Edgar
Davis Mosha mtoto wa mfanyabiashara tajiri na maarufu boss wa kampuni
ya DELINA, Bwana Davis Mosha amehojiwa na VOA (Voice of America). Edgar na
baba yake wametua kwa kishindo nchini Marekani wakitokea Uingereza
ambapo Edgar amepeperusha vyema bendera ya Tanzania kwa kuitwa kufanya
majaribio na klabu ya Chelsea ya Uingereza..
HABARI ZAKISIASA
UTAPATA HABARI MBALIMBALI ZA KISIASA KUTOKA NDANI NA NJE YA NCHI, UKIWA HAPAHAPASAID NUHU
HABARI ZA BURUDANI
UKIWA HAPA UTAPATA HABARI ZOTE ZA BURUDANI KUTOKA KILA KONA YA DUNIA...SAID NUHU
HABARI ZA MICHEZO
UKIWA HAPA UTAPATA HABARI ZA KILA AINA YA MICHEZO, KUANZIA MPIRA WA MIGUU, BASKETBALL, GOLF NKSAID NUHU
HABARI ZA KIMATAIFA
HAPA UTAPATA HABARI ZA KIMATAIFA KUTOKA KILA KONA YA DUNIAMore
Sunday, July 28, 2013
WATANZANIA WALIOKAMATWA NA MADAWA HONG KONG WATUMA WARAKA MZITO..WATAJA WAHUSIKA WAKUU..WAMO VIGOGO NA WAFANYABIASHARA MAARUFU
WATANZANIA walio gerezani nchini Hong Kong kwa makosa ya kukutwa wakisafirisha madawa hatari ya kulevya,wametuma waraka mzito kwa wananchi wenzao kuelezea mambo mengi ambayo wananchi wa kawaida hawayajui kuhusu biashara hiyo inayopigwa vita duniani kote,na pia wamewataja wahusika ambao ndio wamiliki wakuu wa biashara hiyo waraka wenyewe ni huu hapa chini..usome kwa makini:
Friday, July 26, 2013
VYAMA VYA USHIRIKA NI MAGENGE YA WEZI-KIKWETE
Rais Kikwete |
Kikwete aliyasema hayo juzi jioni alipokuwa
akizungumza na wananchi baada ya kufungua jengo la kitega uchumi la
Chama cha Ushirika cha Mkoa wa Kagera (KCU), mjini Bukoba.
“Acheni kuwa wachuuzi tu wa kununua na kuuza mazao
ya wananchi na badala yake mjiingize katika shughuli za uwekezaji na
maendeleo ya kwelikweli ya wanachama wenu,” alinena Rais.
“Hapa Kagera ni kitovu cha ushirika na KCU ni
kitovu cha kuboresha na kuleta usasa katika shughuli za ushirika. Siyo
kama vyama vingine ambavyo ni mkusanyiko wa wezi wanaokula waziwazi
mchana bila hata aibu ….wanakula bila kunawa,” alisisitiza.
Rais Kikwete alisema huko nyuma Serikali ilifanya
uamuzi wa kulipa madeni yote ya ushirika nchini ili kuvipunguzia vyama
mzigo wa kujiendesha.
Alisema hata hivyo sasa vyama hivyohivyo, vimeanza
kujitumbukiza tena katika madeni na kwamba hiyo inatokana na kukosa
viongozi waaminifu na waadilifu.
Kabla ya kuzindua jengo hilo, Rais Kikwete aliweka
jiwe la msingi kwenye upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Bukoba ambao
unapanuliwa ili kuufanya kuwa wa kisasa. Kazi hiyo itagharimu Sh21.015
bilioni, itakapokamilika.
Mradi huo wa upanuzi wa uwanja ulianza Februari mwaka jana na unatarajiwa kukamilika Februari mwakani.
Upanuzi huo ukikamilika uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuhudumia wasafiri 500,000 kwa mwaka sawa na wasafiri 150 kwa saa.
Uwanja huo umekuwa ukilalamiwa kuwa ndiyo kikwazo
cha kukosekana kwa huduma za uhakika za usafiri wa anga kati ya Kagera
na mikoa mingine nchini.
Kwa sasa wananchi wengi wa mkoa huo wanaosafiri
lwa ndege, wamekuwa wakiishia katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza na
baadaye kusafiri kwa meli.
HUU NI WARAKA MZITO KWA WATANZANIA KUTOKA KWA KALA JEREMIAH KUHUSU LOWASSA
Msanii wa Hip hop Kala Jeremiah |
TANGAZO KWA UMMA
MIMI KALA JEREMIAH NILIKUWA MSANII WA KWANZA TANZANIA KUMSEMA MHESHIMIWA EDWARD LOWASA KUPITIA WIMBO WANGU UITWAO WIMBO WA TAIFA BAADA YA MHESHIMIWA KUKUMBWA NA KASHFA YA UFISADI WA RICHMOND.KWA KIPINDI KILE KILA MMOJA WETU ALIHAMAKI SANA NA KUONA KWELI MZEE WA WATU NI FISADI.KWENYE WIMBO HUO KUNA MISTARI NILISEMA. mi siyo mwana siasa sisubiri tume ichunguze nistaafu ka Lowasa.
KWA KUWA MIMI NI MZURI SANA KWENYE KUFANYA UCHUNGUZI BINAFSI NILITUMIA MUDA MWINGI SANA KULICHUNGUZA SWALA HILI LA KASHFA HII NA BAADAE NILIGUNDUA KUWA NI SWALA LA KISIASA.NA YALIKUWA NI MAPITO AMBAYO MWANADAMU YOYOTE HUPEWA MUDA WA KUPITIA MAGUMU ILI KUPIMWA IMANI YAKE KWA MUNGU.
BAADA YA KUGUNDUA HAYO MWAKA JANA NILITENGENEZA WIMBO UNAOITWA AZIMIO LA ARUSHA AMBAO UPO KWENYE ALBUM YANGU YA PASAKA AMBAYO IKO SOKONI TOKEA MWAKA JANA. KATIKA WIMBO HUO WA AZIMIO LA ARUSHA NILIANDIKA MISTARI IFUATAYO. walipiga dili waka msakizia lowasa ili kuficha siri kali.NILIANDIKA MSTARI HUU BAADA YA KUFANYA UCHUNGUZI NA KUJIRIDHISHA KUWA MHESHIMIWA NI KIONGOZI BORA SANA NA HASA KWA UAMUZI WAKE WA KUJIUZULU BILA SHINIKIZO KUBWA NA WAKATI KWA NAFASI ALIYOKUWA NAYO YA UWAZIRI MKUU ALIKUWA NA UWEZO WA KUGOMA KUJIUZULU NA HASA KWA KUWA HAKUWA FISADI KAMA ILIVYOSEMWA.
MWEZI WA TATU MWISHONI MWAKA HUU NILITOA WIMBO UNAOKWENDA KWA JINA LA KARIBU DAR AMBAKO NILISEMA dar es salam ingekuwa nchi Rais angekuwa Lowasa huku watu washashtukia kuna mchezo kwenye siasa HAPA NILIKUWA NAMAANISHA KUWA WATU WENGI WANAOISHI DAR WANAWAHI KUJUA MAMBO YA WANASIASA KWA KUWA WANASIASA WANAISHI HUKU LAKINI PIA WATAFITI WENGI WA MAMBO YA KISIASA WANAISHI HUKU KWA HIYO NI RAHISI ZAIDI KUUJUA UKWELI MAPEMA.
NAAMINI KUONDOKA KWA LOWASA KWENYE UWAZIRI MKUU KUMEZOROTESHA MAENDELEO YA TAIFA KWA KIASI FLANI
NDUGU ZANGU WATANZANIA NI WAZI KUWA LOWASA NI JEMBE TENA JEMBE LA KAZI KUMBUKENI BILA LOWASA KUSINGEKUWA NA SHULE ZA KATA TANZANIA,NA ANGEENDELEA KUWEPO MADARAKANI ALIKUWA NA MPANGO WA KUANZA MCHAKATO WA ZAHANATI ZA KATA.IKUMBUKWE PIA LOWASA NDIYE ALIYESIMAMIA UJENZI WA CHUO CHA UDOM TENA KWA PESA ZA KITANZANIA BILA KUOMBAOMBA VIMIKOPO.
MRADI WA MAJI KUTOKA MWANZA KWENDA SHINYANGA NI KAZI YA LOWASA. ZIPO KAZI NYINGI AMBAZO NIKIZITAJA ZOTE NAWEZA KUJAZA UKURASA.NACHOJARIBU KUSEMA HAPA NI KWA KUWA MIMI NI MSANII NA NI KIOO CHA JAMII NINGEOMBA WEWE MWANAJAMII CHUKUA HATUA YA KUFANYA UCHUNGUZI BINAFSI KUHUSU LOWASA.BILA KUFUATA MKUMBO WA KISIASA NAAMINI UTAKUBALIANA NA MIMI KUWA LOWASA NI JEMBE.
MIMI HUWA NAPENDA KUSOMA VITABU VYA WANAHARAKATI NA KUNA KITABU KIMOJA NILIKIPITIA CHA MWANAHARAKATI KUTOKA ITALY AITWAE NICCOLO MACHIAVELLI AMBAYE ALIZALIWA MWAKA 1469 NA KUFARIKI 1527. KATIKA ENZI ZA UHAI WAKE ALIWAHI KUANDIKA VITABU KADHAA LAKINI KATI YA VITABU HIVYO KITABU KIITWACHO THE PRINCE NDICHO KILIMPA HESHIMA KUBWA SANA KWA KUWA ALIIKOSOA SERIKALI YA KIFALME YA KIPINDI HICHO KITU AMBACHO HAKIKUWA RAHISI KWA MTU KUFANYA HASA IKIKUMBUKWA KUWA ENZI ZA UFALME ZILIKUWA ENZI ZA UBABE. KATIKA MANENO KUTOKA KWENYE KITABU HICHO AMBAYO NINGE PENDA KUKUSHIRIKISHA WEWE NDUGU YANGU MTANZANIA NI MANENO YAFUATAYO MACHIAVELLI ALIANDIKA HIVI. kuna kipindi ambacho mataifa yanapita katika vipindi vigumu. na kwa kipindi hicho kigumu mataifa hayo yatahitaji sana kupata kiongozi mwenye kuweza kuchukua maamuzi magumu,na ambaye hatakuwa chini ya sauti ya mtu mwingine, na ambaye ataweza kuyatekeleza maamuzi magumu kwa haraka hata kama ni kwa kuwaumiza wachache ili wengi wawe huru.atakayekuwa tayari kutekeleza jambo baya ili likapita na kusahaulika na atakayetekeleza mambo mazuri kwa muda mrefu na yakaendlea kukumbukwa.kiongozi huyo atatakiwa kuchagua kuogopwa ama kupendwa lakini ni bora akachagua kuogopwa lakini akitenda haki kwa wananchi husika.HAYO NI BAADHI YA MANENO ALIYOANDIKA MACHIAVELLI KWENYE THE PRINCE KITABU AMBACHO KILIMPELEKEA KUITWA NA MFALME NA KUPEWA NAFASI YA JUU YA UONGOZI KATIKA SERIKALI HIYO YA KIFALME.
KWA MAONI YANGU NADHANI TAIFA LETU LIMEPITIA VIPINDI VIGUMU KADHAA NA KWA MANENO YA BWANA MACHIAVELLI NADHANI KIONGOZI ANAYEFAA AMBAYE ANAWEZA AKACHUKUA MAAMUZI MAGUMU NA AMBAYE HAWEZI KUWA CHINI YA SAUTI YA MTU MWINGINE NI MHESHIMIWA EDWARD NGOYAI LOWASA.
tafakari chukua hatua
MIMI KALA JEREMIAH NILIKUWA MSANII WA KWANZA TANZANIA KUMSEMA MHESHIMIWA EDWARD LOWASA KUPITIA WIMBO WANGU UITWAO WIMBO WA TAIFA BAADA YA MHESHIMIWA KUKUMBWA NA KASHFA YA UFISADI WA RICHMOND.KWA KIPINDI KILE KILA MMOJA WETU ALIHAMAKI SANA NA KUONA KWELI MZEE WA WATU NI FISADI.KWENYE WIMBO HUO KUNA MISTARI NILISEMA. mi siyo mwana siasa sisubiri tume ichunguze nistaafu ka Lowasa.
KWA KUWA MIMI NI MZURI SANA KWENYE KUFANYA UCHUNGUZI BINAFSI NILITUMIA MUDA MWINGI SANA KULICHUNGUZA SWALA HILI LA KASHFA HII NA BAADAE NILIGUNDUA KUWA NI SWALA LA KISIASA.NA YALIKUWA NI MAPITO AMBAYO MWANADAMU YOYOTE HUPEWA MUDA WA KUPITIA MAGUMU ILI KUPIMWA IMANI YAKE KWA MUNGU.
BAADA YA KUGUNDUA HAYO MWAKA JANA NILITENGENEZA WIMBO UNAOITWA AZIMIO LA ARUSHA AMBAO UPO KWENYE ALBUM YANGU YA PASAKA AMBAYO IKO SOKONI TOKEA MWAKA JANA. KATIKA WIMBO HUO WA AZIMIO LA ARUSHA NILIANDIKA MISTARI IFUATAYO. walipiga dili waka msakizia lowasa ili kuficha siri kali.NILIANDIKA MSTARI HUU BAADA YA KUFANYA UCHUNGUZI NA KUJIRIDHISHA KUWA MHESHIMIWA NI KIONGOZI BORA SANA NA HASA KWA UAMUZI WAKE WA KUJIUZULU BILA SHINIKIZO KUBWA NA WAKATI KWA NAFASI ALIYOKUWA NAYO YA UWAZIRI MKUU ALIKUWA NA UWEZO WA KUGOMA KUJIUZULU NA HASA KWA KUWA HAKUWA FISADI KAMA ILIVYOSEMWA.
MWEZI WA TATU MWISHONI MWAKA HUU NILITOA WIMBO UNAOKWENDA KWA JINA LA KARIBU DAR AMBAKO NILISEMA dar es salam ingekuwa nchi Rais angekuwa Lowasa huku watu washashtukia kuna mchezo kwenye siasa HAPA NILIKUWA NAMAANISHA KUWA WATU WENGI WANAOISHI DAR WANAWAHI KUJUA MAMBO YA WANASIASA KWA KUWA WANASIASA WANAISHI HUKU LAKINI PIA WATAFITI WENGI WA MAMBO YA KISIASA WANAISHI HUKU KWA HIYO NI RAHISI ZAIDI KUUJUA UKWELI MAPEMA.
NAAMINI KUONDOKA KWA LOWASA KWENYE UWAZIRI MKUU KUMEZOROTESHA MAENDELEO YA TAIFA KWA KIASI FLANI
NDUGU ZANGU WATANZANIA NI WAZI KUWA LOWASA NI JEMBE TENA JEMBE LA KAZI KUMBUKENI BILA LOWASA KUSINGEKUWA NA SHULE ZA KATA TANZANIA,NA ANGEENDELEA KUWEPO MADARAKANI ALIKUWA NA MPANGO WA KUANZA MCHAKATO WA ZAHANATI ZA KATA.IKUMBUKWE PIA LOWASA NDIYE ALIYESIMAMIA UJENZI WA CHUO CHA UDOM TENA KWA PESA ZA KITANZANIA BILA KUOMBAOMBA VIMIKOPO.
MRADI WA MAJI KUTOKA MWANZA KWENDA SHINYANGA NI KAZI YA LOWASA. ZIPO KAZI NYINGI AMBAZO NIKIZITAJA ZOTE NAWEZA KUJAZA UKURASA.NACHOJARIBU KUSEMA HAPA NI KWA KUWA MIMI NI MSANII NA NI KIOO CHA JAMII NINGEOMBA WEWE MWANAJAMII CHUKUA HATUA YA KUFANYA UCHUNGUZI BINAFSI KUHUSU LOWASA.BILA KUFUATA MKUMBO WA KISIASA NAAMINI UTAKUBALIANA NA MIMI KUWA LOWASA NI JEMBE.
MIMI HUWA NAPENDA KUSOMA VITABU VYA WANAHARAKATI NA KUNA KITABU KIMOJA NILIKIPITIA CHA MWANAHARAKATI KUTOKA ITALY AITWAE NICCOLO MACHIAVELLI AMBAYE ALIZALIWA MWAKA 1469 NA KUFARIKI 1527. KATIKA ENZI ZA UHAI WAKE ALIWAHI KUANDIKA VITABU KADHAA LAKINI KATI YA VITABU HIVYO KITABU KIITWACHO THE PRINCE NDICHO KILIMPA HESHIMA KUBWA SANA KWA KUWA ALIIKOSOA SERIKALI YA KIFALME YA KIPINDI HICHO KITU AMBACHO HAKIKUWA RAHISI KWA MTU KUFANYA HASA IKIKUMBUKWA KUWA ENZI ZA UFALME ZILIKUWA ENZI ZA UBABE. KATIKA MANENO KUTOKA KWENYE KITABU HICHO AMBAYO NINGE PENDA KUKUSHIRIKISHA WEWE NDUGU YANGU MTANZANIA NI MANENO YAFUATAYO MACHIAVELLI ALIANDIKA HIVI. kuna kipindi ambacho mataifa yanapita katika vipindi vigumu. na kwa kipindi hicho kigumu mataifa hayo yatahitaji sana kupata kiongozi mwenye kuweza kuchukua maamuzi magumu,na ambaye hatakuwa chini ya sauti ya mtu mwingine, na ambaye ataweza kuyatekeleza maamuzi magumu kwa haraka hata kama ni kwa kuwaumiza wachache ili wengi wawe huru.atakayekuwa tayari kutekeleza jambo baya ili likapita na kusahaulika na atakayetekeleza mambo mazuri kwa muda mrefu na yakaendlea kukumbukwa.kiongozi huyo atatakiwa kuchagua kuogopwa ama kupendwa lakini ni bora akachagua kuogopwa lakini akitenda haki kwa wananchi husika.HAYO NI BAADHI YA MANENO ALIYOANDIKA MACHIAVELLI KWENYE THE PRINCE KITABU AMBACHO KILIMPELEKEA KUITWA NA MFALME NA KUPEWA NAFASI YA JUU YA UONGOZI KATIKA SERIKALI HIYO YA KIFALME.
KWA MAONI YANGU NADHANI TAIFA LETU LIMEPITIA VIPINDI VIGUMU KADHAA NA KWA MANENO YA BWANA MACHIAVELLI NADHANI KIONGOZI ANAYEFAA AMBAYE ANAWEZA AKACHUKUA MAAMUZI MAGUMU NA AMBAYE HAWEZI KUWA CHINI YA SAUTI YA MTU MWINGINE NI MHESHIMIWA EDWARD NGOYAI LOWASA.
tafakari chukua hatua
Monday, July 22, 2013
ORPHANED GIRL BURNT WITH HOT WATER BY HER KEEPER IN AN ARGUMENT OVER DISAPPEARED PART OF FOOD
Dora after after reciving medical treatment |
A twelve years old girl,student of Wazo Hill Primary School in Dar Es Salaam,has claimed that she was burnt with hot water by her niece, Saum Masudi.
The little girl whose name is Dora said she faced that kind of atrocity few days ago in the Wazo area where she lives with Saum, her niece, and keeper after the death of her father.
In her account of the tragedy Dora said that in the morning of that day she woke up early and cleaned the house and in that course visited the den where they keep ducks to clean it.
"After finishing with cleanliness I went inside the main house and found thick porridge which was left over since yesterday.I took few slabs off and gave them to ducks in the den,my sister (niece) was asleep at the time.When she woke up,she found the thick porridge was halved so she demanded to know what happened to the food.I told her that I served some to our ducks.She didn`t believe me,so she pulled me to the den to prove it.At the time we arrive at the den,there was nothing, the food was long been eaten by ducks.She called me a liar,and started to tie my hands and legs together.After that she splashed very hot water around my body."
Dora shows off severity of inflictions she received |
She said she was wounded in different parts of her body and she never received instant medical care after that.After few days the wounds started to rot and stink until the day one of her relatives paid a visit and wanted to shave her untidy hair.In the process the relative told her to take off the T-shirt she was wearing so it doesn`t get covered by her falling hair.That`s when the relative came to the horrific scene of stinking wounds.After recovering from her shock of the day, the relative wanted to know what really happened .Dora explained it all and Dora`s keeper fled the house immediatelly.
Dora poses with her helper Kauthari Isack |
After the news of her miseries broke it`s boundaries,Dora said a good samaritan Kauthari Isack who was emotinally touched by Dora`s story took her to the Police station and then to hospital for medical care.Kauthari confirmed that she helped Dora to hospital after becaming emotinally very touched by her story
"I took her firstly to the police station to get Police Form 3 so she could be accepted by medical staff at the hospital, and people at the police station opened a case no.KW/RB/6034/2013.The search for suspect has just begun and they (police) have husband of the suspect to help the search.
The Kinondoni Regional Police Commander ACP Camillius Wambura has confirmed the incident regarding Dora inflictions and of the ongoing searching of the suspect
"I warn all members of the public, that this kind of cruelty can not be tolerated.People should refrain from doing such things, because we have severe punishment in store for this"
HUU NI UKATILI MKUBWA..YATIMA AMWAGIWA MAJI YA MOTO,KISA KIPORO CHA UGALI!
Mtoto Dora baada ya kupata msaada kutoka kwa msamaria mwema |
Mtoto Dora Juma,12, mwanafunzi wa Shule ya Msingi Wazo Hill, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam imedaiwa ameunguzwa kwa maji ya moto na binamu yake aliyetajwa kwa jina la Saum Masud.
Dora ambaye ni yatima alikutwa na dhahama hiyo hivi karibuni eneo la Wazo Dar alikokuwa akiishi na binamu yake huyo kama mlezi wake baada ya kufiwa na baba yake.
Akisimulia tukio hilo Dora alidai kuwa siku ya tukio aliamka asubuhi kufanya usafi wa uwanja nyumbani na akaingia katika banda la bata kwa ajili ya kulisafisha.
“Baada ya kumaliza usafi niliingia ndani na kukuta kiporo cha ugali nikakata kipande nikawapa bata bandani, wakati huo dada (Saum) alikuwa amelala, alipoamka na kukuta kiporo cha ugali kimekatwa aliniuliza nikamueleza nimewapa bata, hakuamini.
“Akaniambia twende bandani kuangalia kama nasema kweli, tulifika tukakuta bata wameula hali iliyomfanya dada kutoamini, alinifunga mikono na miguu na kuniunguza kwa maji ya moto sehemu mbalimbali mwilini,” alidai Dora.
Mtoto Dora akionesha alivyounguzwa mgongoni kwa kumwagiwa maji ya moto |
“Aliniambia nivue fulana ili nywele zisinidondokee, nilipovua alishangaa kuona nina vidonda mwilini, nilipomueleza mkasa mzima aliwapigia simu ndugu wengine hali iliyofanya dada Saumu kukimbia na kwenda kusikojulikana,” alidai.
Dora alisema alichukuliwa na msamaria mwema aitwaye Kauthari Issack ambaye aliliambia kuwa kweli alimchukua binti huyo baada ya kuguswa na unyama aliofanyiwa.
Mtoto Dora akiwa na msamaria mwema Kauthari Isack |
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni ACP Camillius Wambura amethibitisha mtoto huyo kufanyiwa kitendo hicho na kusakwa mtuhumiwa. “Niwaonye wananchi kwamba ukatili kama huu hauwezi kuvumiliwa, watu wajiepushe nao maana watachukuliwa hatua kali za kisheria,” alionya Kamanda Wambura.
MJANE WA MWANAJESHII ALIEUAWA DARFUR `ATOLEWA NDUKI`
Hata kabla ya maziko askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ), waliouawa Darfur, Sudan hayajafanyika, mchumba wa mmoja wa
wapiganaji hao, Amina Juma ameonja chungu nyingine baada ya kutimuliwa
kwenye nyumba aliyokuwa akiishi na marehemu mwenza wake.
Amina ambaye inadaiwa kuwa alikuwa akiishi na
Fortunatus Msofe aliyekuwa askari katika Kambi ya Msangani, 36KJ Pwani
alisema jana: “Kumekuwa na mzozo wa hali ya juu na ndiyo maana
tumeshindwa hata kufika Uwanja wa Ndege kuupokea mwili na hata kesho
(leo) sidhani kama nitakwenda... kuna mtafaruku mkubwa wa kifamilia.”
Amina Juma |
Baada ya kutimuliwa, Amina ambaye hawakuwahi
kupata mtoto na marehemu Msofe, alilazimika kuondoka kwenye nyumba hiyo
na kwenda Mlandizi kwa wazazi wake.
“Nimeishi na Msofe kwa miaka mitatu, akiwa kambini
mimi niko hapa na wakati mwingine alikuwa analala huku... lakini leo
wamenitimua,” alisema huku akilia.
Habari zilizothibitishwa na baadhi ya waombolezaji
waliokuwa nyumbani kwa marehemu Visiga, Kibaha zinasema baadhi ya
wanandugu walimkana Amina siku chache baada ya kutangazwa vifo hivyo.
Ilidaiwa kwamba Amina alitimuliwa katika nyumba
hiyo Ijumaa iliyopita, saa saba mchana baada ya ndugu watatu wa marehemu
kufika hapo wakitokea Tanga.
Walipofika inadaiwa kuwa walitangaza kusitishwa msiba huo katika nyumba hiyo na kutangaza kutomtambua mke huyo.
Watu hao waliwaeleza waombolezaji kuwa walitumwa
na baba mzazi wa marehemu, Willbad Msofe kutoka Kange, Tanga kufika
Kibaha kusitisha msiba uliokuwa ukiendelea nyumbani kwa mtoto wake huyo.
Inadaiwa pia kuwa katika msafara huo, alikuwapo mdogo wa marehemu ambaye aliwahi kuishi kwa miaka miwili na Amina hapo Visiga.
Ilidaiwa kuwa walipofika nyumbani hapo walionana
na mfiwa, Amina na wazazi wake ambao pamoja na majirani na watu wengine
wengi, walikuwa wakimfariji binti yao huyo.
Mmoja wa waombolezaji alisema baada ya salamu
wanandugu hao walianza kuulizia mali za marehemu na walikuwa wakimuuliza
Amina ambaye aliwaleza kila kitu kilipo na baada ya hapo ndipo
walipomweleza kuwa wametumwa na baba wa marehemu kuwa watu hawatakiwi
kuomboleza kwenye eneo hilo kwani msiba upo Tanga tu ambako ndiko iliko
familia yake.
Alipoulizwa baba wa marehemu, Mzee Msofe alisema:
“Mimi ndiye niliyeagiza nyumba ifungwe na ukweli ninamfahamu Amina,
lakini simtambui kama mkewe kwa kuwa hawajafunga ndoa... Hata wewe si
unayafahamu haya? Uchumba si ndoa na ukifunga ndoa ndipo unatambulika
rasmi,” alisema
WALIVYOISHI NA MAREHEMU
Akiwa kwa wazazi wake Mlandizi jana, Amina alisema:
“Namwachia Mungu maana hayo yote nashangaa
yanatokea wakati huu mume wangu ‘Fortu’ amekufa, mbona kipindi chote cha
miaka mitatu iliyopita familia ya Tanga dada zake na mdogo wake
tuliishi nao vizuri kwangu nilipokuwa na marehemu? Nimeishi na ndugu
wote lakini hawakuwahi kuhoji, hata nilipokwenda na mume wangu Kange
baba na mama Msofe nilikaa nao zaidi ya wiki na hawakunikana, ila
nashangaa,” alisema na kulia kwa uchungu.
Akizungumzia kitendo hicho, baba yake Amina, Juma
Juma alisema: “Nimeshangaa hizi taarifa. Tulikuwa tunajiandaa kupokea
msiba wa mwanetu, lakini leo yanakuja mengine kwa kweli imetushangaza
sana.”
“Nasubiri baada ya kumzika marehemu, nitazungumza
nao... Kinachonishangaza ni kwamba walituandikia barua ya kumposa binti
yangu na tukawajibu na gharama zilikuwa Sh1.2 milioni... Tutazungumza,
ngoja hili lipite kwanza,” alisema mzee Juma.
WALIVYOISHI NA MAREHEMU
Akisimulia maisha yao, Amina alisema: “Tulianza
kuishi Mbezi Luis mwaka 2010 katika nyumba ya kupanga na nikamshawishi
tununue kiwanja na kwa kuwa mimi ni mwenyeji wa Kibaha, niliwatumia
marafiki wa familia yangu Mlandizi wakatafutia eneo na mwaka 2011
tulipata na tukaanza ujenzi.
“Tukiwa Mbezi, tulianza kufyatua matofali kisha
ujenzi ukaanza Visiga mwaka 2012 mwanzoni na Septemba mwaka huo
tulihamia kwenye nyumba yetu na hapo ndiyo ilikuwa makazi yetu hadi
marehemu anaondoka kwenda Darfur.
“Wakati wote huo ‘Fortu’ alikuwa keshaniposa na
hata barua zote za posa zipo na tulikuwa tukisubiri utaratibu wa kijeshi
marehemu kukamilisha miaka sita ya kukaa kambini kisheria ndipo
aruhusiwe kuoa.
“Fortu alikamilisha miaka hiyo mwaka 2012 mwishoni
na wakati akijiandaa kwa kufunga ndoa ndipo ikatokea safari ya Darfur
mwanzoni mwa mwaka huu na tukakubaliana tusitishe kwanza akirudi
tukamilishe, lakini haikuwa.... Halafu wananifukuza wanasema hawanijui,”
alieleza huku akiangua kilio.
CHANZO:GAZETI LA MWANANCHI
CHANZO:GAZETI LA MWANANCHI
Sunday, July 21, 2013
SHILOLE AFANYA MAHOJIANO NA `TAKE ONE` NYUMBANI KWA DIAMOND
Mtangazaji
wa Clouds Tv, Zamaradi Mketema, alikuwa nyumbani kwa msanii wa muziki wa
kizazi kipya (Bongoflava)Nasib Abdul (Diamond Platinumz) ambako msanii
huyo alikuwa akifuturisha.Bi Mketema alipata wasaa wa kumhoji msanii
mwingine katika tasnia hiyo ya muziki Zuwena Mohamed`Shilole`.Mahhojiano
hayo yalikuwa mahsusi kwa kipindi cha TAKE ONE cha Clouds Tv
kinachoendeshwa na Bi Mketema.Watu hao wawili walikuwa ni sehemu ya watu
kadhaa walioalikwa kwa ajili ya kufuturu nyumbani kwa Diamond.
Katika mahojiano hayo
ambayo yanatarajiwa kurushwa hewani na Clouds Tv siku ya Jumanne hii saa
3.30 usiku,Shilole amelezea faida alizopata kama msanii katika safari
yake nchini Marekani,na pia matarajio yake baada ya safari hiyo,ikiwamo
ya kufanya kazi na msanii mmoja mkubwa wa nchi hiyo.
NUSU YA WAZAZI WA KIUME NCHINI WANALEA WATOTO WA KUBAMBIKIWA
Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali nchini imesema karibu
nusu ya watu waliojitokeza kupima vinasaba (DNA) ili kubaini uhalali wa
watoto wao, vipimo vimeonesha si wazazi halisi wa watoto waliopimwa.
Takwimu
hizo ni kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2010, ikionesha
kuwa, asilimia 48.32 ya wazazi 'wanalea' watoto wasio wa kwao wakati
asilimia 51.68 ndio wazazi halali.
Hayo yameelezwa jana na Mkuu wa
Kitengo cha Makosa ya Jinai, Vinasaba na Baiolojia wa ofisi hiyo, Gloria
Machuve katika mkutano na wanahabari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari
(MAELEZO), Dar es Salaam.
Ingawa hakutaja idadi kamili ya
waliojitokeza kupima DNA, alisema idadi hutofautiana mwaka hadi mwaka.
Ili kufanya vipimo vya DNA, wazazi hulazimika kulipia Sh 100,000.
Machuve alisema kazi ya DNA si kutambua watoto halali na wasio halali pekee, bali vipimo hivyo vina umuhimu mkubwa kwa jamii.
Alitoa
mfano kuwa, matumizi ya Teknolojia ya vinasaba vya binadamu yamewezesha
kesi mbili za mauaji ya vikongwe na albino kutolewa hukumu katika mikoa
ya Shinyanga, Kagera na Sumbawanga baada ya kufanyika kwa uchunguzi
katika matukio manane.
Aidha, alisema katika majanga mbalimbali yaliyokumba nchi ikiwa pamoja na milipuko ya mabomu yaliyotokea Mbagala, Dar es Salaam mwaka 2010 walitambua mabaki ya askari sita ambao baadaye walichukuliwa na ndugu zao na kuzikwa.
Alitolea pia mfano wa tukio
la moto katika Shule ya wasichana ya Idodi mkoani Iringa ambako licha ya
kuungua vibaya, miili ya wanafunzi 12 ilitambuliwa hivyo makaburi yao
kutambuliwa. Katika Jengo la ghorofa lililoporomoka mtaa wa Kisutu mwaka
huu, marehemu 23 walitambulika.
Aidha, katika ajali ya Ndege ya
Comoro mwaka 2010 mabaki ya miili ya marehemu 25 ilitambuliwa huku
katika masuala ya uhamiaji teknolojia hiyo ilitumika kudhihirisha hawana
uhusiano na wananchi wa Tanzania.
Machuve alisema katika masuala ya ubakaji na mimba za utotoni teknolojia hiyo imesaidia kuwa fikisha wahusika mahakamani pamoja na katika wizi wa kutumia silaha.
WAENDA JELA KWA KUPOST NYAMA YA NGURUWE NA KEJELI KWENYE FACEBOOK WAKATI WA MFUNGO
Alvin Tan na Vivian Lee wakiwa chini ya ulinzi |
Wamiliki wa Blog moja inayojihusisha na masuala ya ngono Alvin Tan na Vivian Lee wamefunguliwa mashtaka na kuwekwa ndani bila ya dhamana nchini Malaysia baada ya kuweka picha inayowakosea waumini wa kiislam kwenye Facebook.Wanakabiliwa na adhabu ya kifungo cha miaka minane jela.
Alvin na Vivian kwenye picha iliyowaponza ambayo ina ujumbe unaotafsirika kama"Futari njema furahi na nyama ya nguruwe,harufu nzuri, tamu, inayotia hamu ya kula" |
Picha iliyowaponza ilikuwa ikiwaonesha wakila nyama ya nguruwe ikiwa na ujumbe wa kuwatakia waislam ramadhan njema.Mamlaka inayosimamia sheria nchini humo imelichukulia tuko hilo kuwa ni kosa kubwa,ikizingatiwa kuwa nyama ya nguruwe ni haram (hairuhusiwi) kwa waumini wa kiislam.Ingawa watu hao walijitetea kuwa walilenga katika kuonesha ucheshi wao,imechukuliwa kuwa inawavunjia heshima baadhi ya watu katika jamii na pia kuzingatia na kazi wanayojihusisha nayo wakosaji pia si nzuri ambapo wamekuwa wakiweka video za ngono kwenye ukurasa wao wa Youtube uitwao `Sexcussions with Alvin` na pia wanamiliki blog inayoegemea kwenye masuala ya ngono.
Picha za ngono ni marufuku kwenye nchi za Malaysia na Singapore,hivyo tukio hilo limesababisha Tan mwanafunzi wa sheria Chuo Kikuu cha Malaysia kunyang`nywa hati za masomo ya juu (Scholarship) ya nchi za ASEAN,baada ya malalamiko ya wananchi dhidi ya blog yao.
Tan na Lee wameshakana mashtaka yao na wamewekwa ndani bila dhamana hadi kesi yao itakapoanza kusikilizwa Agosti 23 mwaka huu.Baada ya tukio hilo waliomba radhi kwenye ukurasa wao wa Youtube kwa kusema:
"Tunarekodi video hii ili kuwaomba radhi waumini wa kiislam kwa kuwa tumewakosea kwenye mwezi huu mtukufu wa Ramadhan"
Wednesday, July 17, 2013
BREAKING NEWS:LUKUMAY WA KLABU MASAI AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI
LUKUMAY (kulia)enzi za uhai wake |
Habari nilizozipata
muda mchache uliopita ambazo zimethibitishwa na ndugu na jamaa wa karibu
zinasema Benedict Charles Lukumay amefariki kwa ajali ya gari eneo la
Mikumi mkoani Morogoro usiku huu.
Chanzo cha kifo chake kimeelezwa kuwa ni ajali ya gari iliyotokea eneo la Mikumi mkoani Morogoro majira ya saa mbili usiku. Meneja mkuu wa Meridian Hotel LTD Mzee Mponda amethibitisha juu ya kifo hicho, huku huku akisema kuwa ilitokana na ajali ya gari.
"Wakiwa na mwenzake aliyefahamika kwa jina la Adrian na gari binafsi wakielekea mkoani Iringa gari aliyokuwamo marehemu iligonga nyuma ya roli lililokuwa limesimama njiani." alisema Mzee Mponda.
Adrian ambaye ndiye aliyekuwa anaendesha gari alinusurika kwenye ajali hiyo.
Benedict alikuwa ni mmoja kati ya Wakurugenzi watendaji wa kampuni ya Meridian Hotel LTD inayomiliki na kuendesha kumbi za burudani zikiwemo Masai Kinondoni, Masai Ilala na Masai Galapo Ilala.
Kifo
chake kimeacha pengo kubwa si tu kwa familia bali hata wapenda
burudani, akifahamika kimchango katika kusimamia na kuendeleza burudani
na yakiwemo maonyesho mbalimbali ya wanamuziki wa bongo fleva na fani
nyinginezo.
Mungu alaze Pema ROHO ya Marehemu Ben..
MKONGWE GEORGE MASATU ALILIA KURUDI SIMBA
ALIYEKUWA mchezaji wa Simba miaka kumi na tano iliyopita George Magere Masatu, amesema kuwa kwa sasa yuko tayari kurejea kwenye timu hiyo.
Masatu hivi sasa amerejea nchini akiwa tayari amestaafu soka lakini ana kadi ya uanachama wa timu hiyo yenye maskani yake Msimbazi jijini Dar es Salaam.
Masatu amesema kuwa yuko tayari kurejea kama kocha na siyo mchezaji tena kama ilivyokuwa awali Masatu alisema kuwa, ana uwezo na uzoefu kufundisha aliyoupatia katika shule ya soka ya Arsenal huko Indonesia alikokuwa akicheza soka la kulipwa kwa zaidi ya miaka mitano.
“Kweli nimerudi nyumbani kuendelea na maisha, lakini ukisema kuhusu Simba mimi ni mwanachama.Na kama wakisema nifanye nao kazi,niko tayari haina shida
“Nimekuwa kocha kwenye shule ya watoto ya Arsenal kule Indonesia kwa zaidi ya miaka mitatu. Ninajua kazi inavyofanyika na wakisema wanataka tufanye kazi, basi tutafanya hivyo,” alisema Masatu aliyekuwa beki kisiki wakati wa enzi zake.
Masatu alianza kufanya vizuri akiwa na Pamba ya Mwanza kabla ya kujiunga na Simba mwanzoni mwa miaka ya 1990.
Pamoja na kuwa na umbo dogo, Masatu alikuwa ndiye beki nyota na imara zaidi wa kati nchini na jina lake halijawahi kushuka chati pamoja na kuwa nje ya Tanzania kwa muda mrefu.
BAN KI MOON ALAANI MAUAJI YA WANAJESHI WA TANZANIA DARFUR
Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UNO), Ban K-Moon(pichani), amesema
amesikitishwa na kuhuzunishwa na mauaji ya askari saba wa Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ), lililofanywa na waasi wa Sudan Julai 13, mwaka huu.
Askari
hao wa JWTZ waliokuwa Darfur, Sudan ya Kusini kulinda amani kwa mujibu
wa UNO, walishambuliwa na waasi hao karibu na kambi ya Manawashi eneo la
Khor Abeche, mji wa Darfur Jimbo la Nyala ambapo pia askari wengine 17
walijeruhiwa baadhi yao vibaya.
Katika
salamu zake hizo kupitia kwa Msemaji wake, Katibu Mkuu huyo wa Uno,
ameelezea masikitiko yake kuhusiana na vifo hivyo na kutoa pole kwa
familia za marehemu waliokuwa wakilinda amani, Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Vikosi vya Umoja wa Afrika kwa Umoja wa Mataifa vya Kulinda
Amani (Unamid).
Ban
K-Moon amelaani shambulio hilo dhidi ya Unamid na kuelezea matumaini
yake kwamba Serikali ya Sudan itachukua hatua zinazofaa kuhakikisha
kwamba wahusika wanafikishwa mbele ya sheria.
Wakati
huo huo, Taarifa iliyotolewa na Unamid juzi jioni ilisema wajumbe wa
Baraza la Usalama wanalaani kwa nguvu zote mashumbulizi hayo dhidi ya
askari wa vikosi vya Unamid.
"Wajumbe
wa Baraza la Usalama wameelezea masikitiko yao na kutuma salamu za pole
kwa familia za marehemu hao pamoja na kwa Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Aidha, wameitaka Sudan kufanya upelelezi wa kina kuhusiana na tukio hilo na kuwafikisha wahalifu hao mbele ya mkono wa sheria.
Taarifa hiyo ya Unimad
iliongeza kuwa shambulio lolote dhidi ya vikosi vya Unimad halikubaliki
na kuonya kuwa lisitokee tena shambulio lingine la aina hiyo huku
ikisisitiza pande zinazovutana Darfur kushirikiana kwa lengo la kufikia
malengo yaliyokusudiwa.
USHINDI WA ARSENAL WAFANYIWA PROPAGANDA ZA KISIASA INDONESIA
Sege Gnaby wa Arsenal akikwepa daruga la mchezaji wa Indonesia, Roby |
Mgombea urais katika uchaguzi wa Rais wa 2014 kupitia Chama cha Great Indonesia Movement Party (Gerindra) Jenerali mstahafu Prabowo Subianto ameutumia mchezo kati ya timu ya taifa ya nchi hiyo na Arsenal kuishambulia serikali iliyo madarakani katika hotuba ya mkutano wa Kampeni za uchaguzi wa Rais wa nchi hiyo wa mwaka 2014
Baada ya timu ya taifa ya Indonesia kupokea kipigo cha goili 7-0 kutoka Gunners mgombea Prabowo aliilaumu serikali kwa kutoisimamia vizuri timu hiyo na kuahidi iwapo ataingia madarakani kama rais wa Indonesia atahakikisha kikosi cha timu ya taifa kinafanya vizuri katika mechi zake
"
Iweje hata timu yetu ya taifa inashindwa kwenye mechi na wachezaji 11 wa ngazi ya klabu.Tutahakikisha tunalipa umuhimu wa pekee suala zima la timu ya taifa.Kwa hiyo ninachofikiri ni kwamba matatizo haya yanasababishwa na udhaifu katika uendeshaji,na uwezo mdogo wa kufikiri.Matatizo katika uongozi.Tunataka Indonesia iwe na timu ya taifa iliyo imara"
Jenerali Prabowo ambaye aliwahi kuwa askari wa kikosi maalum,aliwahi kuwania kiti cha umakamu wa rais 2009 ambapo alibwagwa na mpinzani wake Megawati Sukamoputri.Ni mmoja kati ya wagombea wanaopewa nafasi kubwa ya kuingia ikulu ya nchi hiyo ya mashariki ya mbali 2014
ASKARI POLISI AELEZEA KILICHOTOKEA KATIKA SHAMBULIO LA DARFUR
Askari wa JWTZ walionusurika wakiwa Hospitali |
WAKATI Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), likiwa
bado halijatangaza rasmi majina ya wapiganaji wake waliofariki huko
Sudan, askari polisi aliyeko huko ameeleza chanzo na mazingira ya tukio
hilo. Wapiganaji saba na wengine 14 walijeruhiwa Jumamosi iliyopita.
Askari polisi huyo anayefanya kazi katika Mji wa Nyala uliopo Darfur, alisema mauaji hayo yalitokea wakati askari hao walipokuwa wakifuatilia magari yao yaliyokuwa yameporwa na kundi mojawapo la waasi.
Usalama katika Mji wa Nyala ambao ndiyo mkubwa zaidi katika eneo la Darfur, umekuwa mdogo katika siku za hivi karibuni. “Wale wanajeshi walikuwa doria ya kawaida, ila kama wiki moja iliyopita waasi walivamia tena doria ya wanajeshi wetu na kupora magari manne bila kuua mtu.
Askari polisi huyo anayefanya kazi katika Mji wa Nyala uliopo Darfur, alisema mauaji hayo yalitokea wakati askari hao walipokuwa wakifuatilia magari yao yaliyokuwa yameporwa na kundi mojawapo la waasi.
Usalama katika Mji wa Nyala ambao ndiyo mkubwa zaidi katika eneo la Darfur, umekuwa mdogo katika siku za hivi karibuni. “Wale wanajeshi walikuwa doria ya kawaida, ila kama wiki moja iliyopita waasi walivamia tena doria ya wanajeshi wetu na kupora magari manne bila kuua mtu.
Miili ya askari wa JWTZ waliouawa Darfur ikipewa heshima za mwisho |
“Siku ya mauaji hayo wanajeshi wetu wakiwa tena katika doria
waliyaona yale magari yaliyoporwa kwa mbali yamepaki, waliyafuatilia,
walipokaribia kumbe ulikuwa mtego, wakashambuliwa,” alisema askari huyo
na kuongeza: “Mauaji hayo yametokea takriban kilometa 70 kutoka katika
kambi niliyopo mimi, lakini wote tupo eneo la kusini na hiyo kambi ya
Korabeche inaongozwa na jeshi letu.”
Tofauti na chanzo chetu cha habari huko Darfur, Kanali Mgawe alisema
wanajeshi hao walishambuliwa walipokuwa kwenye msafara wa kusindikiza
walinzi wa amani.
Askari huyo aliyeko Darfur alisema: “Makundi yanayopambana huku yapo mengi ila makubwa yapo kama matano. Kuna moja linaitwa Jeshi la Ukombozi la Watu wa Sudan (SPLA), ambalo limegawanyika katika makundi mawili pia kuna mengine kama JEM, Janjaweed na mengineyo.”
Askari huyo aliyeko Darfur alisema: “Makundi yanayopambana huku yapo mengi ila makubwa yapo kama matano. Kuna moja linaitwa Jeshi la Ukombozi la Watu wa Sudan (SPLA), ambalo limegawanyika katika makundi mawili pia kuna mengine kama JEM, Janjaweed na mengineyo.”
Akizungumzia mshtuko walioupata baada ya mauaji hayo, askari huyo
alisema wafanyakazi wote wanaohusika na ulinzi wa amani wamepatwa na
ganzi… “Huku kwa kweli hali imekuwa chungu, tangu askari hao wauawe hali
haitabiriki kabisa, tupo nje hapa (hospitali walimohifadhiwa),
tunasubiri uhakika.”
“Hawa jamaa (waasi), wamesheheni silaha na wana vifaa vya kisasa
kiasi kwamba hata ndugu zetu walizidiwa kutokana na wenzao kuwa na
silaha nzito, nikija Tanzania nitakuonyesha picha za mapambano yao,”
alisema.
Akizungumzia kazi ambazo polisi wanazifanya huko, alisema
hawaruhusiwi kushika silaha, bali kuwashirikisha wananchi katika masuala
ya amani.
“Sisi majukumu yetu ni kuungana na jamii na kuwafundisha masuala
mbalimbali, hivyo sisi tunawasiliana moja kwa moja na wananchi
waliopoteza makazi kisha tunaandaa taarifa. Haturuhusiwi kushika silaha,
wanajeshi wao wanatulinda na kusimamia usalama na kutusindikiza wakati
wa doria,” alisema.
“Huku hali ya usalama haitabiriki. Mpaka sokoni tunakwenda chini ya ulinzi.”
Akizungumza kwa simu jana, Kanali Mgawe alikanusha uvumi wa majina
yaliyosambaa mitandaoni huku akisema kwa utaratibu uliopo, jeshi
haliwezi kutangaza majina hayo hadi ndugu watakapotaarifiwa. “Hayo
majina yanayotajwa kwenye mitandao ni ya uongo. Kwa sasa mimi sijaletewa
majina na utaratibu uliopo ni hadi ‘next of kin’ (ndugu) wao wajulishwe
kwanza,” alidai Kanali Mgawe.
Hata hivyo, alisema Tanzania imewasilisha maombi ya kubadilisha
kanuni za kulinda amani ikitaka kuruhusiwa kujihami kwa silaha za moto
pale wanajeshi wake wanaposhambuliwa kwa kutumia kanuni namba saba ya
Sheria za Majeshi ya Kulinda
VITAMBULISHO VYA TAIFA:MAMLAKA YAANZA KUCHUKUA ALAMA ZA VIDOLE,SAINI NA PICHA
Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (Nida), imeanza zoezi la kuchukua alama za vidole
vyote kumi, kupiga picha na kuweka saini ya kielektroniki kwa wakazi wa
Wilaya ya Temeke tayari kwa kutoa vitambulisho hivyo.
Kaimu Mkuu wa Mawasiliano na Machapisho, Thomas
William aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, kutokana na wingi wa
watu katika Jiji la Dar es Salaam, zoezi hilo limegawanywa katika ngazi
ya wilaya hadi wilaya.
“Hili zoezi tumelianza juzi, tunachukua alama za
vidole kumi, kupiga picha na kuweka saini za kielektroniki kwa wakazi wa
Temeke, tumeanzia Kigamboni na kutokana na ukubwa wake tumeigawanya kwa
kanda saba,” alisema.
William alisema, kanda ya kwanza inahusisha
mitaa yote katika kata za Kimbiji, Pemba Mnazi, Kigamboni, Vijibweni,
Kibada, Mji Mwema, Somangila, Kisarawe 11, Tungi na mitaa ya Mtoni
Kijichi, Mgeni nani na Misheni iliyoko katika Kata ya Kijichi.
Alisema, ili kuboresha mwonekano mzuri wa picha
kwenye kitambulisho hicho, mwombaji anashauriwa kutokuvaa nguo nyeupe,
kijivu, bluu mpauko, pinki na kofia au kapelo wakati wa kupiga picha.
Aidha, William aliwataka waajiri wa mashirika
mbalimbali kuwaruhusu watumishi kushiriki katika zoezi hilo siku
watakayokuwa wamepangiwa ili kurahisisha zoezi hilo na kuepuka usumbufu
wa kurudia eneo.
“Tunawaomba waajiri katika mashirika mbalimbali
nchini wawaruhusu watumishi wao kufika katika eneo muhimu kwa kuzingatia
tarehe aliyopangiwa ili kufanikisha zoezi. Hata wale ambao walikuwa
hawajajaza fomu za kujiandikisha wanatakiwa kufika katika kata zao ikiwa
zoezi linafanyika katika halmashauri hiyo,” alisema William.
Alisema, zoezi hilo limetoa kipaumbele kwa makundi
maalumu ya walemavu na wazee wasiojiweza na kuwa walemavu wa mikono
watapigwa picha bila kuchukuliwa alama za vidole.
Katika Jiji
la Dar es Salaam, zoezi hilo limeanzia Wilaya ya Temeke, likifuatiwa na Ilala na kumalizikia Kinondoni
la Dar es Salaam, zoezi hilo limeanzia Wilaya ya Temeke, likifuatiwa na Ilala na kumalizikia Kinondoni
Sunday, July 14, 2013
MUNGU KAINGILIA KATI?MALAIKA JIBRIL(GABRIEL)`AONEKANA KWENYE MAANDAMANO` MISRI
Waandamanaji wanaomuunga mkono Rais Morsi,wamedai kuwa wameona mwanga wa aina yake..
Kwa mujibu wa gazeti la Al Arabia,taarifa hizi zimetolewa na muhubiri mmoja anayeegemea upande wa Morsi,wakati akiwahutubia wafuasi wa Morsi katika viwanja vya Rabia all-Adawiya jijini Kairo,
Katika hotuba hiyo iliyorushwa na vituo kadhaa vya televisheni vya Misri,muhubiri huyo amesema kuwa malaika Jibril ameonekana miongoni mwa wafuasi wa Morsi wanaoandamana
Muhubiri huyo Sheikh Ahmad Abdel Hadi kutoka kikundi cha Muslim Brotherhood amesisitiza kuwa watu wanaoheshimika kutoka Madina Al-Munawara, Saudi Arabia, wamemueleza kuhusu ndoto malaika Jibril alivyotokea na kuingia kwenye msikiti wa Rabia aL-Adawiya na kuwataka watu wanaoswali wakae kama walivyo.
Vile vile kuna taswira nyingine ilyotokea ya Mtume Muhammad(SAW)amejumuika na Bw Morsi na watu kadhaa.Katika taswira hiyo anasema muda wa swala ulipofika,watu walimuomba Muhammad(SAW)aongoze swala lakini Mtume alimteua Morsi aongoze swala
Muhubiri huyo amesema mtu mwingine wa kuaminika ametokewa na taswira inayoonesha ngamia wapatao 50,pamoja na vijana nawatoto kadhaa wakiwa jangwani.Baada ya muda wale ngamia,vijana na watoto wakaanza kusikia kiu kali.Walianzakuswali kumuomba Mungu awasaidie na papo hapo ardhi aligawanyika na che chem ya maji ikatokea.Baada ya kumaliza kiu yao,sauti ikasikika ikiwaambia vijana `watunzeni ngamia wa Rais Mohammed Morsi`
Wakati huo huo Sheikh Mosad Anwar wa Misri amemfananisha Morsi na Nabii Yusuf,kwa kuwa wote wametawala baada ya kupitia misukosuko kwa miaka mingi ikiwa pamoja na kuwekwa kizuizini mara kwa mara
Katika hatua nyingine Sheikh Shawki Abdel Latif mwakilishi wa Wizara ya Awqaf(Kusimamia Msaada ya Kijamii)ameibeza kauli ya muhubiri Abdel Hadi kwa kusema kuwa "..ndoto kama hizo zimelenga katika kuhalalisha vitu visivyofaa vionekane kuwa vinafaa,Wanaweka sumu kwenye asali kwa kuongea uongo juu ya Mtume Muhammad,amani iwe juu yake"
Shekh huyo alipoulizwa zaidi na gazeti la Al Arabiya kuhusu uwezekano wa malaika Jibril kutokea katika msikiti wa Rabia al-Alawiya alijibu:"Huo ni uongo pia,Jibril ni Malaika na hutokea mbele ya Mtume wa Mungu tu"
"Maneno kama hayo ni njia ya kujaribu kutumia dini kwa manufaa ya kisiasa na kutaka kuhalalisha utawala wa Rais Morsi" Aliongeza Sheikh Abdel Latif
Sheikh Abdel Latif hakuishia hapo,alipendekeza kukamatwa kwa watu wanaoeneza habari kuhusu ndoto ya Mtume Muhammad akimwambia Morsi aongoze swala kwani kauli hiyo ni `tusi` kwa Uislam na Mtume mwenyewe
Makumi Elfu ya waandamanaji wanaomuunga mkono Rais Morsi walimiminika mitaani kwa wingi kuanzia juzi Ijumaa,wakiapa kupambana ili BwMorsi arejeshwe madarakani huku watu wanaounga mkono kupinduliwa kwa Rais Morsi wakiendelea na maandamano na kuweka pabaya mustakabali wa kisiasa wa Misri.
Chama cha Muslim Brotherhood,alikotokea Rais Morsi kinazidi kusambaratika kufuatia kukamatwa kwa viongozi waandamizi kadhaa na wengine kukimbilia kusikojulikana kufuatia mapinduzi ya Julai 3,ambayo chama hicho na wafuasi wake kimeyaita ni ya kijeshi.
Milio ya risasi katika eneo la jeshi jumatatu ya mwanzoni mwa wiki inayokwisha,imewaacha makumi ya watu wakipoteza maisha yao na wengine makumi kujeruhiwa kulingana na takwimu za Wizara ya Afya ya nchi hiyo
Subscribe to:
Posts (Atom)