Pages

 

Sunday, July 7, 2013

BEYONCE APATA MAMA WA KAMBO

0 comments
Wanamuziki Beyonce na Solange ambao ni mtu na dada wamepata mama wa kambo baada ya baba yao kufunga ndoa na mwanamke mwingine,kufuatia kuachana na mama yao mzazi akina Beyonce
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la AP, Mathew Knowles,baba wa akina Beyonce,ambae pia alikuwa meneja wa Beyonce alifunga ndoa na rafiki yake wa kike,mwanamitindo Gena Charmaine Avery huko Houston Texas,mwishoni mwa wiki iliyopita.Mathew Knowles mwenye umri wa miaka 61 na Gena Avery mwenye umri wa miaka 48,walikuwa wameshachumbiana mwaka mmoja na nusu uliopita.Beyonce na Solange hawakuhudhuria harusi.
Mathew Knowles alitalakiana rasmi na mama mzazi wa akina Beyonce,Tina Knowles,mwaka 2011 baada ya mama huyo kufungua kesi ya kudai talaka mwaka 2009.Ndoa yao ilidumu kwa miaka 29.
Read more...

ZITTO KABWE ATUMA WARAKA KWA WAANDAAJI WA TAMASHA LA MATUMAINI AKIWA MAREKANI

0 comments
Global Publishers leo 7.7.2013 waliandaa Tamasha la Matumaini. Bahati mbaya sana sikuweza kuwahi kutokana na safari nilizonazo. Hii ni hotuba niliyopanga kuitoa na kuwatumia waandaaji.

TAMASHA LA MATUMAINI

Leo nilikuwa niwe nanyi kwa ajili ya siku hii muhimu sana kwa nchi yetu, siku ya matumaini kama inavyoandaliwa na Kampuni ya Global Publishers. Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa ndugu yangu Erick Shigongo kwa kuandaa tamasha hili kila mwaka. Nasikitika kuwa sitaweza kufanya pambano la ngumi na ndugu Ray na pia kuchezea timu yangu ya Wabunge wa Simba dhidi ya watani zetu Yanga. Hata hivyo naamini kuwa tamasha litakuwa na mafanikio makubwa na nipo nanyi japo sipo Dar es Salaam.

Ilikuwa niwepo Dar es Salaam leo, lakini nimeshindwa kuondoka Marekani kwa sababu Spika wa Bunge Mama Anna Makinda ameniagiza kwenye safari nyingine ndefu kwenda visiwa vya Cayman na baadaye Namibia kwa shughuli za Umoja wa Wabunge wa Jumuiya ya Madola. Sikuweza kukwepa jukumu hili la kitaifa maana limekuja ghafla na mimi nipo huku jirani na maeneo hayo. Naomba radhi sana kwamba sipo nanyi leo.

Nawaomba muiombee amani nchi yetu na msimamie haki kwa wananchi wote bila kubagua dini zao, rangi zao, hali yao kimaisha na ufuasi wa vyama vya siasa. Mwaka huu tumeshuhudia matukio ambayo yanatikisa msingi wa Taifa letu – Umoja. Hivi sasa msingi wetu una nyufa ambazo kwa kweli hatujajua bado nini kinacholeteleza mambo haya kama kulipua makanisa, kulipua mikutano ya vyama vya siasa na kuua viongozi wa dini.

Matukio haya yanatuelekeza kuwa makini sana na kauli zetu kwani baadala ya kuunganisha wananchi tunawezajikuta tunawagawa zaidi Watanzania na hivyo kuwa na mzunguko wa machafuko (vicious circle of violence). Ni wajibu wa viongozi wa kisiasa na wananchi kuepuka kabisa kuanza kurushiana maneno na lawama kuhusu matukio haya, kwani inawezekana lawama na maneno yetu yakawa yanampa nguvu adui wetu ambayo hatujamjua bado.

Napenda niwakumbushe kwamba ni rahisi sana kusambaza chuki na ni vigumu sana kuondoa chuki miongoni mwa wananchi. Viongozi hatari kama Hitler walitumia sana mbinu ya kueneza chuki dhidi ya jamii ya Jews na matokeo yake yalikuwa ni vita vikuu vya pili vya dunia na zaidi ya watu milioni 6 wasio na hatia kupoteza maisha. Sisi sote tuna jukumu moja la kuhakikisha tunajenga Taifa lenye kujali HAKI na lenye mshikamano mkubwa miongoni mwa raia. Kwa nia hii tu ndio tutaweza kuwa na Taifa imara lenye heshima mbele ya mataifa mengine duniani. Ni kwa njia hiyo tu ndio tutaweza kutokomeza umasikini uliokithiri mijini na vijijini hapa nchini kwa kuongeza uzalishaji na kupanua ajira. Ikumbukwe bila HAKI hakuna AMANI na bila UWAJIBIKAJI hakuna UTULIVU.

Tukiegemea siasa za CHUKI. Tukashindwa kuwa na mahusiano ya kawaida miongoni mwa viongozi kuhusu masuala ya msingi ya nchi. Tukashindwa kujadiliana kwa hoja kuhusu sera zetu. Tutapata viongozi aina ya Hitler nchini mwetu. Wote tukatae. Sisi ni Watanzania. Muwe na Tamasha jema la Matumaini.

Zitto Kabwe
7.7.2013, Aspen Colorado, USA
Read more...

AIBU!!DIAMOND PLATINUMZ AMUUMBUA DIAMOND FEKI WA KWENYE FACEBOOK !

0 comments
Katika hali ya kuchoshwa na tabia za watu wanaotumia majina ya wasanii na watu maarufu kujipatia wafuasi kwenye akaunti zao za Facebook  au Twitter msanii Naseeb Abdul ambae kisanii anatumia jina la Diamond Platinumz ameibuka na shutuma nzito dhidi ya watu wenye tabia hio na kufikia hatua kumuibua DIAMOND PLATINUMZ feki ambaye kwenye akaunti yake ya Facebook anatumia jina la Diamond Platinumz Swaqq

Muda mfupi baada ya ujumbe wa Diamond Platinumz kuwa hewani Diamond feki aliweka hadharani mambo kwa `washabiki` wake kwa kuweka picha ambayo nayo inatia wasiwasi iwapo haendelei kuwadanganya



Na matusi hayakuishia hapo,Diamond feki bado anaendelea kupokea Comment za kumlaani
Read more...

MJUE MWANAMKE MWENYE KUCHA NDEFU KULIKO WOTE DUNIANI

0 comments
Anaitwa Chris Walton na pia kimuziki anaitwa `The Duchess` ndie alieingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia cha Guinness Book of World Record kama mwanamke mwenye kucha ndefu kuliko wote duniani kwa sasa.
Inasemwa kuwa unapokutana na mwanadada huyo hakuna jinsi bali ni kumwangalia kwa mshangao,lakini angalau kucha zake ni safi na zinang`arishwa kwa dawa maalum
Anaweza akachukuliwa kama mchafu kwa kuwa hajazikata kwa miaka 20 lakini mrembo huyo mwenyeji wa Las Vegas kwa Obama,amewavuta watu wa Guinness World  Book of Record.The Duchess ni muimbaji anaechipukia kwenye fani kwa sasa.Awali mwanamama Lee Redmond ndie aliekuwa  akiongoza kwa kushikilia rekodi ya kuwa na kucha ndefu kuliko wote ambazo zilifikia urefu wa futi 28 kabla hazijavunjika katika ajali ya gari mwaka 2011.Kabla ya ajali ,Bi Redmond hakuwahi kukata kucha za vidole vyake vya mkononi tangu mwaka 1979!
Bibi Lee Redmond


Read more...

MABOMU YA MACHOZI YAITIKISA DAR

0 comments
JESHI la Polisi jijini Dar es Salaam, jana lililazimika kutumia mabomu ya machozi maeneo ya Manzese, kuwatawanya wafanyabiashara wadogowadogo (Machinga) waliogoma kupisha ujenzi unaoendelea wa mabasi yaendayo kasi (DART).
Polisi  wakiwa katika magari yao waliwatawanya wafanyabiashara hao waliokuwa wamegoma kutoka kutokana na kudai kuwa eneo hilo ni muhimu kwao kwa ajili ya kuendeshea biashara.
Wakiwa na silaha mbalimbali, ikiwemo za moto, walifanikiwa kuwatawanya wafanyabiashara hao kwa kutumia mabomu ya machozi.

Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa operasheni hiyo ilianza tangu wiki iliyopita, kutokana na ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama, pamoja na familia yake.

 Operesheni ya kuwaondoa wafanyabiashara hao ilianza jana asubuhi na ilikwenda vizuri, baadaye baadhi ya askari walipungua na kubaki wachache, hapo ndipo wafanyabiashara walipopata mwanya wa kurudi barabarani na kufunga barabara kwa kuweka mawe ili magari yasipite.

“Kosa lilikuwa ni kupunguza askari, hapo ndipo wafanyabiashara tulijikusanya na kuweka mawe ili askari wasipite kuja kutuzuia wala magari yasipite,” alisema askari aliyeshudia.

Mtu mwingine aliyejitambulisha kwa jina Juma Mohamed, alisema wanashangaa askari kuendelea na operasheni hiyo kwa kuwa kama ni ujio wa Obama ulishapita, hivyo waruhusiwe kurudi katika maeneo hayo.

Magari ya Makamanda wa Polisi (OCD) wa vituo mbalimbali, ikiwemo Kimara na Kinondoni, yakiwa na Makamanda wao, yalikuja kuongeza nguvu, huku gari jingine la polisi likiwasomba waliokamatwa katika oparesheni hiyo.

Aidha, maeneo ya kuanzia Darajani mpaka soko la Manzese kulikuwa kumewekwa mawe barabarani, huku barabara inayojengwa ikiwa imevunjwa katika baadhi ya maeneo kutokana na vurugu hizo.

Maeneo hayo yote palikuwa kimya, tofauti na siku zote ambapo kunakuwa na biashara mbalimbali zikiendelea, huku polisi wakiwaaamuru watu wanaopita kutembea kwa mwendo wa haraka pamoja na kutosogelea eneo la tukio.

Pia maduka yote katika maeneo hayo yalikuwa yamefungwa na baada ya muda wa mapambano hali ilianza kutulia kuanzia saa 9:00 alasiri.

Operasheni hiyo inaelezwa kulenga kuwaondoa wafanyabiashara wadogowadogo ili kuweza kupisha ukamilishaji wa ujenzi wa Barabara ya Morogoro, inayojengwa kwa ajili ya mabasi yaendayo kasi (DART).

Read more...

USAIN BOLT KUCHEZEA MANCHESTER UNITED!

0 comments
Usain Bolt
Ile ndoto ya gwiji wa mashindano ya kukimbia mita 200, Usain Bolt wa Jamaica,kuchezea timu ya Manchester United,  imeonekana kutimia baada ya kujumuishwa kuwa kati ya wachezaji watakaochezea timu hiyo katika mechi maalum ya kumuenzi  mlinzi mahiri wa timu hiyo,Rio Ferdinand, mwezi Agosti.
Mwanariadha huyo, ambaye inasemekana ndie binadamu mwenye kasi kuliko wote duniani,atakuwepo katika kikosi kitakachomenyana na timu ya Seville kutoka Hispania,katika dimba la Old Trafford, siku ya tarehe 9 mwezi ujao.
"Matamanio yake sasa yatatimia,Bolt atakuwemo kwenye kikosi na kucheza sambamba na Rio.Utakuwa mchezo wa aina yake,kwa kuwa watu watapendeza kuona kama kasi yake inaweza kwenda na uwezo wake wa kumiliki mpira."Kimeongea chanzo cha ndani ya klabu hiyo.
Uteuzi wa Bolt kwenye kikosi hicho unatarajiwa kutangazwa wiki ijayo.
Read more...

Saturday, July 6, 2013

REFA NA MCHEZAJI WAUAWA KINYAMA BRAZIL

0 comments
Baada ya kwisha kwa pilikapilika za Kombe la Mabara nchini Brazil,sambamba na vurugu mitaani,huku nchi hiyo kubwa ya Amerika ya Kusini ikikabiliwa na changamoto nyingine ya kuwa mwenyeji wa mashindano yajayo ya Kombe la Dunia 2014,nchi hiyo imeingia kwenye taswira mbaya-kwa mara nyingine-baada ya kuripotiwa kutokea mauaji ya kutisha ya mchezaji na mwamuzi katika mechi mjini Maranhao ,kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Taarifa zinasema kuwa Otávio Jordão da Silva ambae alikuwa mwamuzi wa mechi hiyo na ambae alikuwa akishambuliwa kwa matusi muda wote wa mechi, alichomoa kisu baada kumaliza mechi na kisha kumchoma nacho mchezaji mmoja mwenye umri wa miaka 31 aitwae Josemir Santos na kumsababishia majeraha ambayo hatimae yalisababisha kifo chake.

Ndugu na marafiki wa mchezaji huyo walipogundua kuwa Santos ameshafariki,walilipiza kisasi kwa kumchoma kisu mwamuzi huyo,ambae baadae kundi la watu liliendelea kumpiga,na kummalizia kwa kumkata vipande vipande na kunyofoa kichwa chake kabla hawajakichomeka kwenye mti na kukiweka kama bendera katikati ya uwanja.
Hakuna taarifa zaidi juu ya tukio hilo, lakini picha zilizowekwa mtandaoni na mtandao wa 101GREAT GOALS zimethibitisha kutokea kwa tukio hilo

Marehemu Josemir Santos Abreu
Read more...

Friday, July 5, 2013

FACEBOOK YAZINDUA HASHTAG

0 comments
Kwa wale watumiaji wa Twitter nadhani wanaelewa inapotajwa HASHTAG...neno ambalo kwa mitandao inaiyotumia huwa ni kama neno linaloweza kuwaunganisha moja kwa moja kuingia kwenye topic (jambo linaloongelewa) inayohusiana nayo ambayo ipo hewani inazungumziwa...ili iwe HASHTAG neno lenyewe lazima lianze na alama (symbol) # na bila kuacha nafasi linafuata neno lenyewe;mfano HASHTAG hii #saidnuhublog...kwahiyo watu wote ambao hujadili Said Nuhu Blog watatumia HASHTAG hii ili kumuunganisha na wengine wanaotaka kuchangia ,huo ni mfano tu...na yeyote ambae yuko mtandaoni akikutana na alama-neno hii,akaibonyeza, basi mtandao utampeleka moja kwa moja kwenye mjadala husika.aidha ataangalia mjadala unavyokwenda au anaweza kuchangia anachojisikia.
Kampuni ya FACEBOOK imezindua matumizi ya HASHTAG kwa ajili ya watumiaji wake wote ikifuata nyayo za kampuni ya Twitter...hatua hii ni jitihada za kampuni hiyo kuboresha huduma zake ili isiachwe nyuma na makampuni mengine,lakini wachunguzi wa mambo ya mitandao ya kijamii wanaona kuwa wazo hili litakuwa na faida zaidi kwa watu wanaotangaza biashara zao kupitia mitandao ya kijamii

CHANZO:THE UNDERCOVER RECRUITER

Read more...

THIAGO ALCANTARA:ANAWEZA ASICHEZEE BARCELONA MSIMU UJAO,USHAHIDI HUU HAPA

0 comments
Miamba ya soka ya Hispania FC Barcelona wametoa wameiondoa taswira ya mchezaji wao Thiago Alcantara kutoka katika picha ya pamoja ya wachezaji wa timu hiyo.Awali kwenye picha hiyo taswira ya Alcantara ilikuwepo kwenye picha hiyo lakini sasa imeondolewa kama ilivyoonekana katika toleo jipya la picha hiyo ndani ya mtandao wa Instalgram katika ukurasa wa timu hiyo jana.

Dogo huyo  amekowa gumzo kubwa kipindi hiki cha usajili wa wachezaji barani Ulaya huku bosi mpya wa Manchester United David Moyes akionesha nia ya kumnyakua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22

chanzo :mirror football
Read more...
 
Said Nuhu © 2012 SAID NUHU BLOGS. BLOG IMETENGENEZWA NA BongoClan blog designer nipigie 0658184797