HABARI ZAKISIASA
UTAPATA HABARI MBALIMBALI ZA KISIASA KUTOKA NDANI NA NJE YA NCHI, UKIWA HAPAHAPASAID NUHU

HABARI ZA BURUDANI
UKIWA HAPA UTAPATA HABARI ZOTE ZA BURUDANI KUTOKA KILA KONA YA DUNIA...SAID NUHU

HABARI ZA MICHEZO
UKIWA HAPA UTAPATA HABARI ZA KILA AINA YA MICHEZO, KUANZIA MPIRA WA MIGUU, BASKETBALL, GOLF NKSAID NUHU

HABARI ZA KIMATAIFA
HAPA UTAPATA HABARI ZA KIMATAIFA KUTOKA KILA KONA YA DUNIAMore
Sunday, July 7, 2013
AIBU!!DIAMOND PLATINUMZ AMUUMBUA DIAMOND FEKI WA KWENYE FACEBOOK !
Katika hali ya kuchoshwa na tabia za watu wanaotumia majina ya wasanii na watu maarufu kujipatia wafuasi kwenye akaunti zao za Facebook au Twitter msanii Naseeb Abdul ambae kisanii anatumia jina la Diamond Platinumz ameibuka na shutuma nzito dhidi ya watu wenye tabia hio na kufikia hatua kumuibua DIAMOND PLATINUMZ feki ambaye kwenye akaunti yake ya Facebook anatumia jina la Diamond Platinumz Swaqq
Muda mfupi baada ya ujumbe wa Diamond Platinumz kuwa hewani Diamond feki aliweka hadharani mambo kwa `washabiki` wake kwa kuweka picha ambayo nayo inatia wasiwasi iwapo haendelei kuwadanganya
Na matusi hayakuishia hapo,Diamond feki bado anaendelea kupokea Comment za kumlaani
Muda mfupi baada ya ujumbe wa Diamond Platinumz kuwa hewani Diamond feki aliweka hadharani mambo kwa `washabiki` wake kwa kuweka picha ambayo nayo inatia wasiwasi iwapo haendelei kuwadanganya
MJUE MWANAMKE MWENYE KUCHA NDEFU KULIKO WOTE DUNIANI
Anaitwa Chris Walton na pia kimuziki anaitwa `The Duchess` ndie alieingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia cha Guinness Book of World Record kama mwanamke mwenye kucha ndefu kuliko wote duniani kwa sasa.
Inasemwa kuwa unapokutana na mwanadada huyo hakuna jinsi bali ni kumwangalia kwa mshangao,lakini angalau kucha zake ni safi na zinang`arishwa kwa dawa maalum
Anaweza akachukuliwa kama mchafu kwa kuwa hajazikata kwa miaka 20 lakini mrembo huyo mwenyeji wa Las Vegas kwa Obama,amewavuta watu wa Guinness World Book of Record.The Duchess ni muimbaji anaechipukia kwenye fani kwa sasa.Awali mwanamama Lee Redmond ndie aliekuwa akiongoza kwa kushikilia rekodi ya kuwa na kucha ndefu kuliko wote ambazo zilifikia urefu wa futi 28 kabla hazijavunjika katika ajali ya gari mwaka 2011.Kabla ya ajali ,Bi Redmond hakuwahi kukata kucha za vidole vyake vya mkononi tangu mwaka 1979!

![]() |
Bibi Lee Redmond |
MABOMU YA MACHOZI YAITIKISA DAR
JESHI
la Polisi jijini Dar es Salaam, jana lililazimika kutumia mabomu ya
machozi maeneo ya Manzese, kuwatawanya wafanyabiashara wadogowadogo
(Machinga) waliogoma kupisha ujenzi unaoendelea wa mabasi yaendayo kasi
(DART).
Polisi wakiwa katika magari yao waliwatawanya
wafanyabiashara hao waliokuwa wamegoma kutoka kutokana na kudai kuwa
eneo hilo ni muhimu kwao kwa ajili ya kuendeshea biashara.
Wakiwa na silaha mbalimbali, ikiwemo za moto, walifanikiwa
kuwatawanya wafanyabiashara hao kwa kutumia mabomu ya machozi.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa operasheni hiyo ilianza tangu wiki
iliyopita, kutokana na ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama, pamoja
na familia yake.
Operesheni ya kuwaondoa wafanyabiashara hao ilianza jana asubuhi
na ilikwenda vizuri, baadaye baadhi ya askari walipungua na kubaki
wachache, hapo ndipo wafanyabiashara walipopata mwanya wa kurudi
barabarani na kufunga barabara kwa kuweka mawe ili magari yasipite.
“Kosa lilikuwa ni kupunguza askari, hapo ndipo wafanyabiashara
tulijikusanya na kuweka mawe ili askari wasipite kuja kutuzuia wala
magari yasipite,” alisema askari aliyeshudia.
Mtu mwingine aliyejitambulisha kwa jina
Juma Mohamed, alisema wanashangaa askari kuendelea na operasheni hiyo
kwa kuwa kama ni ujio wa Obama ulishapita, hivyo waruhusiwe kurudi
katika maeneo hayo.
Magari ya Makamanda wa Polisi (OCD) wa
vituo mbalimbali, ikiwemo Kimara na Kinondoni, yakiwa na
Makamanda wao, yalikuja kuongeza nguvu, huku gari jingine la polisi
likiwasomba waliokamatwa katika oparesheni hiyo.
Aidha, maeneo
ya kuanzia Darajani mpaka soko la Manzese kulikuwa kumewekwa mawe
barabarani, huku barabara inayojengwa ikiwa imevunjwa katika baadhi ya
maeneo kutokana na vurugu hizo.
Maeneo hayo yote palikuwa
kimya, tofauti na siku zote ambapo kunakuwa na biashara mbalimbali
zikiendelea, huku polisi wakiwaaamuru watu wanaopita kutembea kwa mwendo
wa haraka pamoja na kutosogelea eneo la tukio.
Pia maduka yote
katika maeneo hayo yalikuwa yamefungwa na baada ya muda wa mapambano
hali ilianza kutulia kuanzia saa 9:00 alasiri.
Operasheni hiyo
inaelezwa kulenga kuwaondoa wafanyabiashara wadogowadogo ili kuweza
kupisha ukamilishaji wa ujenzi wa Barabara ya Morogoro, inayojengwa kwa
ajili ya mabasi yaendayo kasi (DART).
USAIN BOLT KUCHEZEA MANCHESTER UNITED!
![]() |
Usain Bolt |
Mwanariadha huyo, ambaye inasemekana ndie binadamu mwenye kasi kuliko wote duniani,atakuwepo katika kikosi kitakachomenyana na timu ya Seville kutoka Hispania,katika dimba la Old Trafford, siku ya tarehe 9 mwezi ujao.
"Matamanio yake sasa yatatimia,Bolt atakuwemo kwenye kikosi na kucheza sambamba na Rio.Utakuwa mchezo wa aina yake,kwa kuwa watu watapendeza kuona kama kasi yake inaweza kwenda na uwezo wake wa kumiliki mpira."Kimeongea chanzo cha ndani ya klabu hiyo.Uteuzi wa Bolt kwenye kikosi hicho unatarajiwa kutangazwa wiki ijayo.
Saturday, July 6, 2013
REFA NA MCHEZAJI WAUAWA KINYAMA BRAZIL
Baada ya kwisha kwa pilikapilika za Kombe la Mabara nchini Brazil,sambamba na vurugu mitaani,huku nchi hiyo kubwa ya Amerika ya Kusini ikikabiliwa na changamoto nyingine ya kuwa mwenyeji wa mashindano yajayo ya Kombe la Dunia 2014,nchi hiyo imeingia kwenye taswira mbaya-kwa mara nyingine-baada ya kuripotiwa kutokea mauaji ya kutisha ya mchezaji na mwamuzi katika mechi mjini Maranhao ,kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Taarifa zinasema kuwa Otávio Jordão da Silva ambae alikuwa mwamuzi wa mechi hiyo na ambae alikuwa akishambuliwa kwa matusi muda wote wa mechi, alichomoa kisu baada kumaliza mechi na kisha kumchoma nacho mchezaji mmoja mwenye umri wa miaka 31 aitwae Josemir Santos na kumsababishia majeraha ambayo hatimae yalisababisha kifo chake.
Ndugu na marafiki wa mchezaji huyo walipogundua kuwa Santos ameshafariki,walilipiza kisasi kwa kumchoma kisu mwamuzi huyo,ambae baadae kundi la watu liliendelea kumpiga,na kummalizia kwa kumkata vipande vipande na kunyofoa kichwa chake kabla hawajakichomeka kwenye mti na kukiweka kama bendera katikati ya uwanja.
Hakuna taarifa zaidi juu ya tukio hilo, lakini picha zilizowekwa mtandaoni na mtandao wa 101GREAT GOALS zimethibitisha kutokea kwa tukio hilo

Marehemu Josemir Santos Abreu |
Friday, July 5, 2013
FACEBOOK YAZINDUA HASHTAG
Kwa wale watumiaji wa Twitter nadhani wanaelewa inapotajwa HASHTAG...neno ambalo kwa mitandao inaiyotumia huwa ni kama neno linaloweza kuwaunganisha moja kwa moja kuingia kwenye topic (jambo linaloongelewa) inayohusiana nayo ambayo ipo hewani inazungumziwa...ili iwe HASHTAG neno lenyewe lazima lianze na alama (symbol) # na bila kuacha nafasi linafuata neno lenyewe;mfano HASHTAG hii #saidnuhublog...kwahiyo watu wote ambao hujadili Said Nuhu Blog watatumia HASHTAG hii ili kumuunganisha na wengine wanaotaka kuchangia ,huo ni mfano tu...na yeyote ambae yuko mtandaoni akikutana na alama-neno hii,akaibonyeza, basi mtandao utampeleka moja kwa moja kwenye mjadala husika.aidha ataangalia mjadala unavyokwenda au anaweza kuchangia anachojisikia.
Kampuni ya FACEBOOK imezindua matumizi ya HASHTAG kwa ajili ya watumiaji wake wote ikifuata nyayo za kampuni ya Twitter...hatua hii ni jitihada za kampuni hiyo kuboresha huduma zake ili isiachwe nyuma na makampuni mengine,lakini wachunguzi wa mambo ya mitandao ya kijamii wanaona kuwa wazo hili litakuwa na faida zaidi kwa watu wanaotangaza biashara zao kupitia mitandao ya kijamii
CHANZO:THE UNDERCOVER RECRUITER
Read more...

THIAGO ALCANTARA:ANAWEZA ASICHEZEE BARCELONA MSIMU UJAO,USHAHIDI HUU HAPA
Miamba ya soka ya Hispania FC Barcelona wametoa wameiondoa taswira ya mchezaji wao Thiago Alcantara kutoka katika picha ya pamoja ya wachezaji wa timu hiyo.Awali kwenye picha hiyo taswira ya Alcantara ilikuwepo kwenye picha hiyo lakini sasa imeondolewa kama ilivyoonekana katika toleo jipya la picha hiyo ndani ya mtandao wa Instalgram katika ukurasa wa timu hiyo jana.
Dogo huyo amekowa gumzo kubwa kipindi hiki cha usajili wa wachezaji barani Ulaya huku bosi mpya wa Manchester United David Moyes akionesha nia ya kumnyakua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22
chanzo :mirror football

Friday, July 6, 2012
IJUE TEKNOLOJIA MPYA YA GOLINI KWA UFASAHA
![]() |
Hawk-Eye |
Washabiki wa soka wanaofuatilia kwa makini Ligi Kuu ya
Uingereza Premier League,wataanza kuiona teknolojia ya golini ikitumika kwenye
ligi hiyo ifikapo mwezi Januari mwakani baada ya Bodi ya Kimataifa ya Vyama vya
Soka Ulimwenguni (IFAB) kutia tiki matumizi ya teknolojia hiyo katikati ya
wiki.
IFAB(International FA Board)imeingiza teknolojia hiyo kuwa
moja ya sheria zitakazoendesha mchezo huo,na kufungua ukurasa mpya kabisa
katika historia ya mchezo huo unaopendwa zaidi duniani
Mifumo miwili ya teknolojia hiyo ndio iliyopitishwa na
kuruhusiwa kutumika baada ya majaribio mengi ya kisayansi kuwa
yamefanyika.Mifumo hiyo Hawk-Eye na GoalRef inafanya kazi hivi:
HAWK-EYE.
Ni mfumo unaotegemea kamera,ambao ulitengenezwa na kampuni
ya Uingereza ya Hawkeye,na kununuliwa na kampuni ya Kijapan ya Sony mwaka jana,teknolojia
ambayo kwa muda imekuwa ikisaidia maamuzi kwenye michezo ya kriketi na tennis
Kamera 6 au 7 zenye uwezo wa kupiga picha kwa kasi ya ajabu
zitafungwa pande zote mbili za uwanja na nyingine juu,zitakuwa na kazi ya kufuatilia
mpira kila utakapokwenda ndani ya uwanja,kompyuta yenye uwezo wa kusoma taarifa
kwa usahihi wa hali ya juu itakuwa ikipokea picha kutoka kwenye kamera
hizo,kuzitafsiri kwa kasi na hapo hapo kutuma matokeo kwenye kifaa mfano wa saa
ambacho mwamuzi atavaa mkononi kama kinavyoonekana pichani.
Kitu ambacho badomkinatia shaka ni iwapo kamera hizo
zitafanya kazi kwa ufanisi iwapo mpira utakuwa umekumbatiwa na golikipa katika
jitihada za kuwahi kuokoa.
Ingekuwa jambo zuri iwapo picha zinazotoka kwenye kamera
hizo zingerushwa kwenye `replay`(picha za marudio) za kwenye TV pale unapotokea
utata ili na sisi watazamaji tushuhudie jinsi teknojia hiyo inavyofanya
kazi,lakini bahati mbaya FIFA wamesisitiza kuwa picha hizo hazitaoneshwa, si
kwenye TV za uwanjani tu, hata majumbani!Kitu pekee kitakachofanyika ni mwamuzi
wa mchezo kupewa ishara na kifaa alichovaa iwapo mpira utavuka mstari wa goli.
![]() |
GoalRef |
GOALREF
Teknolojia hii ina mfumo uliobuniwa kwa ushirikiano wa
wataalam wa Denmark na Ujerumani,na imeundwa kwa mfumo wa sumaku maalum ambayo
inauwezo wa kugundua iwapo mpira utavuka mstari wa goli.
Kamba maalum ndogo
ndogo 3 zenye sumaku zinawekwa kwa ndani kwenye mpira eneo kati ya gozi na
blada na mpira utnapo vuka mstari wa goli sumaku hii iliyo ndani ya mpira hutoa
ishara kwenye vifaa maalum (sensor) vilivyowekwa ndani ya nguzo ya juu na zile
mbili za goli.
Zile sensor zinapopata taarifa kutoka kwenye sumaku huwa
kama zimetekenywa na kutoa aina ya mawimbi ya umeme ambayo bila kuchelewa
hudakwa na kompyuta ambayo nayo hupeleka taarifa kwenye kifaa kama saa
atakachovaa mwamuzi mkononi mwake..yote hayo niliyoyataja hufanyika chini ya
sekunde moja!
Hii teknolojia ya GoalRef inatarajiwa kuwa na gharama kidogo
katika kununua na kuifunga kuliko ile ya Hawk-Eye,lakini kampuni
zinazotengeneza mipira bado zinajishauri iwapo ni sahihi kuweka sumaku ndani ya
mipira yao,ila wataalam wa GoalRef
wanaendelea kutoa ushawishi wa kitaalam kuthibitisha kuwa hakuna tatizo.
…………………JE UNA MAONI GANI MSHABIKI WA SOKA?
Subscribe to:
Posts (Atom)