaajabisha ambayo si ya kuyakalia kimya-lakini ni vyema wale wanaotaka kuziweka taarifa zao salama zaidi wajue"
Uchunguzi unaonesha kuwa facebook inakusanya taarifa nyingi za watumiaji pengine bila watuimiaji wenyewe kujua

Mtumiaji atashangaa kufahamishwa kuwa facebook wanakusanya taarifa kila anapoingia kwenye website yenye alama ya `like` bila kujali iwapo amebonyeza  alama au la...au ana akaunti ya facebook, au hata kama haja log in

Wachunguzi hao wamewashauri wamiliki wa facebook kulichukulia suala la usalama wa taarifa za watumiaji kwa umakini kwa kuweka nyenzo zitakazo dhibiti watumiaji wajanja.Pia wametahadharisha kuwa taarifa za watumiaji zinapochukuliwa ni jambo la hatari

Watumiaji walioulizwa mikakati yao katika kuweka salama taarifa zao kwenye facebook walitoa majibu ya kustaajabisha,robo yao huwa wanaweka taarifa  za uongo kwenye akaunti zao za facebook,ikiwa ni pamoja na  majina na tarehe za kuzaliwa

Idadi ya watu waliokiri kutumia taarifa za uongo imeongezeka maradufu ukilinganishwa na miaka miwili ilyopita swali hilo hilo lilipoulizwa,ingawa kisheria kitendo hicho ni kinyume na mkataba wa matumizi ya facebook

Mtandao wa facebook unasubriwa kwa hamu kubwa utakapoingia kwenye soko la hisa kwa mara ya kwanza wiki chache zijazo na kutarajiwa kuuza hisa zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 10,ikiwa ni kiasi kikubwa zaidi kuwahi kuuzwa na kampuni za internet katika soko la hisa la Wall Street

Idadi ya watumiaji wa facebook duniani imeongezeka na kufikia milioni 901 hadi ilipofika robo ya mwaka kwa mujibu wa nyaraka za kampuni hiyo.
Kwa taarifa zaidi tembelea link hii  http://www.consumerreports.org/cro/magazine/2012/06/facebook-your-privacy/index.htm
Read more...

Thursday, May 3, 2012

BIG BROTHER AFRICA HEWANI JUMAPILI, WASHIRIKI HAWA HAPA, RAPPER `PREZZO` WA KENYA NAYE NDANI YA MJENGO!

0 comments
Hii ndio logo ya gemu msimu huu wa 7
Lile shindano maarufu la kwenye televisheni duniani kwa upande wa Afrika, BIG BROTHER AFRICA,linaanza rasmi siku ya Jumapili tarehe 6 huko nchini Afrika Kusini.Shindano hilo linalorushwa na kampuni ya televisheni ya kulipia (PPV) ya DSTV kupitia chaneli maalum namba 198 na Africa Magic (chaneli namba114) litaanza kuwa hewani  siku hiyo  kuanzia  majira ya saa 3.00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki,huku washiriki wa shindano hilo linalopendwa kwa kiwango kikubwa na vijana,wakitangazwa na kuoneshwa jinsi wanavyoingia ndani ya jumba la Big Brother lililopo katika eneo la  Hendrik Verwoerd Drive, Randburg 2194, South Africa.Jumba la 
Sebule inavyoonekana
Chumba cha kulala washiriki
Sehemu ya kujiswafi aka bafuni and chooni
Big Brother Africa likiwa limeng`arishwa na kunakshiwa upya,litakuwa ni suprise kwa watazamaji kwani Big Brother mwenyewe ameahidi hivyo.Shindano la mwaka huu ni shindano la saba tangu mashindano hayo yaanze mwaka mwaka 2003, huku safari hii likiwa limebatizwa jina la `BIG BROTHER STARGAME.`na washiriki wataitwa `STARMATES `Kawaida nchi 12 hushiriki kwenye kinyang`anyiro hicho lakini safari hii zimeongezwa nchi mbili ambazo ni Liberia na Sierra Leone,nchi zingine ni Angola,Botswana,Ghana ,Kenya,Malawi,Namibia,Nigeria,Afrika Kusini,Tanzania,Uganda ,Zambia ,Zimbabwe,Ethiopia na Msumbiji
Hii ni` batch` ya washiriki maarufu (CELEBRITIES)watakaoingia mjengoni msimu huu

Shindano la mwaka huu ni wazi kuwa litawatia watazamaji homa,kwa sababu tofauti na mashindano yaliyopita safari hii kila mshiriki anatakiwa aingie kwenye jumba akiwa na mwenza ,mpenzi,rafiki,jirani au mama.Kuna suprise nyingi ambazo zimeandaliwa na Biggy na mojawapo ni uwepo wa majumba mawili...UPVILLE na DOWNVILLE.Mshindi atajiondokea na kitita cha dola 300 000 za kimarekani ambazo ni sawa na zaidi ya Tshs. 475 milioni.Kama kawaida ya suprise za Biggy, mwaka jana wakati shindano linaisha Jumapili ya Julai 31 walipatikana washindi wawili, Karen Igo msichana aliekuwa na umri wa miaka 27 kutoka Nigeria ambae alipata dola 200 000 na Wendall Parson mvulana aliyekuwa na umri wa miaka 23 kutoka Zimbabwe ambae nae alipata  dola za kimarekani 200 000


Tayari washiriki saba ambao ni kundi la waburudishaji maarufu barani Afrika (CELEBRITIES) wameshathibitishwa kushiriki huku washiriki wengine wakiendelea kutajwa kila siku zinavyosogea.Waliotajwa ni
Mampi (Zambia)
Roki (Zimbabwe)
Prezzo(Kenya)
Mchekeshaji Derrick ambae atakwenda kwa jina la DKB ( Ghana, miaka 26)

•Msanii wa muziki wa rap Prezzo ambae atakwenda kwa jina hilo hilo Prezzo (Kenya, miaka 32)

•Mwimbaji Martha ambae ataitwa Lady May ( Namibia, miaka 25)

•Mwanamuziki wa pop Suzan ambae ataitwa Goldie ( Nigeria, miaka (28)

•Mwanamitindo na mfanyabiashara,Babalwa ataenda na jina la Barbz ( South Africa, miaka 34)

Barbz (Afrika Kusini)
•Mwananuziki wa R&B Mampi atakaekwenda na jina lake hilo Mampi  (Zambia, miaka25)

•Mwanamuziki wakike Rockford ambae ataitwa Roki ( Zimbabwe,miaka 27)
Eazzy(Ghana ,hajathibitishwa)
Keita (Ghana,hajathibitishwa)
Pia kuna habari ambazo hazijathibitishwa kuwa mwana muziki wa kike wa Ghana Eazzy pamoja na mwanamitindo na mbunifu wa mavazi Keita wataungana na DKB kuiwakilisha Ghana.Tetesi zinasema kuwa Eazzy na Keita wanaingia kama wapenzi na DKB kama msanii maarufu(CELEBRITY) 
DKB ( Ghana)


Goldie(Nigeria)
Rapper J Cole atapamba ufunguzi
Kundi la Mulla kutoka Kenya
Lady May(Namibia)


Ufunguzi wa mwaka huu hapo Jumapili utapambwa na wasanii mbalimbali akiwemo mwanamuziki  J.Cole kutoka Marekani anaeletwa na kampuni ya burudani ya One Entertainment ya Los Angeles,ambayo mwaka jana ilifanikisha ujio wa Busta Rhymes kwenye Big Brother `Amplified.`Habari zinasema kuwa J.Cole atapanda jukwaani kuwasindikiza washiriki na nyimbo tatu,`Can`t Get Enough,Nobody`s Perfect na Work Out` Pia wasanii wengine watakao perform kama Mulla kutoka Kenya na wengine.
IK Osakioduwa wa Nigeria
Kama kawaida IK Osakioduwa atakuwa kilingeni kuendesha mambo.Kwa wale ambao watakuwa mbali na Tv zao wanaweza kuona  shindano hili kupitia mtandaoni kwa link hii:www.africamagic.tv/bigbrother
Read more...

ONA DILI LA DEMBA BA NA SHABIKI WA MAN UTD KATIKA TWITTER ILI AIFUNGE MAN CITY JUMAPILI

0 comments
Mshabiki mmoja wa Man Utd aliyejiita Jordan McDonald ameingia makubaliano na mshambuliaji wa Newcastle Demba Ba kwenye mtandao wa Twitter kuwa iwapo Ba  ataifunga Man City Jumapili hii basi McDonald atapachika jina la DEMBA BA nyuma ya jezi yake ya Man Utd
Read more...

Wednesday, May 2, 2012

PICHA ZAIDI ZA AJALI YA BASI LA NBS

1 comments
Hivi ndivyo hali ilvyokuwa baada ya ajali mbaya ya basi la abiria la kampuni ya usafirishaji ya NBS iliyotokea leo mapema kwenye milango ya saa nne.Habari zinaeleza kuwa dereva basi hilo ni miongoni mwa watu waliopoteza maisha na kwamba mwili wake bado ulikuwa umebanwa na mabati ya mabaki ya basi hilo na hivyo kushindikana kuutoa hadi vifaa maalum vitakapofika eneo la tukio.maiti sita tayari zimeshafikishwa hospitali ingawa zoezi la kutoa miili bado linaendelea.Walioshuhudia wanasema kuwa basi hilo lilipasuka mpira wa tairi moja la mbele likiwa kwenye mwendo wa kasi nahivyo kulifanya liache njia na kwenda kuparamia mti kabla halijajiviringisha..Taarifa hizi zitaendelea kadri zinavyofika
Read more...

BREAKING NEWS...BASI LA NBS LAPATA AJALI MUDA SI MREFU ULIOPITA:waliosalimika ni wanne tu

0 comments
Basi la abiria la kampuni ya NBS linalotoka Tabora kwenda Arusha limepata ajali mchana huu na kusababisha vifo.Habari zilizonifikia zinasema kuwa chanzo cha ajali ni kupasuika kwa mpira wa tairi la mbele na kwamba inasemekana ni watu wanne tu ndio waliosalimika,Nitaendelea kuywaletea habari zaidi za tukio hili kadri ninavyoweza
Read more...
 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797